Dr. Slaa akosoa uharibifu wa nyavu za uvuvi haramu ulinaofanywa na Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa akosoa uharibifu wa nyavu za uvuvi haramu ulinaofanywa na Magufuli

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Oct 22, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,406
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  Alipokuwa kwenye kampeni zake katika kanda ya Ziwa, Dr. Slaa alionyesha kukerwa na mkakati wa Dr. Magufuli - Waziri wa uvuvi na ufugaji - katika kupambana na uvuvi haramu.

  Kwa Dr. Magufuli ni kuharibu nyavu za uvuvi haramu ambazo yasadikiwa zinavua samaki wachanga na ambazo husababisha kupungua kwa kasi ya kukua kwa uzao wa samaki. Hivyo, kuwaharibia nyavu wavuvi hao Dr. Magufuli anaamini ya kuwa kwanza anawaongezea gharama za uvuvi haramu wahusika hao na pili analinda uzao wa samaki hao kutovunwa au kubakwa mapema mno kwa vichanga hivyo..

  Kwa Dr. Slaa kitendo cha kuchoma nyavu ni uchafuzi wa mazingira. Nyavu zingeliweza kurudishwa kiwandani na kutengenezwa upya badala ya kuchomwa kwa nyavu hizo. Lakini kubwa zaidi mbona hao wakubwa wenye hivyo viwanda au wasafirishaji na wauzaji wa hizo nyavu zinazokamata samaki wachanga hawathibitiwi?

  Sasa inakuwaje mvuvi ambaye ana kipato kidogo aumizwe na hatua za serikali wakati yule aliyemsababishia madhara hayo anaachwa aendelee na biashara yake hiyo haramu?

  Haya ni maswali ya kimsingi kabisa na ndiyo maana vita dhidi ya uvuvi haramu havina mafanikio kwa sababu vita hivyo havitafuti kumaliza kiini cha tatizo ila kumjenga Mheshimiwa Magufuli ili aonekane machoni pa watanzania kuwa anachapakazi lakini ukweli ni kuwa anatwanga maji kwenye kinu.............
   
 2. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na Mzee Slaa kwenye mada hii. Na Mzee Magufuli nadhani ajitahidi kuwadhibiti hao wanyonya damu wa soko huria. Sheria ni Msumeno. Soko huria bila sheria bora turudi tuliko kua. tafadhalini wakuu. looo!
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hana lolote mbona hoja ni dhaifu sana


  magufuli alitembelea hadi maduka yenye kuuza nyavu na kutoa angalizo la kushughulikiwa

  ila anapaswa ajue ktk utekelezaji wa jambo kuna vyombo vingi na ngazi nyingi zinahusika

  mropokwaji ambae yeye kila kitu lazima akisemee hata kile asichokijua unajiangusha sio kujishusha
   
 4. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ok sasa tuambie wewe hoja yako nini? ungekuwa wewe ungefanya nini, ungewafuatilia hao wanaotengeneza nyavu au ungeenda kuharibu nyavu za hao watu ambao hata hawaelewi impact ya hizo nyavu wanazouziwa? acha negative zako zisizo na msingi wowote. Ukitaka kupambana na matatizo hayo lazima uende kwenye root of the cause, lazima uhakikishe kuwa wattengenezaji wa hizo nyavu wanaeleimishwa au wanadhinitiwa and then uende kuwaaelimisha watumiaji.

  Achana na ushabiki usio na tija yoyote
   
 5. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Sio lazima kila hoja uchangie na negative views zako.Mropokaji ni wewe ambaye whatever concerns Dr Slaa argument lazima ukurupuke tu.
   
Loading...