Elections 2010 Dr. Slaa akiingia Ikulu viongozi wabovu wasamehewe?

Nova Kambota Is Always A gentle Man Feel Proud To Visit His Site, call 0717-709618 or 0783-610926,email;novakamota@gmail.com,,,,,,,,,,,,,Kingine kitakachoimaliza CHADEMA ni swala la Dr slaa kuhubiri kwenye majukwaa kuwa atatoa elimu bure na afya bure lakini mtu huyuhuyu ni mwenyekiti wa bodi wa hospitali ya CCBRT ambayo inapewa shilingi bilioni moja kwa mwaka halafu bado haitoi huduma bure kwa asilimia mia moja haya hiki ni kiinimacho kingine cha CHADEMA.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

afu uliwahi dai umesoma Ilboru, mbona upembuzi wako hauakisi elimu elimu uliyo nayo?
 
Taratiiiiiiiiiiiiibuu mwisho wa CCM unakaribia, maana wameacha hata kunadi ilani ya uchaguzi walioitunga wenyewe. Jamaa jana anaropoka;

1. Fly-over tano Dar (Ubungo, Magomeni, Temeke, Tazara na Faya) - ndani ya miaka mitano ni upuuuuzi mtupu
2. Machniga complex tano Dar - hata hiyo moja aliyoianzisha Mkapa hajaimaliza, huyu ndiye Rais Ahadi mnayemtaka
 
ndugu zangu wa-tz, sitochoka kutoa duku duku langu juu ya kiongozi huyu mumtakae nyinyi.

Najua wengi mtachukizwa, lakini hii ni haki yangu ya msingi ya kikatiba, hivi kiongozi mwenye visasi kama huyu wa nini? Au taarifa hii mmeifumbia macho na masikio kwa makusudi?

Huyu slaa mnaedhani atakuwa rais, ndiye aliyemchimbia mkwara ndugu mwakipesile.

Kama ndoto zake za kuingia ikulu zilivyomtuma, akaamua kumchimbia mkwara kwa kuona ni kikwazo kwake.

Nna mashaka si mwkipesile tu atakayetafuta pa kupita, watanzania lukuki watakiona kwa ufedhuli atakaoufanya.

Mpaka walom-support katika jf watajuta ila itakuwa too-late.:nono:

Lakini wadau wa jf msiogope, kaka/baba mdogo/mjomba 'enu hatoingia ikulu.

Kikwete ndio chaguo la wa-tz wengi.

Chagua ccm, chagua kikwete.

sio mwakipesile tu, ni mafisado wote. Hata wewe kama ni fisadi au mla makombo ya mafisadi kama unavyofanya utatafuta pa kupita.
 
Nova Kambota Is Always A gentle Man Feel Proud To Visit His Site, call 0717-709618 or 0783-610926,email;novakamota@gmail.com,,,,,,,,,,,,,Kingine kitakachoimaliza CHADEMA ni swala la Dr slaa kuhubiri kwenye majukwaa kuwa atatoa elimu bure na afya bure lakini mtu huyuhuyu ni mwenyekiti wa bodi wa hospitali ya CCBRT ambayo inapewa shilingi bilioni moja kwa mwaka halafu bado haitoi huduma bure kwa asilimia mia moja haya hiki ni kiinimacho kingine cha CHADEMA.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

NDIO MAANA DR SLAA ANATAKA MADARAKA YATAKAYOMWEZESHA KUINFLUENCE SERA ZA KUTOA HUDUMA BURE. NAFASI ALIYONAYO HIVI SASA KATIKA CCBRT HAIMPATII MADARAKA MAKUBWA YA KUWEZESHA HUDUMA KUTOLEWA BURE. MILIONI MIA MOJA INATOSHA KUJENGA SHULE MOJA YA SEKONDARI YENYE MAABARA, MAKATABA, NYUMBA ZA WAALIMU NA VIFAA MUHIMU VYA KUFUNDISHIA. HIVYO BILIONI 133 ZILIZOIBIWA KATIKA EPA ZINGETOSHA KUJENGA SHULE 1330.

KATIKA MWAKA BAJETI YA 2010/11 SERIKALI INATOA MISAMAHA YA KODI HUSUSAN KWA MAKAMPUNI YA MAFUTA KWA KIWANGO KINACHOFIKIA 2.7 YA PATO LA TAIFA (GDp0 BADALA YA KIWANGO KINACHOPENDELEZWA NA WACHUMI CHA 1%. HIVYO MISAMAHA HIYO KUFIKIA BIOIONI 700 BADALA YA BILIONI 200 TU. HIVYO SERIKALI INAKOSEHWA KIASI CHA BILIONI 500 KILA MWAKA KUTOKANA NA SERIKALI ZA CCM KUTOKUWA MAKINI. FEDHA HIZO ZINATOSHA KUJENGA SHULE SEKONDARI 5000 KILA MWAKA. HADI MWAKA 2009 TANZANIA INA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI, BINAFSI, ZA KAT, ZA DINI N.K JUMALA YAKE NI 4102 TU. HIVYO UINAWEZA KUONA NI FEDHA KIASI GANI INAPOTEA KUTOKANA NA WIZI WA VIONGOZI WA CCM KUSHIRIKIANA NA VIBAKA UCHUMI WANAWAITA WAWEKEZAJI.
 
Jatropha umesoma hii............Tatu kisera CHADEMA ni vigeugeu kwa maana ukiangalia katika katiba yao inaeleza wazi kuwa wao wanafata misingi ya ubepari lakini leo hii wanajinadi majukwaani kuwa watatoa elimu bure na afya bure ilihali wanajua fika kuwa katika ubepari hakuna kitu cha bure hata jeneza linauzwa na hata wachimba kaburi wanalipwa, sasa wanapoibuka watu makini wenye upeo mpana kama Maggid Mjengwa anapovitaka vyama vya siasa vijipambanue kiitikadi kwa maneno na vitendo kama wanafata itikadi ya kijamaa au ubepari wanachadema ambao wengi wao hujadili watu badala ya hoja wanalipuka kwa jazba na matusi, haitoshi CHADEMA walikuja na sera ya majimbo 2005 lakini cha ajabu imeyeyuka mwaka huu 2010 bila sababu za kina, lakini haya yote tisa kumi ni hili swala la CHADEMA kukunja ngumi na kusalimiana peoples power………..hivi kwa mtu timamu ngumi nayo hoja? au ugomvi?..............Nova Kambota Is Always A gentle Man Feel Proud To Visit His Site, call 0717-709618 or 0783-610926,email;novakamota@gmail.com
 
WanaJF Habari yenu!
Hii ni mara yangu ya kwanza kujiunga hapa ingawa nimekuwa msomaji mzuri tu wa huu mtandao kwa kipindi kirefu kilichopita.
anyway nimependa tu nichangie hapa kwa kuwa kipindi tulichoacho ni muhimu kwetu Watanzania.

Nafikiri hatuhitaji kiongozi/viongozi wa visasi. Ikiwa hivyo basi nchi itaangamia kwani kiongozi huyohuyo ni mtanzania na anaishi humuhumu nchini. Sidhani kama watu watapenda kuona na kukaa kimya visasi vitakapotawala. Hatima yake ni vita na migogoro.
Suala la umeme kukatika wakati wa kampeni si lazima liwe hujuma, mbona umeme hukatika hata kipindi watu wakiwa katika vyumba vya upasuaji mahospitalini!!! Nafikiri ingekuwa busara kwa Chadema kujiandaa hata kwa jenereta wakijua fika kabisa nchi ina matatizo ya umeme na lolote lingeweza kutokea.
Ni hayo tu wanaJF, tusaidie kuifanya nchi iendelee kuwa kisiwa cha Amani.
 
Taratiiiiiiiiiiiiibuu mwisho wa CCM unakaribia, maana wameacha hata kunadi ilani ya uchaguzi walioitunga wenyewe. Jamaa jana anaropoka;

1. Fly-over tano Dar (Ubungo, Magomeni, Temeke, Tazara na Faya) - ndani ya miaka mitano ni upuuuuzi mtupu
2. Machniga complex tano Dar - hata hiyo moja aliyoianzisha Mkapa hajaimaliza, huyu ndiye Rais Ahadi mnayemtaka

Ndugu Jafar,

Nilishiriki ktk Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wakati huo tukiwa na Five Year Plans. Mbona hizi ahadi za J.K. zinaonekana kana kwamba hakuna mpangilio wowote? Chini ya serikali ya CCM hakuna Mpango unaohakikisha mapato ya Taifa, pamoja na mikopo ambayo tunaweza kupata, yatatumika vipi? Did Five Year Plans lapse with the death of Nyerere?

J.K. akiwa Kanda ya Ziwa aliahidi Vivuko, Meli na barabara za lami, akiwa Kigoma aliahidi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa. Juzi ameahidi Bagamoyo kiwanja cha ndege kingine cha kimataifa pamoja na Bandari ya kisasa. Matumizi ya viwanja hivi wakati Air Tanzania iko mahtuti, hayaeleweki.

Hospitali za Rufaa zimeahidiwa huko Ruvuma na sijui wapi tena. Sasa Dar es Salaam inaahidiwa Machinga complexes tano na Fly-overs ktk kila manispaa. Hivi vyote viko ktk Five Year Plan au ni vya jukwaani tu?

Katika 5Year Plans za siku hizo zetu, tulikuwa tuna-forecast pia upatikanaji wa wataalam wa kikwetu kuendesha miraji tuliyojiwekea. Tulitazama nchi nzima, sio kwa mahitaji ya fedha za maendeleo tu, bali pia kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Serikali na taasisi zake. Hizi ahadi za J.K. endapo atashinda zikitekelezwa, si lazima sehemu nyingine zisubiri? Tusimchague huyu? Amechanganyikiwa!!!!!!!!!

Makwaiya wa Kuhenga ktk kipindi chake katika Runinga anauliza "Je Tutafika?"
 
pongezi kwako hatutaki Rais mwenye visasi.Hizo ni kampeni za vitisho. Ndio maana nasema afadhali ya Dr Kikwete

Mama Porojo,

Hamtaki wewe na nani!!! Ni yupi aliyekutuma umsemee hapa!! Sema simtaki Rais mwenye visasi usiseme hatumtaki kwani kila mtu hapa ana nafsi yake!!!!

Tiba
 
WanaJF Habari yenu!
Hii ni mara yangu ya kwanza kujiunga hapa ingawa nimekuwa msomaji mzuri tu wa huu mtandao kwa kipindi kirefu kilichopita.
anyway nimependa tu nichangie hapa kwa kuwa kipindi tulichoacho ni muhimu kwetu Watanzania.

Nafikiri hatuhitaji kiongozi/viongozi wa visasi. Ikiwa hivyo basi nchi itaangamia kwani kiongozi huyohuyo ni mtanzania na anaishi humuhumu nchini. Sidhani kama watu watapenda kuona na kukaa kimya visasi vitakapotawala. Hatima yake ni vita na migogoro.
Suala la umeme kukatika wakati wa kampeni si lazima liwe hujuma, mbona umeme hukatika hata kipindi watu wakiwa katika vyumba vya upasuaji mahospitalini!!! Nafikiri ingekuwa busara kwa Chadema kujiandaa hata kwa jenereta wakijua fika kabisa nchi ina matatizo ya umeme na lolote lingeweza kutokea.
Ni hayo tu wanaJF, tusaidie kuifanya nchi iendelee kuwa kisiwa cha Amani.

Hilo Limbwata la CCM utakuffa nalo. Usisome katikati ya mistari. Unataka Dr. Slaa ampende kwa lipi? Unamjua Mwakyembe au unamsikia? Muulize Mwandosya, Mwakyembe, Mwakyusa wanamfahamu alivyo mtu mbaya na hatari kwa mustakabari wa Taifa hivi sasa. Huyu mtu hafai kuwa hata kiongozi wa kitongoji na ni msaliti mkubwa.

Kikwete hana visasi????????? Uliza waliopata adha ya visasi vya Kikwete usikurupukie mada. Uliza mgawanyiko uliopo ndani ya CCM kama siyo visasi vya Kikwete. Acha propaganda zisizo na details. CCM imewapumbaza na kuwafumba macho na mmekuwa maskini wa kumbukumbu kiasi hicho????????
 
Mama Porojo,

Hamtaki wewe na nani!!! Ni yupi aliyekutuma umsemee hapa!! Sema simtaki Rais mwenye visasi usiseme hatumtaki kwani kila mtu hapa ana nafsi yake!!!!

Tiba

Achana naye ni wale wale wanatafuta mob support hataweza hata siku moja kusimama yeye kama yeye
 
NAJUA WENGI MTACHUKIZWA, LAKINI HII NI HAKI YANGU YA MSINGI YA KIKATIBA, HIVI KIONGOZI MWENYE VISASI KAMA HUYU WA NINI? AU TAARIFA HII MMEIFUMBIA MACHO NA MASIKIO KWA MAKUSUDI?

Kiongozi mbovu kama Mwakipesile ulitarajia atabebwa hadi lini?
 
Ndugu Jafar,

Nilishiriki ktk Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wakati huo tukiwa na Five Year Plans. Mbona hizi ahadi za J.K. zinaonekana kana kwamba hakuna mpangilio wowote? Chini ya serikali ya CCM hakuna Mpango unaohakikisha mapato ya Taifa, pamoja na mikopo ambayo tunaweza kupata, yatatumika vipi? Did Five Year Plans lapse with the death of Nyerere?

J.K. akiwa Kanda ya Ziwa aliahidi Vivuko, Meli na barabara za lami, akiwa Kigoma aliahidi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa. Juzi ameahidi Bagamoyo kiwanja cha ndege kingine cha kimataifa pamoja na Bandari ya kisasa. Matumizi ya viwanja hivi wakati Air Tanzania iko mahtuti, hayaeleweki.

Hospitali za Rufaa zimeahidiwa huko Ruvuma na sijui wapi tena. Sasa Dar es Salaam inaahidiwa Machinga complexes tano na Fly-overs ktk kila manispaa. Hivi vyote viko ktk Five Year Plan au ni vya jukwaani tu?

Katika 5Year Plans za siku hizo zetu, tulikuwa tuna-forecast pia upatikanaji wa wataalam wa kikwetu kuendesha miraji tuliyojiwekea. Tulitazama nchi nzima, sio kwa mahitaji ya fedha za maendeleo tu, bali pia kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Serikali na taasisi zake. Hizi ahadi za J.K. endapo atashinda zikitekelezwa, si lazima sehemu nyingine zisubiri? Tusimchague huyu? Amechanganyikiwa!!!!!!!!!

Makwaiya wa Kuhenga ktk kipindi chake katika Runinga anauliza "Je Tutafika?"

Akimaliza kuhutubia ukimuuliza amesemaje anakuwa amesahau. jamaa ana matatizo makubwa siyo mchezo. hebu tubadili katiba tusiwe na rais ambaye ni mgombea wa urais wakati huo huo (kabidhi madaraka upambane jukwaani). Sasa hivi kwa hali mbaya aliyonayo anaweza kufanya kitu cha hovyo. kampeni amehamishia kwenye familia, maswahiba na mitandao kujaza wananchi chuki. Huyu ndiyo hana visasi hadi chama chenyewe hakina ukaribu na mgombea!!!!!!
 
hawav watu wametumwa humu na ccm kwa fujo maana wanavo join kwa fujo na thread zao wizi mtupu,....sijui mta mbadili nani mawazo humu maana hamna mjinga JF tofauti na nyie
 
HUYU SLAA MNAEDHANI ATAKUWA RAIS, NDIYE ALIYEMCHIMBIA MKWARA NDUGU MWAKIPESILE.
Tumekushtukia kuwa na wewe ni miongoni mwa hao jamaa wanaolipwa kwa ajili ya kuhamasisha watu wachague CCM na kiongozi wao mwenye afya yenye mgogoro ila sie tunasema 'HATUDANGANYIKI'
 
Huyu anataka watu tupewe ban ya milele.. Watanzania watakaoichagua CCM ni wale wanaonufaika nayo kama wewe kwa kutuibia mali zetu na ninyi mkagawana kama peremende. CCM chaguo la MAFISADI acha kutudhalilisha. Dhiki na shida haijakukuta ndugu yangu laiti kama ungelijua ni kiasi gani watanzania walio maskini wanataabika usingezungumza unalozungumza. Watanzania wanahitaji mabadiliko ya uongozi na wakati wa mabadiliko ni sasa.Mwogope Mungu kwa kauli zako. 'FURAHA YENU IGEUZWE KUWA KILIO NA SHANGWE NAYO IKAWE MAOMBOLEZO, FANYENI ANASA MKAWE VIPOFU'
 
Jatropha umesoma hii............Tatu kisera CHADEMA ni vigeugeu kwa maana ukiangalia katika katiba yao inaeleza wazi kuwa wao wanafata misingi ya ubepari lakini leo hii wanajinadi majukwaani kuwa watatoa elimu bure na afya bure ilihali wanajua fika kuwa katika ubepari hakuna kitu cha bure hata jeneza linauzwa na hata wachimba kaburi wanalipwa, sasa wanapoibuka watu makini wenye upeo mpana kama Maggid Mjengwa anapovitaka vyama vya siasa vijipambanue kiitikadi kwa maneno na vitendo kama wanafata itikadi ya kijamaa au ubepari wanachadema ambao wengi wao hujadili watu badala ya hoja wanalipuka kwa jazba na matusi, haitoshi CHADEMA walikuja na sera ya majimbo 2005 lakini cha ajabu imeyeyuka mwaka huu 2010 bila sababu za kina, lakini haya yote tisa kumi ni hili swala la CHADEMA kukunja ngumi na kusalimiana peoples power………..hivi kwa mtu timamu ngumi nayo hoja? au ugomvi?..............Nova Kambota Is Always A gentle Man Feel Proud To Visit His Site, call 0717-709618 or 0783-610926,email;novakamota@gmail.com
Acha kuonyesha ujinga wako. Marekani ni nchi ya kibepari na inatoa elimu bure kuanzia chekechea hadi high school. It is all about priorities. Lete hoja nyingine!
 
Mkuu kuna majukwaa mengine mengi hapa jamvini nadhani wawezaenda kuchangia huko, Katika hili jamvi huwezi kutuletea jipya. Jaribu kwenye udaku!
 
Hata ingekuwa mimi ndo slaa, nikitinga ikulu naachia wafungwa wote magereza ili kutoa nafasi kwa jk na kundi lake lote, wapo wengi sana maana nikuanzia halmashauri hadi serikali kuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom