THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Ushahidi unajidhihirisha Mbowe hakuwa akichukia mafisadi wala ufisadi bali yeye pamoja na baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliburuzwa tu kufanya hivyo na Dr. Slaa.
Baada ya Dr. Slaa kuondoka Mbowe na wenzake wameamua kuonesha sura zao kamili dhidi ya ufisadi watanzania wameona na dunia nzima imeona.
Dr. Slaa aliondoka na Lowassa kuingia kwa mfano ule wa Wayahudi kuchagua afunguliwe nani kati ya Baraba na Yesu. Mpaka sasa sababu za kumtaka Lowassa dhidi ya Dr Slaa ni fumbo la imani ndani ya CHADEMA.
Baada tu ya kufanikiwa kumuondosha Dr. Slaa na kumkabidhi chama Lowassa ndipo chama kilipotangaza misimamo yake mipya na inayokinzana sana na ile ya mwanzo.
Chama kupitia Lowassa kilipiga marufuku kuwasema hovyo mafisadi. Kilisema ukiwa na ushahidi wa fisadi upeleke mahakamani kama huwezi funga mdomo wako.
Na sasa Mbowe ameenda mbali zaidi na kutangazia umma kuwa kinyume na hatua yoyote ambayo Magufuli ataichukua dhidi ya mafisadi. Mbowe ameamua kutetea maslahi ya mafisadi kwa nguvu zake zote.
Awali Magufuli alipoanza kuchukua hatua dhidi ya wakwepa kodi Lowassa alisema anaonea wanachadema. Yani alimaanisha wanachadema ni wakwepa kodi na hawapaswi kubugudhiwa wakifanya hivyo.
Huu ni ushahidi tosha kwamba ile misimamo ya awali haikutoka kwa Mbowe bali kwa kinara wa vita dhidi ya ufisadi Dr. Wilbrod Peter Slaa.
Uishi maisha marefu Dr Slaa.