Dr. Shein awaapisha watendaji wapya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr.Shein awaapisha watendaji wapya wa serikali ya ya mapinduzi ya Zanzibar

===================================

DSC_2803.jpg


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kabla aklikuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji Uataswi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar,hafla ya kiapo hicho ilifanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,{Picha na Ikulu}

DSC_2773.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar,hafla ya kiapo ilifanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
DSC_2753.jpg

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Alina Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.


DSC_2871.jpg


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Ali (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma (kulia) baada ya kuwaapisha kushika nyadhifa hizo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Picha na Ikulu
 

Attachments

  • CVqIB4BWsAATdZM2.png
    CVqIB4BWsAATdZM2.png
    96 KB · Views: 211
Ni sawasawa.
Wanajaribu kumwekea rais Maalim Seif Shairiff speedgoveror.
Anataka akiondoka Seif afanye kazi na watendaji ambao ni loyal kwake.
Ni dalili za wazi kuwa anaondoka soon!
 
Ni sawasawa.
Wanajaribu kumwekea rais Maalim Seif Shairiff speedgoveror.
Anataka akiondoka Seif afanye kazi na watendaji ambao ni loyal kwake.
Ni dalili za wazi kuwa anaondoka soon!

Mkuu naamini kila rais anaye ingia ana uwezo wa kuteua team yake
 
Huwezi kufanya Dhulma ukaondoka duniani huku unacheka, Mungu atakuonesha tuu hata kama utafurahia miaka 50 ila wa 51 utadhalilika.
 
Back
Top Bottom