Dr shein mfupa uliomshinda fisi, mbweha hauwezi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr shein mfupa uliomshinda fisi, mbweha hauwezi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 9, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  Written by Stonetown (Kiongozi) // 09/02/2011 // Makala/Tahariri // 5 Comments

  [​IMG] • MAFUTA YETU HATUTOI NG’O!
  Na: Malik Nabwa
  Kama kuna kitu kilichopangwa na kushuhulikiwa kwa umakini mkubwa hapa nchini ni Muunagano wa Tanzania na Zanzibar. Yaani kila kitu ambacho bara wanakifanya juu ya Muungano basi huwa ‘’very strategic’’ kiasi ambacho mikakati hiyo inavyopangwa kwa umakini mkubwa laiti ingekuwa inatumiwa kuleta maendeleo ya Taifa basi Taifa hili lingekuwa mbali kimaendeleo.
  Mara kadhaa tumejaribu kuonesha kuwa muungano wa Zanzibar na Tanganyika haukufanywa hata kwa chembe moja ya nia njema. Naufananisha kabisa na mungano wetu na chama cha wachawi huko Ging’ingi. Kwa anaewafahamu wachawi vizuri basi umoja wao huwa hauko katika nyoyo zao bali hamu na matakwa ya nafsi zao tu. Wachawi hawana chembe ya nia njema wala upendo kati yao na walivyonavyo kwa mfano watoto wao au hata familia zao. Hivi ndivyo ulivyo Muungano kwa wenzetu wa bara dhidi yetu.Ni chama cha wachawi tu kila mtu ana lengo lake tena leno baya dhidi ya mwenzake.
  Tumeona kuwa msingi wa kuungana kwetu ulikuwa wa magube matupu. Kwanza hakukuwa na ulazima wa kuungana kwani ukiungana na mchawi lazima siku moja atakuliza tu au kukutia wanja jicho moja, tumulize shekh Karume kama tunataka ushahidi juu ya hili. Pili, mara tu baada ya Muungano tulishuhuduia mambo kadhaa ya kuipora Zanzibar kuwa nchi na kujitegemea kwake. Tuakunganisha vyama na kila kitu. Ikafika wakati lazima kila kitu kiamuliwe bara. Hii ndio taswira halisi ya Muunagno wa kinafiki sawa na muungano wa Kichawi. Muungano usio na nia njema siku zote hukimbilia msihipa ya kuvutia pumzi ya mwenza wake na kuidhibiti. Ikishafanya hivyo mwenye kuzibwa pumzi lazima atii amri na akishindwa basi hana hiari ila ni kufa au kukosa kila kitu kabwi na mtindi. Muungano wetu sisi Wazanzibari umetufikisha hapa.
  Si vibaya tukijikumbusha kidogo ajenda za siri za Muungano kutuchagulia viongozi wa juu kama moja ya mbinu yao ya kuendelea kututawala na kuimaliza mirija michache ya kuvutia pumzi iliyobaki tuanzie na Raisi wa Kwanza. Raisi Karume alipokuja tanabahi tu kuwa kujiingiza katika Muungano lilikuwa kosa la jinai akataka kujitoa pale alipoanza kubwatuka hadharani; ‘’muungano mwisho Chumbe’’ huku akisahau kuwa ukishaingia uchawini huwezi kutoka. Yaliyomkuta ndio yale. Mauaji yake yalikuwa hayahitaji uchunguzi wa CIA,FBI, KVB, wala Scotland Yard.
  Nini kilitokea baada ya kikwazo cha kuendeleza Ubabe wa kutaka kuung’oa Muungano kuondoka yaani baada ya kifo cha Sheikh ‘’K’’. Dodoma ilipanga nani ni mtu wao atakaeweza kutimiza azma yao ya kuidhibiti mirija muhimu ya kuvutia pumzi ya Zanzibar na kuiweka chini ya himaya ya Muungano. Akaletwa Jumbeambae alikuwa mwenzao badala ya Sefu BAKARI alietakiwa na Baraza la Mapinduzi lenyewe. Kwa upande mmoja ilikuwa shufaa kuwekwa Jumbe kuliko Sefu Bakari maana japo Seifu alikuwa hana malengo na Muungano lakini alikuwa kichwa maji kuliko hata Karume kwa hiyo hata angewekwa yeye tusingepata shufaka yoyote. Afadahali huyo Jumbe ni anagalau afadhali ya kung’twa na nge ukakoswa na tandu, wala si afadhali kitu maana mchawi ni mbaya tu hata awe vipi.
  Muungano ulifanikisha azma yake kwa kumuweka Jumbe. Baada ya kupandikiza mtu wao huyu wakajichukulia hatua moja muhimu ya kuudhibiti mshipa mkuu wa pumzi wa Zanzibar. Nao ni pale Jumbe alipokubali Kuunganisha vyama na Nyerere mwaka 1977. Katika kosa kubwa katika historia ya Zanzibar ni hili alilolifanya Jumbe (The grave mistake over Zanzibar future stake in the Union). Kwa kuunganisha Chama ndio alijimaliza yeye mwenyewe kama Rais kamili wa Zanzibar na pia ikawa kashaiondolea kinga dola ya Zanzibar. Kuanzia hapo ndio Zanzibar ikawa ni sehemu tu ya Jamhuri ya Muunagano.
  Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa ngoma ya kichawi haina mwisho mwema. Mwema wako leo kesho ndie mbaya wako wa mwisho. Jumbe akawa amejitia kitanzi mwenyewe na bila kinga wala hifadhi akatolewa kikoa katika hali ya aibu kabisa na idhilali. Haya ndio malipo ya kushirikiana na watu wabaya. Tukumbuke kuwa Nyerere alimtimua Jumbe baada ya kuhakikisha ameshashikilia maeneo muhimu ya Zanzibar. Kwa mfano kama Jumbe hakuunganisha vyama Nyerere angepata nguvu wapi ya Kumfukuza? Lengo lake ikawa limefanikiwa.Kinachofuata sasa ni kung’atuka maana ‘’mission accomplished’’.
  Awamu iliyofuata Nyerere alikuwa amemaliza kazi na akaamua kung’atauka akiamini kwamba adui yake hafurukuti tena ni wa kuchinja tu. Kwa sababu hadi hatua hii yeye alikuwa ndie mwenye maamuzi ya nani aongoze Zanzibar na kwa kukamilisha azma ipi ya Muungano wa kunufaisha bara. Akamleta Mwinyi. Alipoona ana manufaa haraka akamuondosha na kumuharibu roho hadi akamuacha kuwa ni mchawi mbaya kuliko Bi Kirembwe. Tuakaletewa Idirisa, ikawa sawa na mlango wa gunia maana sio wa kumbesa angalau. Ikawa mijambo ya Muungano inajazwa kapuni hadi kufikia ishirini na nne. Nyumba haina mlango na ndani ina mali lazima wajanja waiiibe tu.
  Tukaletewa Komandoo. Akatugawa, akatutia chuki, akatutesa, kisha akaondoa pasipoti ya Zanzibar na kutuingiza TRA. Ikawa hatuna tulichobakisha. Uchaguzi wa mwaka 2000 Dr. Gharibu Bilali akawa chaguo la Zanzibar lakini ikawa hayumo katika mizani ya watu wa Muungano wakiamini kuwa maleno yao yasingeweza kutimizwa pindipo akikaa Bilali huyo. Bila kutegemea akaletwa Dr. Karume wakiamini atakuwa mtumishi mwema na mtiifu kwao
  . Nae akaboronga hadi siku moja alipozinduka akatuachia maridhiano na kutuonesha ukweli na njia ya kujikwamua na ngoma hii ya Kichawi. Lakini aingiae Uchawini nasikia hawezi toka sasa vipi? Dr. Karume alituuza sana lakini atakumbukwa kwa kuwa madhubuti katika suali la mafuta Zanzibar. Alikataa katakata kuyatoa mafuta kuwa mali ya Muungano. Hili likawa kosa kwake lakini ikawa keshamaliza muda wake.
  Uteuzi wa Dr. Sheni kuwa mgombea Urais Zanzibar hakuna alieutegemea. Lakini Dodoma ni watu ‘very Strategic’. Walijua kuwa bila kumuweka kibaraka wao mafuta yatashindikana. Akaletwa Dr. Shein ambapo kwa imani yangu asingepata hata kura nne za kamati kuu hapa Zanzibar. Kilichotumika ni kile alichotuachia Jumbe, kuunganisha vyama na maamuzi makuu ya chama yakotoka Dodoma. Dr. Sheni akaletwa tu kapuni kutoka Dododoma kama vile nyama ya kasa pakachani. Anaetaka kula kasa atakula na asietaka basi japo vumba atanuka lakini ikawa kasa hakwepeki.Ndio kitoweo alichochaguwa baba na mama kakaubali kukipika, mtoto hana hiari hapo, atasusa lakini kasa ndio kitoweo.
  Nionavyo na ndivyo ilivyo Dr. Sheni hakuletwa ili kuja kuwa Raisi wa kwanza Mpemba kama watu wanavyodai kuwa mara hii ni zamu ya Mpemba. Kwanza sisi Wazanzibari hatuna haja ya Raisi Mpemba au Muunguja bali tunataka Raisi mwenye uchungu wa Zanzibar na watu wake. Tafauti na Dodoma wao wanataka Raisi asie na uchungu wa Zanzibar wala watu wake. Na kwa awamu hii ya Saba mtu huyo alikuwa ni Dr. Sheni tu. Nasema Dr. Sheni kaletwa kuja kukamilisha ajenda moja tu ya kumaliza suali la mafuta kuwa mali ya Muungano. Nasema kuwa hili ndio jambo kubwa aliloletwa yeye hapa na anafanya kila aliwezalo kulikamilisha hili.
  Juzi katika kikao na baraza la Mawaziri huko Rais alichomekea suali hili akitafuta kuungwa mkono humo. Matokeo yake hakupata mgawiko bali nguvu ya baraza lote lilikataa ukiachilia mbali mawaziri wachache mno. Na kwa muundo wa baraza la Mawaziri ulivyo Dokta Sheni hawezi kufanikiwa kamwe juu ya hili. Hawezi kufanikiwa pamoja na kuwa tayarai alishapewa mpango na njia ya kulifanikisha hili. Moja ikiwa ni kuunda Serikali kubwa yenye Mawaziri na makatibu wakuu wengi wenye nguvu katika Muungano na mahafidhina akitegemea kuwa watamuunga mkono. Pili, kitendo cha Bi Samia Suluhu kuwekwa Waziri wa muungano, na Nahodha mambo ya Ndani bara ni sehemu ya mkakati wa kumrahsishia Dr. Sheni azma yake hiyo ya kuyahaulisha mafuta kuwa mali ya Muungano sasa. Tatu, utagundua kuwa uteuzi wa makatibu wakuu, na wakurugenzi umzeingatia zaidi uchama kwa kuchagua zaidi watu wenye mtazamo na sura ya Kimuungano muungano akidhani kuwa hawa wote watakuwa ngao kwake kwa ule wingi wao Serikalini. Lakini kiuhalisia yote haya hayawezi kumnusuru Dr. Sheni wala kumuwezesha kufanikisha azma yake.
  Azma ya Dr. Sheni itakuwa ngumu kufikiwa kwa sababu nyini; kwanza kwa kuwepo hii Seriakili ya Umoja wa Kitaifa na baraza mchanganyiko la mawaziri ambalo ndio nguvu kubwa ya Dr. Sheni. Ieleweke kuwa kabla ya hata huu mseto CCM na CUF kwa suali la mafuta walikuwa kitu kimoja na hawakuwa na ubishi juu ya hili. Leo hii ambapo Mawaziri wa CCM na CUF ni masahibu wa kweli wenye kuungana na kuwa na misimamo thabiti na kauli moja ya kuinusuru Zanzibar, itawezekanaje waikubali hoja ya kuyatoa mafuta kwenda Muungano? Hili Dr. Sheni asilitarajie maana hata kwa Mawaziri mahafadihina na wakali akina Shamuhuna basi hili hawalitaki kabisa. Kwa maana hii ni Wazi Dr. Shein Hawezi kufanikiwa kwa hili iwapo atategemea ridhaa za mawaziri wake.
  Iwapo Dr. Sheni anaepigania kulipa fadhila huko Dodoma, anataka kufanikisha hili basi kuna njia moja au mbili tu za msaada kwake. Kwanza, Kutumia kauli mbiu yake ya kuwa ‘’Silazimiki kusikiliza ushauri ninaopewa’’ na kujiamulia moja kwa moja tu kama Raisi kuyachukua mafuta na kuyapeleka Dodoma bila ya kutaka wala kufata ushauri wa yoyote. Njia ya pili, ni kulivunja baraza la Mawaziri ambalo linaghalifiana nae.Lakini isomeke kwamba kulivunja baraza hili ni kuvunja maridhiano pia maana itamlazimu kuunda baraza jipya ambalo bila shaka ni la watu wanaomuunga yeye mkono tu na kwa maana hiyo ni wazi hakutakuwa na mawaziri wa Upinzani humo. Kama hili ataliweza na wananchi wakaendelea kukaa kimya basi tuseme ‘’mafuta Good-bye’’, Zanzibar arijojo!
  Bila ya hivi, Dr. Sheni itamlazimu atafute mbinu mbadala ya kulipa fadhila maana Zanzibar mpya haiko tayari kutoa tena hata unyusi wake kuwa mali ya Muungano kwa sasa sembuse mafuta. Nachukuwa fursa hii adhimu kumtanabahsiha Dokta Sheni kuwa mfupa huu uliwashinda fisi kwa hiyo hapana shaka mbweha huwataweza kuula. Na hicho kikombe ulichokuja nacho toka Dodoma kutilia mafuta kitarudi huko na singo la karafuu tu, ndio zawadi pekee tuwezayo kumpa mgeni kwa sasa na sio hata tone moja la mafuta. Hongereni mawaziri na Wawakilishi wetu kwa misimamo yenu! Tuko pamoja na inshaalwah hili halitafanikiwa milele.
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  so kama mnajua matatizo yoote ya Muungano ni kwaajili uwepo wa CCm, sasa kwanini mlikubali serikali ya umoja wa kitaifa? na pia kwanini mlimchagua huyo Shein badala wa maali hamad? mnajua hata nyie wenyewe wazeji ni wanafiki sana na ndio maana mpaka leo mnashindwa kuungana na kufanya maamuzi pamoja kwa maslahi ya nchi yenu, kwa upande wetu sisi watanganyika wanaharakati hatuutaki kabisa hup muungano na CCm yenu.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu toeni tuu hayo mafuta huu ndo muungano bwana! Tugawane woote acheni uchoyo!
   
Loading...