Dr. Slaa alakiwa na Familia ya Nyerere Butiama

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,488
2,000
Viongozi wakuu wa UKAWA wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa wametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa kijijini Butiama.

Mara baada ya kufika viongozi hao walilakiwa kwa shangwe na wanafamilia ya Mwalimu Nyerere ambapo walikaribishwa kwa mazungumzo mafupi kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Mwalimu Nyerere.

Baada ya mazungumzo hayo ya Faragha waliongozwa kwenda katika kaburi la Baba wa Taifa na kuweka mashada ya maua.

Wakizungumza baada ya mazungumzo hayo wanafamilia hiyo ya Nyerere wameungana na UKAWA kutaka maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Jaji Warioba katika Rasimu ya Katiba yaheshimiwe.

Mmoja wa wanaukoo wa Nyerere akihojiwa amesema ni ulevi tu wa madaraka kupuuza maoni ya wananchi na kumtusi warioba.

Source:ITV Habari/Mitandao.
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938

Source:ITV Habari.

ITV hawakuonyesha hapo kwenye RED. Acheni kuwalisha maneno wanafamilia ya mwalimu.
 
LOMAYANN

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,165
1,250
Hawa waajiriwa wa Lumumba wanahitaji msaada maana nimegundua wengi ni hamnazo kabisa wanasubiri tu m/kiti anasema nini
we have to handle this guys careful because they just carry message no more reasoning in them
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,297
2,000
Mie sioni tatizo lolote Chadema kwenda Bitiama labda cha kujiuliza wamekwenda kufanyaje.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom