Dr. Slaa aitaka tume ya uchaguzi kusimamisha zoezi la kuhesabu kura mara moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa aitaka tume ya uchaguzi kusimamisha zoezi la kuhesabu kura mara moja

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gwallo, Nov 3, 2010.

 1. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa ametoa tamko kwa waandishi wa habari akilitaka tume ya uchaguzi kusitisha zoezi kwa kile anachosema usalama wa taifa kuhujumu kura za watanzania.

  Source taarifa ya habari ya saa 10.TBC
   
 2. S

  Selemani JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  lol
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ile 50% ya Usalama wa Taifa unaoripoti kwake unashindwa kumsaidia? Mfa maji haeshi kutapatapa!
   
 4. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja na Dr. Slaa namuunga mkono hata ikiwezekana kuingia mtaani...TUPO TAYARI kwa lolote hii nchi sio yao yetu sote hakuna aliyezaliwa akakabidhiwa na MUNGU.
   
 5. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.

  Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.

  " Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri' au ' kuridhisha' katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar," alisema Martin.

  Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.

  Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.

  Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.

  "Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika," alisema.

  Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .

  Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.

  " Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible)
   
 6. N

  Ndinimbya Senior Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uchakachuaji wa kura wa nini jamani kisa ni kutafuta asilimia 80? Hii ni mbayaaaaa...!
   
 7. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
 8. W

  We can JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni sisi wa Tanzania tutakaohusika na mambo yetu, SIYO WAANGALIZI WA KIMATAIFA.
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  50% ndio imemwambia kwa sasa wanachakachua!
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,645
  Likes Received: 21,857
  Trophy Points: 280
  Walichosifu waangalizi toka nje ni upigaji kura kuwa huru na haki na utulivu. Swala la kuhesabu na kutangaza matokeo ni jingine kabisa. Tume kama itatoa majumuisho ya 2 + 3 + 4 = 5 basi hiyo ni kasoro ambayo haipaswi kunyamaziwa kwa vile inaondoa maana halisi ya kupiga kura. Haya nasi tukubali uchaguzi ulifanyika kwa haki na uhuru, jee matokeo kwa nini yatangazwe tofauti na taarifa (signed) toka vituoni?
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja Mkuu watu
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180

  Hawa waangalizi wa Africa wote wanafiki tuuu waliona wapi kuna uhuru na haki?
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  lakini jk alise hivi ''hata tusiposhinda tutajishindisha.''
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Thank you Dr. Slaa.
  hicho ndicho nilichokitarajia kutoka kwako. Yaani kusitisha zoezi zima la utangazaji matokeo.

  Na ikibidi tume wapelekwe mahakamani kwa kesi ya kugushi MATOKEO
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  source: michuzi =dailynews=slaa can never be the fifth president

  mwananchi: EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola

  Elias Msuya

  MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

  Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

  "Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

  Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

  Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

  Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

  "Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema Martins.

  Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

  "Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.
  Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

  "Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.

  Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

  "Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema Ndelcheva.
   
 16. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  sio kosa lako bali ni upeo wako mdogo wa kufikiria sababu ulizaliwa MWANANYAMALA kwenye foleni
   
 17. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hawa hawajui umafia uliofanywa hapa.Wanategemea kuwepo na purukushani vituoni ndo waseme haukuwa huru na haki.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Watanzania wote wanajua fika kwamba uchaguzi huu ulikuwa huru na wenye haki isipokuwa kazi kubwa ya uhesabuji wa kura ndio unafanyiwa uchakachuaji jambo ambalo wao wamepigwa nje!
   
 19. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh! Kumbe ni 50% ya wambeya tu! Teh teh teh!!!!
   
 20. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee wa kula kona (King of Kings) hajafanya mavitu yake? Bora umeondoa ile siginecha! Teh teh teh!!!!!

  Peeeooopppllleeeesssss pppoooowwwweeeeerrrrr! Watu kimyaaaaaa!!!!!!
   
Loading...