Dr. Slaa alisema kweli, ccm ndiyo chanzo cha machafuko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa alisema kweli, ccm ndiyo chanzo cha machafuko

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by DOUGLAS SALLU, Nov 1, 2010.

 1. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,745
  Trophy Points: 280
  Akijibu swali la muulizaji mmoja siku ya mdahalo,Dr Slaa alisema kamwe vyama vya upinzani haviwezi kusababisha vurugu katika nchi hii na badala yake ni CCM na vyombo vyake ndiyo inaweza kuwa chanzo cha vurugu. Uchaguzi ulifanyika nchi nzima jana , pamoja na mapungufu na dalili zote za uchakachuaji lakini zoezi la upigaji kura lilikamilika jana saa 10 jioni. Ni matarajio ya kila mpiga kura kupata matokeo ya kura aliyopiga siku ya jana, na kwa ngazi ya udiwani na ubunge kazi ya kuhesabu na kujumlisha kura hizo ilishakamilika tangu jana usiku, sasa kitendo cha kuzuia kutangaza matokeo ambayo tayari watu wanayajua ni sawa na kuwachokoza watu ili watakapokosa uvumilivu mabomu na risasi zitunike kuwatuliza. Siku zote inapotokea matumizi ya ya nguvu lazima yanaishia kwenye umwagaji wa damu.Hivi sasa kwenye majimbo karibu yote ambayo upinzani wameshinda matokeo yamezuiliwa kutangazwa, hii ndiyo mwanzo wa vurugu, chanzo ikiwa ni CCM kutokubali kushindwa. Ni aibu kwa chama kilichokaa madarakani miaka 50, kikiwa na msaada wa vyombo vyote vya dola, kikiwa uwezo mkubwa wa kifedha unaolingana na serikali kutaka kudhulumu vyama vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi huu kwa mazingira magumu. WITO KWA KIKWETE NA CCM YAKE: IOKOE TANZANIA NA MACHAFUKO AMBAYO DHAHIRI YAKO MLANGONI.
   
Loading...