Dr. Slaa afanya mazungumzo na Balozi wa Marekani

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
285
Wadau kuna jamaa kanihabarisha kuwa leo asubuhi Mh. Dr. Slaa alionekana akipokewa na RSO wa ubalozi wa Marekani pale ubalozini. Bado hajafahamu nini kilizungumzwa katika mkutano huo.

Mwenye habari zaidi atujuze.

By the way, Serikali ya marekani imeshampongeza JK kwa ushindi?
 
Wampongeze kwa kumpora Dr. Slaa Uraisi? Marekani ni nchi makini siyo kama sisi ambao kwa kofia, fulana na khanga au kibaba cha unga unapelekeshwa kama pia.............
 
Baada ya viongozi wa DINI , sasa, ni mabalozi, ok ngoja tusubiri siku ile ambayo dr atakuja kwenye press conference na KUDADAVUA kuhusu UCHAKACHUAJI uliofanywa na CCM
 
Bado upepo wa kisiasa Tanzania haijatulia....hata JK na CCM yake naamini bado hawajajua next move ya Dr. Slaa!! Jk anaweza kuwa surprised, tusubiri tuone!!
 
Tegemea Robert Gibbs (Mwandishi wa Habari wa Obama) kuulizwa swali linalohusu JK na uchakachuaji wa kura mara akirejea toka India.
 
Wadau kuna jamaa kanihabarisha kuwa leo asubuhi Mh. Dr. Slaa alionekana akipokewa na RSO wa ubalozi wa Marekani pale ubalozini. Bado hajafahamu nini kilizungumzwa katika mkutano huo.

Mwenye habari zaidi atujuze.
By the way, Serikali ya marekani imeshampongeza JK kwa ushindi?

naona moshi tayari .......lazima kiwake
 
Wadau kuna jamaa kanihabarisha kuwa leo asubuhi Mh. Dr. Slaa alionekana akipokewa na RSO wa ubalozi wa Marekani pale ubalozini. Bado hajafahamu nini kilizungumzwa katika mkutano huo.

Mwenye habari zaidi atujuze.

By the way, Serikali ya marekani imeshampongeza JK kwa ushindi?

Iliripotiwa kabla au wakati wa Kutangaza matokeo Dr. Slaa pia alikutana na maofisa wa balozi mbalimbali.

Let us wait and see what will come out.
 
Wadau kuna jamaa kanihabarisha kuwa leo asubuhi Mh. Dr. Slaa alionekana akipokewa na RSO wa ubalozi wa Marekani pale ubalozini. Bado hajafahamu nini kilizungumzwa katika mkutano huo.

Mwenye habari zaidi atujuze.

By the way, Serikali ya marekani imeshampongeza JK kwa ushindi?

UN wamempongeza JK hiyo inatosha kabisa
 
UN wamempongeza JK hiyo inatosha kabisa

UN wanamaana basi.....wamempongeza raisi wa Afriganstan bana..........Slaa mambambano bano yanaendelea, hii ni good move kwa upinzani next tie ccm watajifikiria mara mbili mbili
 
UN wamempongeza JK hiyo inatosha kabisa
UN wao ni too general kupongeza kwao kunaweza kuwa na maana ya kuendeleza amani ya maziwa makuu, wao huwa hawachagui, yeyote atakayeshinda leo wataipongeza Israel kesho wataipongeza Palestina and vice versa.
 
Ninafarijika sana na kila move ya Dr. Slaa.
Naamini rais wetu wa ukweli anatujali sana. Anafahamu tupo nyuma yake ndo maana anajiamini. sisi tunajiamini kwa sababu yake.
Long live Slaa. mjenzi makini wa taifa
 
nadhani ni wakati wa watanzania kuacha tofauti zetu na kufanya kazi kwa bidii. marekani ni taifa kama mataifa mengine kwahiyo sidhani kwamba wao ndio wanaotupa maelekezo ya kufanya dhidi juu ya nchi yetu.sisi tuko huru na tunajua ya kuwa chaguzi wetu haukuwa huru na haki laikini kwa faida ya taifa letu tuvunje makundi , mbona wao BUSH alipomdhulumu all gore sisi hatukushirikishwa kwenye mahamuzi yao. tusiwe na fikara za kikoloni . tufute tofauti zetu tujenge nchi yetu ni wakati wa kujenga mahusiano mema kwa vyama vyote vya kisiasa
 
Hujanishawishi bado kujenga mahusiano na CCM?! Tangu lini mjima akawa na uhusiano mwema na bepari?? Yaani napenda maisha yawe magumu zaidi na zaidi kwa miaka mi5 ijayo ili watanzania labda tujifunze kuwa kuikumbatia CCM ni maafa
 
Back
Top Bottom