Dr Slaa alakiwa Buhingwe-Kigoma kwa Shangwe Kubwa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Msafara wa Katibu Mkuu, Dkt. Wilbroad Slaa unapokelewa kwa bashasha Wilaya ya Buhingwe, ambapo leo atakuwa na mikutano katika jJmbo la Manyovu.

Wananchi wamejipanga njiani hapa wakinyoosha vidole viwili na kushangilia kila Dkt. Slaa anapowapungia mkono.

Msafara wa pikipiki ndiyo nao ndiyo 'unaunga' hapa kumpokea Katibu Mkuu, kilometa kama 18 kutoka mjini.

Kuna ari kubwa sana ya wanaCHADEMA na wananchi kwa ujumla.

Updates....

Tumemaliza mkutano wa kwanza katika Kijiji cha Janda, Jimbo la Manyovu, wilayani Buhingwe, Mkoa wa Kigoma. Ulikuwa umefana sana na watu wamechangamka wakifurahia mkutano kila dakika inayokwenda.

Sasa msafara unasonga mbele kwenda mkutano wa pili.

Updates No 2.....

Msafara umewasili eneo la Mnanila unapofanyika mkutano wa pili kitambo na hatimaye sasa Dkt. Slaa yuko jukwaani akizungumza na wananchi.

Anazungumzia siku ya uhuru na dhana ya uhuru!


attachment.php


Source: Tumaini Makene Afisa Mkuu wa Habari CHADEMA.
 
Msafara wa Katibu Mkuu, Dkt. Wilbroad Slaa unapokelewa kwa bashasha Wilaya ya Buhingwe, ambapo leo atakuwa na mikutano katika jJmbo la Manyovu. Wananchi wamejipanga njiani hapa wakinyoosha vidole viwili na kushangilia kila Dkt. Slaa anapowapungia mkono. Msafara wa pikipiki ndiyo nao ndiyo 'unaunga' hapa kumpokea Katibu Mkuu, kilometa kama 18 kutoka mjini. Kuna ari kubwa sana ya wanaCHADEMA na wananchi kwa ujumla. Source: Tumaini Makene Afisa Mkuu wa Habari CHADEMA.
Mkuu Makene, Tanzania tunamhitaji kiongozi aina ya Dr. Slaa mwenye msimamo asiyeteteleka, tupia na picha, aibu kwa ccm hiyo
 
Last edited by a moderator:
Huyu Molema sina imani naye kwa uongo! Leo sijui ataweka picha za msafara w wapi?!
 
Endelea kuwahadaa wana BAVICHA wanao fuatilia ziara ya kupigwa mawe kwa Babu Slaa wakiwa Land Mark Hotel kwenye kongamano la kujadili itifaki ya mazishi ya CDM Saccoss in 2015!
 
Back
Top Bottom