Dr Shein: Zanzibar ni ya waafrika na sio waarabu...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Written by
Makengeza // 23/12/2013 // Habari //RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Zanzibar ni nchi iliyo katika bara la Afrika ambayo ilipaswa kujikomboa na kuwa huru ili kujitawala wenyewe na si kuendelea kubaki chini ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza na vibaraka wao wa Kiarabu.

Dk. Shein alisema hayo jana katika uwanja wa mpira wa Shule ya Msingi Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akizindua matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) katika maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.


Alisema mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika baada ya kushindikana kwa njia ya demokrasia katika chaguzi kuu zilizofanyika mara tatu kuanzia mwaka 1957, 1961 na 1963 kama vile chaguzi za 1995,2000,2005 na 2010 zilivyofanyika na kukipora ushindi chama cha CUF.


Alisema mara zote hizo chama cha CUF kilishinda uchaguzi, lakini wakoloni wa bara wakishirikiana na wazanzibara walikinyima madaraka ya utawala.


“Kushindwa kwa CUF kulitokana na Wazanzibari kufanyiwa hila na mbinu chafu na wakoloni wa bara na hili likifanyika tena 2015 vijana wetu watatumia ujasiri na kumwaga sera ili kuleta ukombozi na uhuru kamili,” alisema..


Aidha, aliwataja wana mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume, na mwanawe Dr Karume, Maalim Seif na mzee Hassan Nassor Moyo kwamba wao na wanachama wao wamekuwa na mshikamano, mapatano na umoja wenye nguvu utakaowasaidia kuwashinda wakoloni wa bara.


“Wamefikwa na majaribu mengi ya kutaka kugawanywa na kufukuzwa kwenye vyama, wameshikamana pamoja, hawatayumba na hawatakukubali kudanganyika ili waendelee kubaki chini ya utawala wa bara, watapata ukombozi unaohitaji kulindwa,” alisema.


Awali, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alisema baada ya chama cha ASP kuchoshwa kutawaliwa, walijenga ushupavu na kuwa zaidi ya silaha zilizouondosha utawala wa kisultani wa Kiomani ambao bado wana tamaa ya kurudi tena kutawala kwa kupitia SOOZA na taasisi nyengine.


Maoni Wasemavyo Wazanzibari Waliohojiwa...


Ghalib 23/12/2013 at 5:56 um · Ingia kujibu
Pimbi hajui nini anaongea.


 1. Makame Ame 24/12/2013 at 5:52 mu · Ingia kujibu
  Jee hii ina maana Cuba ni ya Waamerika, Uingereza ni ya wa Uropa, Maldives na Sri Lanka ni ya Waasia, Japan na Philippines ni ya Waasia, New Zealand ya Waawstralia. Seychelles? Mauritius? Na mifano mingine kemkem.
  Ningependa kutafantiana kimawazo
  Africa ni ya Waafrika regardless
  Zanzibar si ya Waafrika
  ZANZIBAR ni ya WAZANZIBARI regardless
  1. Awami 23/12/2013 at 11:36 um · Ingia kujibu
   Dr sheni anatukumbusha mengi miongoni ya maneno aliyokuwa akiyatumia Julias Borito Nyerere ,Mzee borito Nyerere alikuwa anatumia fulani anapotowa dukuduku lake na yanayomkeza katika dini ya Kisilamu bna waisilamu kwa mfano ,mahali anpotaka kuonesha kuwa dini ya Kisilamu na waisilamu ni watu wabaya hutumia neno warabu lakini anapoendelea zaidi unagunduwa amelenga Uisilamu ,,Dr Shein sio wa mwanzo na hatokuwa wa mwisho kuna viongozi wanao sadiki kusema warabu wabaya wameleta biasha ya utumwa ,wamefanya hivi na vile wabaya sana lakini cha kushangaza ukiwauliza sasa hivi hawa watu ni wabaya na wameleta mambo mabaya inakuwaje umekubaliana na Dini walio ileta ?na kwanini usifanye uwamuzi wa kuondokana nayo kuna mambo magumu ndani ya dini waliyokuja nayo kama vile kufunga sala tano kwanini ujikubalishe na hali hiyo ?Ningemuoba Dr Sheni pia awambie watu kuwa Dini ya Kisilamu ni Dini ya warabu na wao ndio waliyo ileta hapa Visiwani na sio ya wafrica nafikiri angesaidia pakubwa sana.
   Makame Ame 24/12/2013 at 4:46 mu · Ingia kujibu
   UGOZI, UGOZI, UGOZI…hiyo ndio sera tangu kuundwa kwa ASP na JKN mwaka 1957. Hakuna jipya na dhuria zimerithi uzuri.
   Lakini Shein na wafuasi wako wa mungu wa kiafrika, Kumbuka Mola Bwana wa viumbe vyote anasema..
   يا ايها الناس انا خلقناكم من ذكر وانثى وجعلناكم شعوبا وقبائل لتعارفوا ان اكرمكم عند الله اتقاكم ان الله عليم خبير
   O mankind! Lo! We have created you male and female, and have made you nations and tribes that ye may know one another. Lo! the noblest of you, in the sight of Allah, is the best in conduct. Lo! Allah is Knower, Aware.
   Zanzibar ni ya Wazanzibari ikiwa weupe ikiwa weusi ikiwa manjano ikiwa maji ya kunde au rangi yoyote ile. lkiwa wewe unayo haki ya kuwa mzanzibari basi na wengine wenye sifa kama zako waliotokea kwengineko kusiko Africa wana haki hiyo vile vile. Maneho yako hayatoweza kuwanyima haki hiyo pamoja na uraisi wako. Huko kwako ni kujidanganya na kuukataa ukweli. Na hilo halisaidii. Hii ardhi ya Allah SWT. Rejea kwa Mola wako kwa kupunguza kibri.
   1. Arshad25/12/2013 at 5:27 mu · Ingia kujibu
    Aliposema maneno yale, palkuepo na watanganyika wengi pale uwanjani kwa ajli ya matembez, hivyo labda alkua anawapa moyo na wao wajione wapo kwao.
    Lakn kasahau kua wenyewe kamili wapo.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,953
2,000
Hii habari imeandikwa kwa kuchochea tu.
Kama maneno ya Mkoloni mweusi wa bara yametoka kinywani mwa Dr Shein basi hana sababu za kubaki CCM.
Alipaswa kuitisha uchaguzi ili haki itendeke.

Kama maneno hayo ni ya Shein basi hana sababu ya kutuma wajumbe wahudhurie bunge la katiba kwani kufanya hivyo ni kumkubali mkoloni mweusi.

Kama maneno hayo ni ya shein basi hapaswi kuwa makamu mwenyekiti wa CCM iliyopora znz uchaguzi.
Na kama maneno hayo ni ya Shein, alipaswa atangaze kuondoa vyombo vya ulinzi vyote katika muungano na aunde vyake.

Mwaka 2010 alikuwa makamu wa rais wa JMT kwahiyo alishiriki upooraji kama kweli hayo ni maneno yake

Waznz hawana sababu ya kutawaliwa na mkoloni mweusi. Fursa mbili zimepita na ya mwisho inakuja. Hawapaswi kukanyaga bara kwenye bunge la katiba. Shein aitishe BLW haraka na kumtuma mwanasheria mkuu apeleke mswada wa kuvunja muungano.

Kama kayasema hayo basi alipaswa kwanza azuie CUF na CCM wasiende bungeni Dodoma.
Kama kayasema hayo na kaachia kila jambo liendelee kama lilivyo basi ni dhahiri yeye na wznz wamekubali ukoloni mweusi wa bara, watulie kimya, waje Dodoma warudi Znz kimya.

Ninajua haya si maneno ya Shein ni maneno ya wznz ambao kwao wanadhani kila mmoja ni mznz na anaweza kuelezwa lolote akaamini. Ni wale wanaowaaminisha wznz kuhusu znz ya makaimati na pilau mwaka 1950 hadi 1963.

Kwetu sisi tunasema Mkija Dodoma mumekubali, basi yaishe. Msipate tabu za kuandika uongo, nendeni Malindi mkazuie wabunge, mawaziri, na wajumbe wa bunge la katiba, mtaipata znz ya neema. Kupiga kelele na kuzua uongo havitawasaidia maana mwisho wa siku mtarudi kwa mkoloni mweusi wa bara kwasababu hamtaki kujikomboa.

Mna hiari kunyoa au kusuka sisi bukheri hatuna shaka.
Tuacheni tupumue

JokaKuu Jasusi Mchambuzi Nape Nnauye
 
Last edited by a moderator:

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,776
2,000
Natumaini katika mbingu na ardhi hii haya maneno hayakutoka kwa Shein. Nasubiri Wazanzibari wayapandishe kama video ili tusikie wenyewe kabla hatujafunguka.

hakika.kwa mtu kama shein ni.vigumu kutoa.maneno makavu kiasi hicho. walete video tuone.ushahidi
 

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,050
1,225
Pia Zanzibar ni ya Wakristo na sio Waislam. Kama hujui historia usibishe bali omba darasa nikupe.
 

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,288
1,195
Hapana.. Hapana.. Hapana.. Haya maneno sio ya Dr. Ally Mohammed Shein.. hizo ni porojo za kidebwedo tu!
 

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,128
2,000
Zanzibar ya wote warabu, wahindi,waafrika na kila anaejihisi kuwa yeye ni mzanzibari,tukumbuke warabu walipofika zanzibar,zanzibar ilikuwa na jumla ya watu wasiozidi elfu ishrini(20,000),warabu walileta wahindi,warabu pamoja na wazanzibari wenye asili ya kihindi na wenye asili ya kiafrika wakaijenga zanzibar,ikawa kama ilivyo sasa.

Kubuka sio wazanzibari walikuwa na asili ya kiarabu au kihindi ndio waliokuwa matajiri au wenye ulwa walikuwepo wazanzibar kama akina TipTip ambao walikuwa na ulwa na utajiri wakati walikuwa sio warabu au wahindi......hizi propanganda za kisiasa ni mbaya sana kwa zanzibar na Tanzania kwa ujumla

Raisi wa zanzibari akisema kuwa zanzibar ni ya watu weusi ni sawa na kuwabagua raia wake mwenyewe,
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,953
2,000
Zanzibar ya wote warabu, wahindi,waafrika na kila anaejihisi kuwa yeye ni mzanzibari,tukumbuke warabu walipofika zanzibar,zanzibar ilikuwa na jumla ya watu wasiozidi elfu ishrini(20,000),warabu walileta wahindi,warabu pamoja na wazanzibari wenye asili ya kihindi na wenye asili ya kiafrika wakaijenga zanzibar,ikawa kama ilivyo sasa.

Kubuka sio wazanzibari walikuwa na asili ya kiarabu au kihindi ndio waliokuwa matajiri au wenye ulwa walikuwepo wazanzibar kama akina TipTip ambao walikuwa na ulwa na utajiri wakati walikuwa sio warabu au wahindi......hizi propanganda za kisiasa ni mbaya sana kwa zanzibar na Tanzania kwa ujumla

Raisi wa zanzibari akisema kuwa zanzibar ni ya watu weusi ni sawa na kuwabagua raia wake mwenyewe,
Jamani mbona hamuoni mchana? Mna uhakika maneno hayo kayasema Shein? Hilo ndilo swali muhimu.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,371
2,000
dr.shein sio mjinga kiasi hiki,yaliyomkuta jumbe hakuna mzanzibari anayeweza kuyahimili..nitakuwa wa mwisho kuamini utunzi huu.
 

Mike 1234

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
1,633
0
jamani jamani mbona tunapenda kuchafua viongozi wetu,kweli Dr Shein azungumze haya! hapana hapana!
 

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,122
2,000
Shein hawezi kuongea upuuzi kama huo. Ni vyema tukatumia kwa busara uhuru wa kutoa habari hapa JF. Tuwe makini. Tusichafue heshma ya JF.
 

K A B U R U

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
658
1,000
Hao waruka sarakasi tu yakheeee....! kiboko yao Dodoma, walitambua hilo atiii........! zingine mbwembwe tu za kupanga maneno na kufurahisha maskani za gahwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom