Elections 2010 Dr slaa ahudhurie au asihudhurie kuapishwa kwa kikwete kesho

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Ndugu zangu uchaguzi umekwisha na matokeo yenye utata yamekwishatolewa na tume ya uchguzi. Matokeo hayo yana kila dalili kuwa yamechakachuliwa kwa nia ya kumuokoa mgombea wa ccm dr jakaya kikwete na kulinda heshima ya ccm.
Najua wengi wetu tuna uchungu sana wa kuibiwa kura zetu. Lakini ni ukweli kwamba chadema imepata madiwani na wabunge wengi kwa mara ya kwanza, mfano katika kanda ya ziwa upo uwezekano mkubwa chadema ikaongoza halamshauri na manispaa zisizopungua 4hadi 6.

Huu ni mzigo mkubwa sana ambao chadema imebeba mbele ya jamii kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Na matarajio ya wananchi ni makubwa sana.

Kama madiwani na wabunge watashindwa kuondoa kero mbali mbali zinazowakabili wananchi katika kata na majimbo chadema iliyopata ushindi ni wazi kuwa idadi ya madiwani na wabunge wa chadema itashuka sana mwaka 2015, jambo ambalo litakuwa shangwe kubwa kwa ccm. Lakini kibaya zaidi chadema itashindwa kupata viti vya wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji mwaka 2014.

Ili chadema iweze kujipanga vyema kushika madaraka katika halmshauri ilizoongoza na wagombea wake wengine walioshinda kutekeleza kwa vitendo ahadi zao kwa wananchi, panahatajika hali ya amani na utulivu miongioni mwetu wote viongozi wa ngazi ya taifa, mikoa, wilaya, madiwani na wabunge wetu.

Ni kuweli usiopingika ili madiwani na wabunge wa chadema waweze kutimiza matarajio ya wananchi, wananchama wote wa chadema katika maeneo husika wanahatajika kushirikai katika kubuni, kuratibu na kusimamia mipango, mikakati na miradi mabali mbali ya maendeleo katika maeneo yao. jukumu hili linahataji wananchama wenye mawzo yaliyotulia.

Jukumu lingine kubwa lililo mbele yetu kama wananchama na makada wa chadema ni kukijenga chama kwa kufungua matawi na mashina nchi nzima ili kujiweka tayari na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa 2015. Hili nalo ni jukumu kubwa linalohitaji wananchama waliotulia.

Hivyo wakati chadema makao makuu ikishughulikia suala la kuibiwa kwa kura zetu, ambapo naamini suluhisho kamili ni kuandikwa upya kwa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kushirikisha wadau mbali mbali; na kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi.

Natoa pendekezo wanachama na mashabiki wa chadema wengine wote tusitishe malumbano ya suala hilo na tujikite zaidi katika majukumu niliyoyataja hapo juu, kwani wananchi waliowapigia kura madiwani na wabunge wetu watakapona tunaendeleza malumbano ya suala hilo watavunjika moyo na kutokuiamini chadema katika chaguzi zijazo. Aidha endapo madiwani na wabunge wetu watakaposhindwa kutimiza ahadi kwa sababu za msingi wapinzani wetu watawaambi wananchi kuwa tulishindwa kutimiza ahadfi hizo kwa sababu ya kugombea kwenda iuklu, hivyo tutakosa kura siku za usoni.

Hivyo kwa kuanzia ili kujenga mazingira mazuri ya nashauri chadema ishiriki katika shughuli ya kuapishwa kwa kikwete ndipo madiwani na wabunge wetu pia wataweza kupata ushirikiano watakaouhitaji kutoka serikalini.

Naomba kuwasilisha
 
Ulianza na hoja nzuri na mapendekezo ya kujenga upinzani/mawazo mbadala.
Mwisho unakuja na propaganda tukuelewe vipi?
 
Back
Top Bottom