Dr. Shein atakuwa Rais pekee wa Zanzibar kuukumbatia Muungano na sera zake?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Historia ya kisiasa ya Zanzibar kuanzia tarehe 26 Aprili 1964 inaonyesha kuwa Marais wote wa Zanzibar waliopita katika muhula wa kumalizia hugeuka mbogo na kuukandia Muungano kwa kuupinga na kuukosoa na kukiri kuwa Muungano ni kikwazo kwa maendeleo na mustakabali wa Zanzibar
  • KARUME: Rais wa kwanza wa Zanzibar alionyesha kuchikizwa na muungano kwa kuzuia hata shughuli za Muuungano na maamuzi yake kufanywa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  1. Alikuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Muungano yaliokuwa Zanzibar. Alimkatalia Nyerere kupeleka majeshi ya JWTZ kutoka Zanzibar kwenda Msumbiji na Uganda kukabiliana na upinzani na kumwambia Nyerere kuwa "hakuna msaada wa roho"
  2. Alimfukuza Ikulu Waziri wa Fedha wa SMT marehemu Jamal na kumwita " mwizi wa kihindi"
  3. Muungao aliufananisha na koti na akawambia wananchi kuwa ilitubana tualivua.
  4. Mawasiliano a moja kwa moja baina ya Karume na Nyerere yalikatika kabisa
  5. Katika Mahkama iliokuwa isikilza kesi ya Mauaji ya Karume yalimtaja "Mr X"(jina lilihifadhiwa) kuwa ndio muhusika mkuu wa mauaji hayo.
  • JUMBE:Kama mtangulizi wake aliihoji uhalali wa Muuungano kwa hoja na kutaka kulipeleka swali la Muungano kwenye mahakama ya kimataifa kupatiwa usumbufu. Jumbe alisisitiza kuwa Muungano waliouhitaji Zanzibar ni " shirikisho" na sio kutawaliwa. Yalomkuta Jumbe tunayajua. Rais aliechaguliwa naazanzibari kwa asilimia 84% kunyofolewa nyadhifa zake zote na mtu mmoja ambae hata asili ya Zanzibar hana.
  • MWINYI: Pamoja na kuwa hakukaa sana kama Rais wa Zanzibar lakini alipandishwa cheo kuwa Rais wa Tanzania baada ya nchi kufilisika. Mwinyi alifanya uteuzi wa wazanzibari katika nafasi nyeti za wizara za Muungano na sizo za muungano. Aliitumia nafasi kutaka kuipeleka Zanzibar OIC. Aliwachukiza wengi hasa kanisa Katoliki
  • IDRIS: Rais mcha mungu wa vitendo. Alikataa dhulma kuifanyia Zanzibar iliopangwa na kuolewa maagizo na bara. Yeye alikuwa anapenda kujibu " ngoja nikawaulize wenyewe" na ndio huwa limetoka. Hakukubali kuendelea kubeba mashinikizo kutoka bara, alikataa kuendelea na muhula wake wa pili kwa mujibu wa KatibaI
  • Komandoo Dr.SALMIN:Rais wa Zanzibr mwenye mvuto na kujiamini. Nae pia alichoshwa na muungano. Nyerere alimwta mbogo Komandoo alimwambia yeye ni Karume mtoto. Kiberiti chake kimejaa. Hakuyumba na alipinga kufanywa Waziri kwenye baraza la mawaziri SMT na hakuhudhuria hata kikao kimoja. Alikitembelea kisiwa cha Fungu Mbaraka kinachotamaniwa na bara na kupachika bendera ya Zanzibar
  • Dr KARUME: Alionekana laini katika muhula wa kwanza lakini kama kawaida aligeuka mbogo muhula wa pili. Alimbia Kikwete hakuna mjadala kuhusu mafuta na gesi ya Zanzibar kuwa ni ya muungano.Alibariki SMT kuitwa wezi wa mchana
  • Dr.SHEIN: Anamaliza muhula wake, je atafuata nyayo za Marais wa Zanzibar waliomtangulia?
 
Back
Top Bottom