Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, Juni 5, mwaka huu, ameanza ziara ya takriban wiki 3 barani Ulaya katika nchi ya Ujerumani.
Kwa mujibu wa habari kwenye Ukurasa wa Facebook ya CHADEMA na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Dkt. Slaa ambaye aliondoka nchini Juni 4, mwaka huu ktk ziara hiyo ya kikazi, atakutana na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.
Namnukuu-''Ni kweli mkubwa, Katibu Mkuu yuko nje ya nchi tangu juzi kwa ziara ya kikazi nchini Ujerumani, itakayochukua wiki tatu...atakuwa na ratiba tight kidogo, akiwa huko kama unavyojua Dkt. Slaa yuko kazini karibu muda wote, kwa sababu kwa sasa hakuna muda wa kupoteza hata sekunde, si unajua M4C iko matendoni mkubwa, ndani na nje ya nchi, ameenda kikazi,'' amesema Makene.
Itakumbukwa mwezi uliopita Dr Slaa alifanya ziara nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alifanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Michael Satta katika Ikulu ya Lusaka.

Eddie,
Walafi daima hufikiria nafsi zao na posho. Wana mageuzi hufikiria namba ya kukomboa mataifa Yao.
Nikuhakikishie, hakuna posho coyote iliyotolewa na hakuna sent hata mmoja ya chadema imetumika katika ziara hii. Dr. Slaa amesafiri na ndege kwa kutumia Economy Class kwa kutambua kuwa ukombozi sio sherehe bali kupitia milim a na mabonde kwa ajili ya watanzania wengi walioweka matumaini yaeo kwa Chadema.
Tarehe 5June, nimekuwa na mikutano mbalimbaeli Karlsruhe na viongozi wa ngazi mbalimbali. Nimejifunza mengi hasa kuhusiana na mfumo wa Utawala wa Local Government, Karlsruhe ipo katika State of Baden Wurtenburg.
Kuanzia Tarehe 6 June nimehudhuria Breakfast Prayer iliyoshirikisha viongozi Wabunge, Maspika, Mabalozi na viongozi wa Vyama kutoka nchi 100 kutoka Dunia nzima, na wajumbe zaidi ya 1,000. Huu ni Mkutano wa 18 tangu Breakfast Prayer Gatherings imeanza. Mkutano umeandaliwa na wabunge wa Bundestag (Bunge la Ujerumani). Kati ya waliohudhuria ni Wabunge wa Iran, Sudan na Southern Sudan. Ilifurahisha sana kuona Spika wa Sudan na Southern Sudan kukaa meza mmoja baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusiana na mgogoro baina ya nchi zao mbili. Huu ni mkutano unaounganisha madhehebu yote ya Dini, bila kubagua mataifa, rangi, na au dini zao. Dini zote zinaamini kuna Mwenyezi Mungu, na kumekuwa na themes mbaelimbali katika mkutano huu wa siku tatu.
Kuanzia kesho Nina mikutano kadhaa katika Lander ( States mbalimbali) kwa mikutano na MinisterPresident ( Mawaziri wakuu wa States hizo pamoja na maofisa mbalimbali. Kila nitakapopata nafasi nitakuwa nikiwajulisha matukio mbalimbali. Wenye nia njema wanaweza kuniuliza wanavyopenda kuliko kufanya posts za upotoshaji. Nawatakia nyote neema na baraka tele. Yako mengi yanayotuunganisha watanzania katika swala la dini zetu mbalimbali kuliko yanayotutenganisha. Nimejifunza mengi kwa Iran, ambayo ni takriban 99% Islamic lakini Bunge Lao Lina wabunge Waislamu, wayahudi na Wakristu.