Engineer Mohamed
JF-Expert Member
- Jul 27, 2007
- 451
- 11
Shein aenda Denmark, Uingereza
2008-04-15 10:33:26
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, jana aliondoka nchini kwenda Copenhagen, Denmark na London, Uingereza kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na ofisi ya Makamu wa Rais ilieleza, akiwa nchini Denmark, Dk. Shein atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kwanza wa Kamisheni ya Afrika unaotarajiwa kufanyika kesho.
Kamisheni hiyo ya Afrika ambayo imebuniwa na serikali ya Denmark, inalenga kuyapa msukumo na kipaumbele masuala ya ukuaji wa uchumi na ajira barani Afrika katika ngazi ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mbali na kuhudhuria kikao hicho, Makamu wa Rais pia atakutana na baadhi ya viongozi wa Denmark akiwemo Waziri Mkuu Bw. Anders Fogh Rasmussen na Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Per Sting Moller
Nchini Uingereza ambako atawasili keshokutwa asubuhi, Dk. Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa uwekezaji ambao utafanyika baadae mchana na jioni atahudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yake na waandaaji wa mkutano huo.
Siku inayofuata Makamu wa Rais atazindua `forum` ya watanzania waishio nje ambapo anatarajiwa kuelezea dhamira ya serikali ya kushirikiana na kusaidia namna Watanzania waishio nje wanavyoweza kutoa mchango wao katika maendeleo humu nchini.
Makamu wa Rais anatarajiwa kurejea nchini Jumamosi ijayo.