Dr.slaa aandae baraza la mawaziri kwa serikali yake kivuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.slaa aandae baraza la mawaziri kwa serikali yake kivuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Nov 6, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Kwanza nampongeza Dr.Slaa kwa ushindi aliopata japo kaporwa.Watanzania wenzangu wanakukubali wala usiwe na shaka kabisa


  Pili naomba nianze kwa kutoa ushauri kwa Dr.SLAA aanze kuunda baraza la mawaziri wa serikali kivuli yenye muundo wa WIZARA 15 kama alivyopendekeza wakati wa kampeni hii inatokana na sababu zifuatazo;
  • Sote tunafahamu kuwa CHADEMA wameibuka na ushindi wa kishindo katika majiji yote ya Tanzania yaani Mwanza, Arusha, na sehemu kubwa ya Jiji la Dar-es-salaam kwa upande mwingine baadhi ya miji mikubwa nchini kama vile Iringa, Moshi, Manyara,Kigoma na mengine mengi. Ninavyoona mimi hapa kuna kazi ya ziada ya kufanya ili kuuthibitishia umma wa watanzania na serikali ya CCM kuwa Chadema ina mikakati mbadala ya kuwaletea wanachi maendeleo
  • Sote tunafahamu kuwa kuna miji ambayo kwa matokeo ya awali chadema iliongoza katika kura za wabunge na madiwani lakini baadae uchakachuaji ulibadilisha matokeo, miji hiyo ni Shinyanga, Sumbawanga,Bukoba n.k lakini kuna taarifa kuwa madiwani wengi katika mikoa mingi wanatoka chadema kwa sababu hizi ni dhahiri kwamba Halmashauri za miji hiyo zitaundwa na chadema na hivyo kuongeza majukumu kwa chadema ya kuwaletea maendeleo wananchi
  • Kumbukeni kuwa Dr.SLAA atakapofanya ziara za kikazi maeneo hayo atapokelewa kama RAIS KIVULI kwa hiyo tunatakiwa kuandaa mikakati ya namna ya kuongoza halmashauri hizo
  Kutokana na sababu hizo tatu ninashawishika kusema kuwa DR.SLAA anakuwa na hadhi sawa na JK tena kwa kiwango fulani DR.SLAA uko juu kwani JK atakuwa akiripoti kwa serikali kivuli hasa katika hiyo miji na majiji kwani halmashauri zitaundwa na chadema.

  Ningefurahi kuona serikali kivuli ikianza kazi mapema na kuweka wazi mission and vision towards 2015 na kuwafahamisha watanzania tutafanyaje.
  Dr.SLAA naamini atafanya hivyo kwani asipofanya mapema muda unakimbia sana 2015 ni kama tayari imefika.CHADEMA tusipoonyesha the difference kwa CCM katika maeneo husika tutajiweka katika mazingira magumu come 2014 wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa

  Kwa maoni yangu sasa tuanze kuunda serikali kivuli itakayokuwa ndogo ya wizara 15 itakayoongoza serikali kivuli Contemporarily

  Dr.slaa tunamwamini na tunamkubali tuanze kuchukua hatua tusije kuwa kama serikali ya OBAMA iliyojihisi itakaa milele kumbe balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
   
 2. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Baraza la mawaziri wa serikali kivuli linaweza kuundwa na CUF kwa kushirikiana na NCCR, TLP na UDP.

  CUF wana viti 24 wakati CHADEMA wana 22.
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  naunga mkono aslimia 100< kweli penye chadema wengi hapaharibiki kitu, pia kuna haja ya kuwekeza zanzibar, lindi na tanga
   
 4. The Kop

  The Kop JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 208
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Mie ntamtambua JK kuwa rais wangu pale atakapowaomba radhi WTZ kwa kuwakumbatia wezi wakubwa wa rasilmali za umma, cjawah kuona amiri jeshi mkuu ambaye ni swahiba wa wezi, sitakosea kama ntasema kuwa na yeye ndo walewale....mwiziiiiiii.....!
   
Loading...