Dr Shein weka mashine ya ukaguzi bandari ya Zanzibar kwa abiria wanaotoka Dar au wanaokwenda Dar

lutemi

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
1,747
1,385
Mpendwa Rais Dr shain. Naomba sana weka mashine ya ukaguzi bandari ya Zanzibar kwa abiria wanaotoka Dar es Salaam au wanaokwenda Dar es Salaam. Inatia aibu unafungua begi wale maaskari wanaangalia mpaka machupi machafu alafu hawajavaa hata groves hii wanahatarisha Afya zao alafu pia Zanzibar ni tourism attraction unapokea mataifa mengi sana basi naomba ufunge hizo mashine.

Nimeongea na mmoja wa Askari amesema wamesema weee lakini hawasikilizwi wanaomba nasi tuwasemeee.

Hii inatushushia hadhi
Kwanza hata upekuzi wenyewe sio mzuri huwezi ona chochote wanachokikusudia kwa upekuzi ule uliopo bandarini.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Zanzibar
Mungu akubariki Dr again Rais wa Zanzibar
Ahsante kwa kuchukua hoja hii na kuifanyia kazi kwa haraka na kwa unyeti wa jambo hili.
 
Hili jambo linakera sana. Tena wana utaratibu wa hovyo sana. Kwanza in short hakuna utaratibu wa kufata, sasa usiombe ukakuta kuna meli/boat mbili au tatu zimekuja kwa wakati mmoja. Utatamani kutapika.. Naonaga watalii wanabokua disgusted na hii jambo. Yani mara elfu moja upande ndege ila sio boat
 
Ule ni upuuzi kabisa. Ni bora kutokagua kabisa kuliko kutia tia mikono mizigo.
Si ustaarabu na ushamba. Hii ni 2017. Ila nahisi wanasubiri Bahresa awawekee nashine kama alivyowajengea hiyo bandari.
Hata wale askari wa uhamiaji sioni kazi yao pale. Yaani unakagua nini na mtu yupo Tanzania?
 
Back
Top Bottom