Dr. Slaa aalikwa kwenye kongamano Ujerumani

Jason Bourne

JF-Expert Member
May 11, 2011
200
438
TAARIFA KWA UMMA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Peter Slaa amealikwa kuwa mmoja wa wanajopo (panelists) wanne, kutoka Mabara ya Afrika, Asia, Amerika Kusini na Ulaya, watakaojadili mada isemayo "Demokrasia Shinikizoni (democracy under pressure)" nchini Ujerumani.

Katibu Mkuu Dkt. Slaa ambaye amesafiri jana jioni kuelekea Ujerumani, atakuwa pamoja na wanajopo wenzake wengine ambao ni Prof. Dr. Kyaw Yin Hlaing (Academic Director Myanmar Egress; kutoka Rangum/Myanmar), Dkt. Aliaksandr Milinkiewitsch (Chairman, Movement for Freedom; kutoka Minsk/ Belarus), Gavana Henrique Capriles Radonski (Leader of the Opposition Movement Mesa de la Unidad Democratica; kutoka Carcas/ Venezuela).

*Mjadala wa mada hiyo ya Demokrasia Shinikizoni, itakuwa ni sehemu ya sherehe za miaka 50 za Siku ya Shirika la Konrad-Adenauer-Stiftung (KAS Day) katika mahusiano yake ya kimataifa na wadau wake mbalimbali kutoka nchi 80 duniani.

Mwenyekiti wa wanajopo katika kuendesha mjadala huo ni Christoph Lanz (Director of Global Content; Deutsche Welle, Berlin/ Germany)

Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Kansela wa Ujerumani, Dr. Angela Merkel, Rais Mstaafu wa Chile, Seneta Eduardo Frei Ruiz-Tangle na Rais Mstaafu wa Bunge la Ulaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa KAS, Dr. Hans-Gert Pottering.

Shirika la KAS linatimiza miaka 50 tangu lilipoanza rasmi kujihusisha na ukuzaji wa demokrasia, uhuru, amani maendeleo na haki. Kwa muda wote huo limekuwa likifanya kazi na wadau katika nchi mbalimbali duniani kutimiza malengo hayo tajwa.

Mpaka sasa KAS ina ofisi 80 sehemu mbalimbali duniani (pamoja na Tanzania), ikishirikiana na wadau wake katika kuendesha miradi inayohusiana na malengo hayo katika nchi 120.

Katika kusherehekea Jubilee ya Miaka 50 ya Siku ya KAS itakayofanyika Juni 27, 2012, shirika hilo limeamua kukutana na wadau na marafiki zake ambao pia wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika utendaji kazi wa KAS katika shughuli za kupigania demokrasia na maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa nchi husika.

Katika mada ya "Demokrasia Shinikizoni", wanajopo watajadili changamoto zinazowakabili watetezi wa demokrasia katika tawala mbalimbali zinazotumia njia dhalimu zinazobana upanukaji wa demokakrasia ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo ya watu.

Imetolewa leo Juni 25, 2012, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Afisa Habari CHADEMA
 
Slaa, kaalikwa kwenye sherehe na wafadhili wao Konrand Adenauer Stiffing (KAS) wanatimiza miaka 50 hivi ukialikwa kwenye Jubilee ndio kongamano.
lipumba ndiye aliyealikwa kwenye jubilee la uchumi duniani akajibatiza uenyekiti
 
Slaa, kaalikwa kwenye sherehe na wafadhili wao Konrand Adenauer Stiffing (KAS) wanatimiza miaka 50 hivi ukialikwa kwenye Jubilee ndio kongamano.

Wakati flani huwa napata shida sana kuuelewa upeo wako wa kufikiri, haya mkuu!
 
Wakati flani huwa napata shida sana kuuelewa upeo wako wa kufikiri, haya mkuu!

Pombekali
Unaweza kuwa unanichukia bure sababu tunapishana mitazamo natanguliza msamaha kama nakukwaza lakini ndio maana ya forum mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Slaa, kaalikwa kwenye sherehe na wafadhili wao Konrand Adenauer Stiffing (KAS) wanatimiza miaka 50 hivi ukialikwa kwenye Jubilee ndio kongamano.

Kumbe Ritz hujui ndani ya Jubilee kunaweza kuwa na kongamano, we umefika darasa la ngapi? Pole sana.
 
Tanzania soon itakombolewa.Hongera Dr Slaa kwenda kuwakilisha wanyonge
 
Halafu hili tangazo,lilitakiwa lisomeke ''TAARIFA KWA WANACHAMA WA CHADEMA'' na sio taarifa kwa umma kama lilivyo andikwa,dr slaa sio kiongozi wa umma ni kiongozi wa chama,otherwise ingekua ni taarifa inayomhusu jk au kiongozi yeyote wa serikali ndo ingekua taarifa kwa umma.
 
Slaa, kaalikwa kwenye sherehe na wafadhili wao Konrand Adenauer Stiffing (KAS) wanatimiza miaka 50 hivi ukialikwa kwenye Jubilee ndio kongamano.

Mkuu Dr. Slaa amealikwa kwenye shughuli muhimu ya chama kinachotetea Demokrasia kwa wanyonge, hajaenda kupiga picha na kina 50 cent kama afanyavyo JK....
 
Mradi asije akaomba msaada hatuna shida na misaada,tuna shida na utaalam wa watoto wetu basi.
 
Back
Top Bottom