Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wanabodi,

Baada ya kupitishwa kwa katiba mpya tuipendayo ya serikali mbili, watu wote wenye hoja za serikali tatu, ni watu wa hatari sana kwa mustakabali wa taifa hili.

Mmoja wa watu hawa ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, huyu ni mtu hatari sana kwa mustakabali na majaaliwa ya kupitishwa kwa hii "Bora Katiba" kwa upande wa Zanzibar, hii ni kufuatia Mwanasheria huyo, kutetea hoja ya serikali tatu, inayolinda maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa mabadiliko halali ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, ambayo ni halali Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, lakini mabadiliko hayo ni haramu na kinyume cha katiba ya JMT.

Mabadiliko hayo ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, yameitambua rasmi Zanzibar kama ni nchi, na kulimega eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyemela na kinyume cha katiba ya JMT, na kuliita ni mipaka ya nchi ya Zanzibar, ambayo sasa Zanzibar ni nchi ndani ya nchi!, kitu ambacho ni kinyume kabisa cha katiba ya JMT ambayo inaitambua Zanzibar kama sii nchi, bali ni sehemu ya JMT, nchi ni Tanzania Pekee!.

Kwanza mwanasheria huyo, alipeleka hoja 17 za kuutetea ile haramu iliyofanywa na marekebisho ya katiba ya Zanzibar, kuiita Zanzibar ni nchi, kitu ambacho kwa mujibu wa katiba katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni haramu!. Kisha huyu jamaa akataka hiyo haramu kuigeuza halali, kwa kuilazimishia kwenye katiba mpya!, wajumbe makini wa kamati ya uandishi wa katiba wakiongozwa na mmoja wa viongozi waadilifu sana nchini, ambaye watu wenye husuda, wanamuonea tuu kijicho na wivu dhidi tujisenti twake, Mheshimiwa sana, Shujaa, Mtemi Chenge!, wakavitupilia mbali hivyo vipengele 17 haramu ndani ya katiba ya Zanzibar, visiingizwe kwenye rasimu ya katiba mpya!. Mwanasheria huyo hatari, aliyetaka kuvichomekea, ili kuigeuza haramu hiyo ya Zanzibar kuwa halali!.

Baada ya haramu hiyo kukataliwa na kupigwa chini pale Dodoma, huyu jamaa alikasirika sana baada ya kugonga mwamba, hivyo alisusa!.

Baada ya hilo kushindikana, kwanza akajitoa kwenye kamati ya uandishi wa katiba, akabakia Dodoma akiranda randa tuu!, ulipofika wakati wa kupiga kura!, kwanza alisusa kupiga kura ile siku ya kwanza ili hali yuko Dodoma, siku ya pili pia akasusa!, ila kabla ya upigaji kura kufungwa rasmi, sijui shetani gani, akamtembelea, mara akaingia bungeni mbio mbio na kuomba kupiga kura ya wazi!, Muungwana Sitta, akamkubalia!, ningekuwa mimi, kamwe nisingemkubalia!

Na baada ya kukubaliwa, si ni ndio akafanya kituko kile cha mwaka cha kupiga kura ya wazi ya hapana iliyohatarisha kupatikana kwa katiba yetu tuipendayo!, yaani just imagine, ungekuwa sio ule utaratibu wa "zisipo tosha zinatosheshwa!", hali ingekuwaje kwa watu hatari kama hawa mpaka sasa, bado wapo ndani ya serikali hii huku wameachwa tuu hivi hivi?!.

Kama Hamid ambaye ni shemeji kabisa wa Rais Karume, alifutwa kazi mara moja, na kutimuliwa kama mwizi toka ndani ya kile tukipendacho, chetu Chama cha Mapinduzi!, sasa huyu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, yeye ni nani haswa, aipinge serikali ya CCM!, iweje mpaka saa hii bado yuko kazini?!.

Kwa kadri anayoendelea kubaki kazini, ndio alivyo na chances kubwa zaidi kumwaga sumu kama hii, dhidi ya hii katiba mpya tuipendayo!, namshauri, rais Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein, amfute kazi haraka na mara moja, Mwanasheria Mkuu huyu, kabla hajaeneza zaidi sumu hii, na aende akaungane rasmi na kile chama cha kutetea serikali, tatu zinazotaka kutuvunjia huu muungano wetu adhimu!.

Kwa msiozijua hoja za sumu kwa serikali mbili, za Mwanasheria huyu Mkuu wa Zanzibar, hebu msikilize hapa!.


Kamati ya Maridhiano Six:MWANASHERIA OTHMAN MASOUD AUCHAMBUA MUUNGANO NA KATIBA MPYA
Paskali
 
Last edited by a moderator:
Dr. Shein na Mwanasheria mkuu ni kitu kimoja, support kubwa wanapata toka kwa maalim seif na Karume. Anachokifanya Mwanasheria mkuu kina baraka zote toka ikulu ya znz.

Kuna taarifa chini ya kapeti kuwa, huenda Dr. Shein asipewe kipindi cha pli cha uongozi kwa kuruhusu haya yaliyotokea.
 
Great thinker Pasco unanifurahisha sana na uandishi wako!
Nina hakika sio kila mtu anaposoma kichwa cha habari anaelewa unachokizungumzia.
Ni uandishi mzuri sana wa fasihi iliyotukuka ambayo maudhui na ujumbe vimefichwa ndani ya riwaya!
Mwenye macho ya kuona yaliyofichwa na aone, na mwenye masikio na asikie!
Asante sana Mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Wakija Lb7 hapa bila ya kusoma vizuri watashabikia kweli kweli ,tunakushukuru mkuu kwa janja ya nyani uliyoionesha katika uandishi wako.
 
Mwanasheria gani huyo ambaye hata ethics za taaluma yake hazijui?

ethics za taaluma yake.ni zipi?ama ni kukubali kila kitu hata kama hakifai?au ni kufuata mkuu wako hata kwa mambo yasiyofaa?maadili ya taaluma yoyote yapo kwa ajili yako na watu wote na wala sio kwa ajili ya mtu fulani.hii ni demekrasia,kila mmoja anahaki ya kutetea analoliona lina manufaa kwa wote
 
Back
Top Bottom