Dr. Slaa aanza ziara ndefu barani Ulaya

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, Juni 5, mwaka huu, ameanza ziara ya takriban wiki 3 barani Ulaya katika nchi ya Ujerumani.

Kwa mujibu wa habari kwenye Ukurasa wa Facebook ya CHADEMA na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Dkt. Slaa ambaye aliondoka nchini Juni 4, mwaka huu ktk ziara hiyo ya kikazi, atakutana na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.

Namnukuu-''Ni kweli mkubwa, Katibu Mkuu yuko nje ya nchi tangu juzi kwa ziara ya kikazi nchini Ujerumani, itakayochukua wiki tatu...atakuwa na ratiba tight kidogo, akiwa huko kama unavyojua Dkt. Slaa yuko kazini karibu muda wote, kwa sababu kwa sasa hakuna muda wa kupoteza hata sekunde, si unajua M4C iko matendoni mkubwa, ndani na nje ya nchi, ameenda kikazi,'' amesema Makene.

Itakumbukwa mwezi uliopita Dr Slaa alifanya ziara nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alifanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Michael Satta katika Ikulu ya Lusaka.
Eddie,
Walafi daima hufikiria nafsi zao na posho. Wana mageuzi hufikiria namba ya kukomboa mataifa Yao.
Nikuhakikishie, hakuna posho coyote iliyotolewa na hakuna sent hata mmoja ya chadema imetumika katika ziara hii. Dr. Slaa amesafiri na ndege kwa kutumia Economy Class kwa kutambua kuwa ukombozi sio sherehe bali kupitia milim a na mabonde kwa ajili ya watanzania wengi walioweka matumaini yaeo kwa Chadema.

Tarehe 5June, nimekuwa na mikutano mbalimbaeli Karlsruhe na viongozi wa ngazi mbalimbali. Nimejifunza mengi hasa kuhusiana na mfumo wa Utawala wa Local Government, Karlsruhe ipo katika State of Baden Wurtenburg.

Kuanzia Tarehe 6 June nimehudhuria Breakfast Prayer iliyoshirikisha viongozi Wabunge, Maspika, Mabalozi na viongozi wa Vyama kutoka nchi 100 kutoka Dunia nzima, na wajumbe zaidi ya 1,000. Huu ni Mkutano wa 18 tangu Breakfast Prayer Gatherings imeanza. Mkutano umeandaliwa na wabunge wa Bundestag (Bunge la Ujerumani). Kati ya waliohudhuria ni Wabunge wa Iran, Sudan na Southern Sudan. Ilifurahisha sana kuona Spika wa Sudan na Southern Sudan kukaa meza mmoja baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusiana na mgogoro baina ya nchi zao mbili. Huu ni mkutano unaounganisha madhehebu yote ya Dini, bila kubagua mataifa, rangi, na au dini zao. Dini zote zinaamini kuna Mwenyezi Mungu, na kumekuwa na themes mbaelimbali katika mkutano huu wa siku tatu.

Kuanzia kesho Nina mikutano kadhaa katika Lander ( States mbalimbali) kwa mikutano na MinisterPresident ( Mawaziri wakuu wa States hizo pamoja na maofisa mbalimbali. Kila nitakapopata nafasi nitakuwa nikiwajulisha matukio mbalimbali. Wenye nia njema wanaweza kuniuliza wanavyopenda kuliko kufanya posts za upotoshaji. Nawatakia nyote neema na baraka tele. Yako mengi yanayotuunganisha watanzania katika swala la dini zetu mbalimbali kuliko yanayotutenganisha. Nimejifunza mengi kwa Iran, ambayo ni takriban 99% Islamic lakini Bunge Lao Lina wabunge Waislamu, wayahudi na Wakristu.
 
Inapendeza, hawa maccm wataruka ruka mwisho wao umewadia, mkuu anachapa kazi kwenda mbele , ni kushambulia pande zote mpka kieleweke
 
Kunya anye kuku akinya bata kaharaa...............perdiem zake lazima ajilinganishe na raisi kama kawaida yake, duuh wiki tatu.......sianatumia ruzuku yote ya chama

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Hongereni chadema tuwapige magamba kotekote nje na ndani wao china sis ujerumani. Peopleeeeeeeeeeees!
 
..atakuwa na ratiba tight kidogo, akiwa huko kama unavyojua Dkt. Slaa yuko kazini karibu muda wote, kwa sababu kwa sasa hakuna muda wa kupoteza hata sekunde, si unajua M4C iko matendoni mkubwa, ndani na nje ya nchi, ameenda kikazi,'' amesema Makene.
PEOPLE CHOOSE TO TALK ABOUT CHANGE, SOME TRY TO AVOID, WHILE OTHERS TAKES PARTY ON IT.

Hii nimeipenda.Bila shaka Dr.Slaa Atarudi akiwa na mambo mengi sana ya kulisaidia taifa hili.Ngoja tumsikilize atakaporejea.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, Juni 5, mwaka huu, ameanza ziara ya takriban wiki 3 barani Ulaya katika nchi ya Ujerumani.

Kwa mujibu wa habari kwenye Ukurasa wa Facebook ya CHADEMA na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Dkt. Slaa ambaye aliondoka nchini Juni 4, mwaka huu ktk ziara hiyo ya kikazi, atakutana na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.

Namnukuu-''Ni kweli mkubwa, Katibu Mkuu yuko nje ya nchi tangu juzi kwa ziara ya kikazi nchini Ujerumani, itakayochukua wiki tatu...atakuwa na ratiba tight kidogo, akiwa huko kama unavyojua Dkt. Slaa yuko kazini karibu muda wote, kwa sababu kwa sasa hakuna muda wa kupoteza hata sekunde, si unajua M4C iko matendoni mkubwa, ndani na nje ya nchi, ameenda kikazi,'' amesema Makene.

Big up Dr. W.P.Slaa.

Kwanza nimpongeza Dr. Slaa kwa umakini mkubwa wa sera za Chama chake ambacho kimepelekea sasa Tanzania kwenda kuwa na Katiba mpya kabla ya 2015. Rasimu ya Katiba Mpya tayari ina mwelekeo wa kutokomeza tamaa,ukiritimba na uimla wa Chama cha CCM kutaka kutawala Tanzania milele! This is one step ahead to State House.

Bila ya shaka Dr. Slaa atakuwa ameenda kupata mawaidha na ushauri namna CHADEMA watakavoendesha Serikali yao ya Tanganyika/Tanzania Bara hapo ifikapo 2015. Hilo halina ubishi.

Peoplesssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssss?.....Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer!!!

Chezea CHADEMA wewe!!!!!
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, Juni 5, mwaka huu, ameanza ziara ya takriban wiki 3 barani Ulaya katika nchi ya Ujerumani.

Kwa mujibu wa habari kwenye Ukurasa wa Facebook ya CHADEMA na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Dkt. Slaa ambaye aliondoka nchini Juni 4, mwaka huu ktk ziara hiyo ya kikazi, atakutana na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.

Namnukuu-''Ni kweli mkubwa, Katibu Mkuu yuko nje ya nchi tangu juzi kwa ziara ya kikazi nchini Ujerumani, itakayochukua wiki tatu...atakuwa na ratiba tight kidogo, akiwa huko kama unavyojua Dkt. Slaa yuko kazini karibu muda wote, kwa sababu kwa sasa hakuna muda wa kupoteza hata sekunde, si unajua M4C iko matendoni mkubwa, ndani na nje ya nchi, ameenda kikazi,'' amesema Makene.

Amealikwa na nani? Just curious!
 
Jahazi inazama huku uchaguzi wa kata 25, katibu kaitosa meli anakimbizia posho.....
 
Jahazi inazama huku uchaguzi wa kata 25, katibu kaitosa meli anakimbizia posho.....

wewe Mzenji hebu achana na mambo ya huku Tanganyika, Pia uwe na adabu hasa pale unapochangia kwny thread inayomhusu Mkombozi na Rais wetu.
 
Wasira si alisema CDM chama cha msimu,atuambie sasa msimu unaanza lini
 
Ni muhimu sana katibu akakutane na watu bana.

Inaniuma sana yaani katibu mkuu inabidi asafiri nje ya nchi wiki tatu ili akutane na watu?

Pole mkuu ingawa ni ngumu kumeza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom