Dr. Shein: Hakuna wa kuniondoa madarakani

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema hakuna nchi au jumuiya za kimataifa zitakazomwondoa madarakani yeye kwa sababu amechaguliwa kihalali na wananchi kwa kura nyingi kwa mujibu wa Katiba.

Dk Shein alisema hayo wakati akizungumza na wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika matawi ya Wesha Tibirinzi, Pembeni Shengejuu na Maziwa Ng’ombe, Micheweni katika ziara ya kuwafariji kutokana na matukio ya hujuma zilizofanywa na wapinzani huko Pemba.

Aliwataka wafuasi wa CCM na wanachama wake waliopo Pemba, wasibabaishwe na kauli zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa wanaopita na kudai kwamba uchaguzi mwingine unakuja.

“Mimi ndiye Rais halali wa Zanzibar nimechaguliwa katika uchaguzi ulioitishwa na Tume ya Uchaguzi... wananchi msisikilize uvumi na kauli za wapinzani zenye lengo la kuwababaisha na kuwayumbisha katika shughuli zenu za maendeleo,” alieleza Dk Shein.

Dk Shein alisema amesikitishwa na kauli za uchochezi zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa zenye malengo ya kuishajihisha jamii kutengana na kugombana na kususiana hata katika shughuli za jamii ikiwemo misiba.

Alisema kiongozi anayefanya vitendo vyenye lengo la kuwagawa wananchi kwa malengo ya kisiasa kwamba huyo ameishiwa na hana nafasi katika jamii. “Huyo kiongozi anayewashawishi wananchi kususia shughuli za jamii na maendeleo basi huyo ameishiwa kisiasa na hana nafasi katika jamii ya wananchi na ninyi mpuuzeni.

Alikuwa na nafasi ya kushiriki katika uchaguzi lakini alisusa,” alieleza. Alisema viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wameishiwa hoja kwa sasa na hawana la kufanya baada ya kugomea kushiriki katika uchaguzi halali wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu ambao umetoa nafasi kwa CCM kushinda katika uchaguzi wa kishindo.

Mapema Dk Shein ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM aliwataka wanachama wa chama hicho kutembea kifua mbele na kuachana na unyonge kwa sababu chama chao ndiyo kilichoshika dola na kuunda serikali.

Akizungumzia yanayotokea Pemba, Dk Shein alisema, “Nimesikitishwa na taarifa za matukio mbalimbali yanayofanyika huku Pemba ikiwemo watu kususiwa maiti, kushushwa katika gari za abiria baada ya kuwa na itikadi tofauti......haya matukio hayakubaliki na yanakwenda kinyume cha maamrisho ya dini zote.”

Aliwataka viongozi waliopewa majukumu kwa mujibu wa Katiba kufanya kazi zao na kupambana na vitendo vya ubaguzi ikiwemo vya kuonewa kiholela wananchi.
 
Baeleze baba, baeleze hao. Nchi inaongozwa na sheria.
 
Kwani yale magari yetu ya polisi yaliyojaa kipindi cha uchaguzi si tuyatumie kuea wananchi wetu wa ccm pemba kwenye shughuli za maendeleo
 
Tanzania ni nchi pekee duniani mwizi anauwezo wa kusimama mbele ya kadamnasi na kuwakebehi aliowaibia! Ni Tanzania tu ambako raia wake hawana aibu na hawana mshipa wa soni! Hivi hata mwanafunzi wa darasa la kwanza angeendelea kumsikiliza shain kweli? Kweli Marehemu Jomo Kenyatta alikuwa yuko sahihi kumwambia Nyerere anaongoza marehemu
 
anaongea hayo lkn moyoni mwake kunauma mbayaaa!!!! anajua kiasi gani anamkosea mungu sema basi atafanyaje na kishapigwa biti LA hatari?
 
Ni hivi,

Nchi hii na kwa kizazi hiki ni ndoto na hakitaweza na hakiwezi kuiondoa CCM Madarakani, nafasi kubwa kwa kizazi hiki ilikuwa October 25 mwaka 2015 lakini kizazi hiki hakikuitumia hii nafasi vizuri, hivyo CCM kushinda.
Siwakatishi wapinzani tamaa na wala si nia yangu hiyo ila ni lazima nieleze ukweli ili tuone tunaendaje huko mbele kwa Pamoja.

Uoga, Unafiki na Usaliti kwa kizazi hiki ndicho kikwazo kikubwa cha kutoingia madarakani mwaka jana, Kama hiki kizazi kingekuwa Jasiri mwaka jana, kwamba, hata kisiogope Mabomu, wala polisi, Upinzani ungeingia madarakani kilaini sana, tatizo la kizazi hiki kinataka eti kipewe Amri au tamko kwamba ingieni mtaani utadhani huyo mnayetaka uwaambie hana akili timamu...!!

Tukubali kwamba, kwa kizazi hiki, jamani CCM haiwezi kuondoka madarakani hakuna mtanzania mwenye ubavu wa kupambana na polisi na kuvumilia mabomu, hili Viongozi wa upinzani wanalijua vizuri sana ila huwa hawataki kulisema waziwazi ili wasiwakatishe tamaa vijana ambao bado wapo front.

Hata Kenya waliweza si kwa kupewa tu mezani, ila kwa kufight, lakini eti muitoe CCM kwenye makaratasi? hivi mnaijua CCM au mnaisikia? mm nimeijua mwaka jana nikaamua kurudisha majeshi yangu nyuma, maana kwa akili zangu timamu nimegundua kuwa CCM haiwezi kuachia madaraka kwa njia ya makarakasi labda kama itakuwa imelala usingizi wa pono.

Ni lazima Upinzani utafute njia nyingine ambayo utaiwezesha kuingia madarakani siyo kwa njia ya kura, mwenye akili timamu atakubaliana na mimi juu ya hili sipo hapa kuwakatisha tamaa makamanda waliobaki front vitani ila ni bora na ni vizuri kuelezana ukweli.

Kwanza, mtanzania ni mtu asiyehaminika kabisa na ni mtu mwenye maneno mengi kuliko vitendo, hivyo ndugu zangu wa Ukawa ni vizuri tubuni njia nzuri ya kuingia madarakani, mm nimekata tamaa kabisa kutumia njia ya kura kuingia Ikulu na hayupo wa kunishawishi kwamba njia hiyo inafaa kuwafanya wapinzani kuingia Ikulu, hakuna kitu kama hicho.

Hata kama Tume huru itakuwepo bado siyo guarantee ya upinzani kuingia Kuingia IKULU, kwa system ya nchi hii ilivyo si rahisi sana kama mnavyodhani kuitoa CCM madarakani.
 
Sometimes siasa Za Tanzania Ni Biashara.
 
Mkuu nakuhakikishia...

CCM haiwezi na haitaweza kutolewa madarakani kwa njia ya makaratasi tena kwa kizazi hiki, ni ndoto za mchana na za kudanganyana, hakuna kitu kama hicho, najua viongozi wanalijua hili swala vizuri sana ingawa hawataki na hawawezi kulisema waziwazi maana watu watakata tamaa.
 
Nkuruzinza bin Shein tena kwenye kashfa za kisiasa anadhidi kuonyesha ulimwengu his utarahamwe wa kiwango cha UDOM
 
Hivi huyu jamaa ukiachilia mbali ni daktari wa falsafa na pia ni mzee,sijui muislamu safi haoni hata aibu kusema hayo anayoyasema ??
 
Ni hivi,

Nchi hii na kwa kizazi hiki ni ndoto na hakitaweza na hakiwezi kuiondoa CCM Madarakani, nafasi kubwa kwa kizazi hiki ilikuwa October 25 mwaka 2015 lakini kizazi hiki hakikuitumia hii nafasi vizuri, hivyo CCM kushinda.
Siwakatishi wapinzani tamaa na wala si nia yangu hiyo ila ni lazima nieleze ukweli ili tuone tunaendaje huko mbele kwa Pamoja.

Uoga, Unafiki na Usaliti kwa kizazi hiki ndicho kikwazo kikubwa cha kutoingia madarakani mwaka jana, Kama hiki kizazi kingekuwa Jasiri mwaka jana, kwamba, hata kisiogope Mabomu, wala polisi, Upinzani ungeingia madarakani kilaini sana, tatizo la kizazi hiki kinataka eti kipewe Amri au tamko kwamba ingieni mtaani utadhani huyo mnayetaka uwaambie hana akili timamu...!!

Tukubali kwamba, kwa kizazi hiki, jamani CCM haiwezi kuondoka madarakani hakuna mtanzania mwenye ubavu wa kupambana na polisi na kuvumilia mabomu, hili Viongozi wa upinzani wanalijua vizuri sana ila huwa hawataki kulisema waziwazi ili wasiwakatishe tamaa vijana ambao bado wapo front.

Hata Kenya waliweza si kwa kupewa tu mezani, ila kwa kufight, lakini eti muitoe CCM kwenye makaratasi? hivi mnaijua CCM au mnaisikia? mm nimeijua mwaka jana nikaamua kurudisha majeshi yangu nyuma, maana kwa akili zangu timamu nimegundua kuwa CCM haiwezi kuachia madaraka kwa njia ya makarakasi labda kama itakuwa imelala usingizi wa pono.

Ni lazima Upinzani utafute njia nyingine ambayo utaiwezesha kuingia madarakani siyo kwa njia ya kura, mwenye akili timamu atakubaliana na mimi juu ya hili sipo hapa kuwakatisha tamaa makamanda waliobaki front vitani ila ni bora na ni vizuri kuelezana ukweli.

Kwanza, mtanzania ni mtu asiyehaminika kabisa na ni mtu mwenye maneno mengi kuliko vitendo, hivyo ndugu zangu wa Ukawa ni vizuri tubuni njia nzuri ya kuingia madarakani, mm nimekata tamaa kabisa kutumia njia ya kura kuingia Ikulu na hayupo wa kunishawishi kwamba njia hiyo inafaa kuwafanya wapinzani kuingia Ikulu, hakuna kitu kama hicho.

Hata kama Tume huru itakuwepo bado siyo guarantee ya upinzani kuingia Kuingia IKULU, kwa system ya nchi hii ilivyo si rahisi sana kama mnavyodhani kuitoa CCM madarakani.

Kama ungekuwa kiongozi wangu basi ningekuwa mfuwasi wako mtiifu.upo juu ya mstari wa ukweli.wenye akili zitumieni
 
Punda afe lakini mzigo wa tajiri ufike... hiyo ndiyo staili ya watawala wa kiafrika. Kwa hiyo hatushangai sana.
 
Back
Top Bottom