Dr Shein: Anabaguliwa?

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
833
Forget about Sumaye ambaye hana shughuli zaidi ya kupolute hali ya hewa na kumaliza tax payers maoney kwa kuzunguka kila kona ya nchi kasoro Unguja, Pemba na Mafia

Makamo wa Rais yeye naye yuko bored na hana cha zaidi ya kuzingua vitu ambavyo mtanzania wa kawaida havijui

Bwana Shein alivyokuwa bored sasa hivi kama una shughuli yoyote ya kuzindua kitu basi wee mwite itabidi tumuite "MZEE WA KUZINDUA"


Labda huyu ana get away with things kwani sijamsikia kabisa kwenye haya majina ya wala RUSHWA...hivi jamani huyu mtu ana mitikasi gani au ndio kama Al Marhum Dr OMAR ALI JUMA?

ZAIDI YA HAYO PROFILE YA DAKTARI SHEIN NI HII HAPA CHINI:



CURRICULUM VITAE

Name: Dr. ALI MOHAMMED SHEIN
Born 13/03/1948, Chokocho, Pemba, Zanzibar
Married with children



Education:
1956 – 1964 : Primary education at Lumumba College, Zanzibar. GCE “O” Level
1969 – 1970 : Preparatory Faculty, Voronezh State University, USSR; “A” Level

High Education
1970 – 1975 Undergraduate Course at Odessa State University, USSR
1984 – 1988 M. Sc. in Medical Biochemistry at the Medical School University of
Newcastle Upontyne England, U.K.
Doctor of Philosophy (Ph.D) inClinical Biochemistry and Metabolic Medicine,
specializing in “Inborn Errors of Metabolism”.

Others
1981 : Blood Transfusion Services and Operation of Blood Bank, Stockholm, Sweden
1994 : A course in Management and Situation Leadership, Dar es Salaam
1995 : Planning for HIV/AIDS in Developing Countries; University of East Anglia,
Norwich, U.K.

Work Experience
May 1969 – September 1969: Clerk at the Ministry of Education and Assistant to the
Deputy Principal Secretary, Education.
1976 – 1984 – Head of the Department of Diagnosis and the Department of Pathology,
Ministry of Health
1989 – 1991 – Specialist in Diagnosis and Head of the Department of Pathology,
Ministry of Health
Nov. 1991 – July 1995 – Programme Manager, AIDS Prevention Project, Ministry of
Health, and Advisor to the Ministry on Laboratory Services and Diagnosis.
29 October 1995 : Appointed by the President of Zanzibar to be Member of the House of
Representatives
12 November 1995 – Deputy Minister Ministry of Health
6 November 2000 – Member of the House of Representatives, Mkanyageni Constituency
22 November 2000 – Minister of State, President’s Office, Constitution and Good Governance

Political Career
1966 - Member of Afro Shiraz Party Youth League- A.S.P.Y.L.
Jan. – Dec. 1969 – Publicity Secretary, A.S.P.Y.L., Lumumba College
1968 – A.S.P.Y.L. Secretary, Zanzibar Secondary School.
1969 – Member of the Afro Shiraz Party
13 June 1977 to date – Member of Chama.Cha.Mapinduzi.(CCM)
2 September 1977 – Member of the National Executive Committee of C.C.M., Pemba
South Region.
27 September 1997 – Member of The National Executive Committee of Chama Cha Mapinduzi

Organisations and Committees

1990 – 1994 - Member of WHO Committee of Experts, Africa Region.
1990 – 1995 – Member of the Academic Council of the Muhimbili University College of
Health Sciences
1990 – 1995 – Member of the Advisory Committee of the Tanzania Commission for
Science and Technology
1990 – 1995 – Secretary to the Research Council, Ministry of Health
1989 – 1995 – Member of several committees in the Ministry of Health and others in
Zanzibar

Membership in Professional Associations
1985 – 1995 – Member of the Association of Clinical Biochemists of U.K.
1992 to present – Member of the Association of Clinical Pathologists for Eastern,
Southern and Central Africa(APESCA).
1992 – 1995 – member of the Association of Clinical Pathologists of Tanzania
1987 – 1992 – Member of International Association of Inborn Errors of Metabolism

Research Articles in Journals and Presentations at Various Fora

Short Communication/Posters - Total 29
Full Papers - Total 3
Thesis - Total 2; M.Sc.and Ph.D.

Participation in Meetings and Seminars
Participated and presented papers in 12 foreign countries
Appointed to be reporter at various international seminars
Zanzibar Government Delegations to the World Health Assembly Geneva 1997 and 1999; and to the Family Planning Project in Indonesia in 1997.
Has presented papers and chaired many meetings and seminars in Tanzania

Countries Visited
1969 to present – Has toured 19 countries in Europe, Asia and Africa

Hobbies
Athletics, football, reading books and newspapers.
 
Leo kuna habari inaeleza kuwa Ris Jakaya amekuwa anamtenga Shein na kumpendelea Pinda kwa nia ya kumwandaa kuwa Rais wa 2015. Nini maoni yenu kuhusu hili? Mimi naona hii habari kama yakichochezi hivi na ina nia ya kuchonganisha Wazanzibari na Wabara.
 
Uzushi huo tena MOD ikiwezekana funga thread hii.

Kwanini unataka ifutwe? I am copying the news for you!

Tangu ateuliwe kushika wadhifa wa Uwaziri Mkuu takriban miezi mitatu iluiyopita, Mizengo Pinda amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika shughuli za nje ya nchi mara tatu. Kwa wastani amefanya hivyo mara moja kila mwezi.

Katikati ya mwezi wa nne (tarehe 17 Aprili) Waziri Mkuu Pinda alimwakilisha Rais mjini Nairobi wakati wa kuapishwa kwa baraza jipya la mawaziri wa serikali shirikishi iliyoundwa.

Mapema mwezi huu Pinda alimwakilisha Rais huko Maputo, Mozambique, kwenye mkutano wa Nane wa Muungano wa maendeleo ya Elimu barani Afrika (ADEA). Na mapema wiki hii Pinda alimwakilisha Rais katika mkutano wa siku tatu wa Jukwaa la Uchumi wa Dunia (World Economic Forum) kuhusu Mashariki ya Kati.

Tusisahau pia kwamba wakati Kikwete akiwa ziarani huko China, ni Pinda, na siyo Dr Shein, aliyemwakilisha katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Iringa. Aidha, kinyume na ilivyotarajiwa, Dr Shein hakuiwakilisha Tanzania katika mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi za SADC ulifanyika Lusaka ulioitiswa na Rais Levy Mwanawasa wa Zambia. Dr Shein alibakia nchini kusimamia mapokezi ya mwenge wa Olympic.

Madhumuni ya makala hii ni kuchambua, pamoja na mambo mengine, uamuzi wa Rais, kiuhalali, kiutaratibu, kisheria, au hata kikatiba wa kupendelea kumchagua Waziri Mkuu wake, na si Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein kumwakilisha katika shughuli za nje, na iwapo pia ziko sababu nyingine za kufanya hivyo mbali na masuala niliyotaja.

Ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano haimpi makamu wa rais haina majukumu makubwa kama vile yale ya Waziri Mkuu ambaye ndiyo kiongozi mkuu wa shughuli za serikali, lakini ndiye mwenye madaraka makubwa, kingazi, au kicheo kuliko Waziri Mkuu.

Na hi inatokana na uhalali wake kidemokrasia -- katika ngazi hiyo kwani amechaguliwa na wananchi. Katika uchaguzi mkuu, Makamu wa Rais alikuwa katika karatasi moja ya kupigia kura (ballot paper) na mgombea wa urais.

Na ndiyo maana anapoondoka rais nchini, kikatiba madaraka yanamuangukia Makamu wa Rais, na si Waziri Mkuu, ambaye anakuja katika ngazi ya tatu. Hali kadhalika, katiba iko wazi kabisa kwamba iwapo lolote litatokea kwa Rais na kumfanya asiweze tena kuendelea na wadhifa wake – kama vile kuondolewa madarakani kisheria, maradhi au kifo, basi mara moja Makamu wa Rais anaapishwa kuwa rais na kumalizia kipindi cha urais kilichobakia – na si Waziri Mkuu.

Kwa maneno mengine, katika muhula wote wa utawala wa Rais husika, Makamu wa Rais ni kama “Rais mtarajiwa” – kwa lolote linaloweza kutokea kwa Rais. Suali ni kwamba katika kulizingatia hili, kwa nini Makamu wa Rais wa sasa, Dk Ali Mohammed Shein, anaonekana kuwekwa pembeni na Waziri Mkuu ndiyo anaonekana kuwa ndiye mwakilishi zaidi wa Rais hasa katika masuala ya kimahusiano ya kitaifa?

Ni suali gumu katika kupata jibu kiurahisi lakini pengine ni vyema tukaanzia namna Dr Shein alivyokuja kuwa Makamu wa Rais chini ya awamu hii ya Rais Kikwete.

Ikumbukwe kwamba Dr Shein aliteuliwa tu na Rais wa awamu iliyopita, Benjamin Mkapa kushika wadhifa wa Umakamu wa Rais mwanzoni tu mwa muhula wake wa pili, mwaka 2001, baada ya kufariki kwa aliyekuwa anashika wadhifa huo, Dr Omar Ali Juma.

Nasema Dr Shein aliteuliwa na Rais, hakuchaguliwa na wananchi kama ilivyokuwa kwa marehemu Dr Omar Ali Juma katika uchaguzi wa mwaka 1995, au kwa Dr Shein mwenyewe mwaka 2005. Kulikuwa fununu, wakati wa kinyang’nyiro katika chama chama tawala – CCM – cha uteuzi wa wagombea wa urais mwaka 2005 kwamba Dr Shein hakuwa chaguo la Kikwete kama mgombea wake mwenza, alishinikizwa tu na Kamati Kuu ya chama hicho chini ya mwenyekiti wake, aliyekuwa Rais wakati huo, Benjamin Mkapa.

Inasadikiwa kwamba baada ya Mkapa kushindwa kumpitisha “mtu wake” katika kugombea wa urais (kwani Kikwete hakuwa chagua lake) aliona ni bora akakishinikiza chama kumrejesha tena “mtu wake” – Dr Shein katika nafasi ya umakamu wa Rais.

Hapo Kikwete alizidiwa kidogo kete kwani Dr Shein kamwe hakuwa mmojawapo wa “wanamtandao” wake. Inasadikiwa alikuwa anamtaka Zakia Meghji kuwa mgombea mwenza wake.

Na tumekwisha kushuhudia katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili ya awamu ya Kikwete, mitikiso yote iliyotokea – hasa katika masuala ya tuhuma za ufisadi, Dr Shein hajaguswa kamwe. Ni hakika hakuwa “mwanamtandao”. Na hapa sisemi kwamba “mtandao” wote ni wa kifisadi, la hasha, lakini ni dhahiri kuona hali halisi.

Hata hivyo katika nchi nyingi zenye mfumo wa kuwapo nafasi ya makamu wa rais – nafasi hiyo huwa haina majukum makubwa sana, na mara nyingi huwapo katika kutimiza matashi tu ya kisiasa, kama vile kwa lengo la kuridhia pande fulani.

Hapa Tanzania tuliwahi kuwa na makamu wa rais wawili. Misri haina makamu wa rais kwa muda mrefu tu sasa, na sababu kubwa, inadaiwa, ni kwamba kuna mtu maalum anaandaliwa kumrithi Rais Hosni Mubaraka akimaliza kipindi chake hiki ifikapo mwaka 2011. Na huyo si mwingine bali ni mwanaye – Gamal Mubarak.

Kutokana na mfumo mpya wa serikali nchini Kenya uliyotokana na serikali shirikishi, makamu wa Rais Kalonzo Musyoka sasa amejikuta hana kazi, hasa baada ya kuanzishwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Ni Marekani tu ambako Makamu wa Rais (ambaye namna ya kuchaguliwa wake ndiyo tunaoutumia hapa) ana kazi kubwa aliyopewa kikatiba. Yeye, pamoja na majukumu mengine, ni mwenyekiti wa vikao vya Bunge kuu la nchi hiyo – Senate.

Na tukirudi hapa kwetu, huenda pia uamuzi wa Kikwete kumpendelea zaidi Waziri Mkuu Pinda, na siyo Makamu wa Rais Dr Shein, amwakilishe katika masuala ya kimataifa katika nchi za nje unatokana na suala la “utayarishwaji” wa Pinda huko mbeleni.

Kama alivyo Dr Shein, Pinda hana doa lolote kuhusu tuhuma za ufisadi, lakini anamzidi Shein kwa sababu ni mtu wa kutoka Tanzania Bara.

Inasadikiwa pia kwamba Kikwete kadhamiria kumkabidhi Pinda kuyashughulikia masuala yote ya kuhusu vita dhidi ya ufisadi, na tayari tumeanza kuona kuwa yeye ndiye mzungumzaji mkuu wa serikali kuhusu masuala hayo. Na bila shaka hii pia inatokana na yeye kukubalika zaidi kwa wafadhili.

Hakuna haja ya kusema kuwa kuna masuala ya msingi yanayomfanya Kikwete asizungumzie ufisadi – na kubwa hapa ni kwamba kuna baadhi ya maswahiba wake wakuu aliyowaamini wameanguka kutokana na tuhuma za ufisadi.
 
yakhe umeipaste ila ina ukweli ati,kumbe muungwana alikuwa amtaka ma mkwe awe makamu wake,yakhe si ingekuwa balaa ati
 
Sheni hauwezi Uraisi na yeye mwenyewe anajua ila hapo alipo anaweza kubakia hata miaka mia hana makuu , mwenyewe na mikasi yake yaani mambo ya ndani tu si mtu wa misafara halafu jamaa ana wivu kibao si mnamwona ?Anaweza akakuchoma mkasi.
 
Leo kuna habari inaeleza kuwa Ris Jakaya amekuwa anamtenga Shein na kumpendelea Pinda kwa nia ya kumwandaa kuwa Rais wa 2015. Nini maoni yenu kuhusu hili? Mimi naona hii habari kama yakichochezi hivi na ina nia ya kuchonganisha Wazanzibari na Wabara.

Mkuu Job, natanguliza heshma. Mkuu,hii ni tetesi tena ya kutungwa na haina maslahi ya taifa, inaonyesha kujaa chuki binafsi hivyo sioni umuhimu wa kuijadili tena katika kipindi hiki cha hoja nyingi nzito zenye manufaa kwa taifa kama vile ufisadi na kifo cha Balali.
 
Mwacheni Pinda naye apate exposure!! Kuhusu kuwa anaandaliwa, duh! ina maana JK inampango wa kukaa mpaka 2010!! Mungu naomba utuepushe na hili!!!!!!
 
unajua saa nyingine napenda watu wakienda deep kuconsider vitu ambavyo we dont know whats going on around that cycle (shein,jk) anyway tuwaache watu watufurahishe !

Huu ni ukweli. Nimetafakari sana kuhusu hili na kugundua kitu muhimu sana. Nchi zinazofuata mfumo wa "Presidential" kama Marekani, Naibu Rais/Makamu ana nguvu sana. Tatizo letu ni kuwa tumechanganya Parliamentary system na presidential. Katika mfumo huu, Rais anakuwa mtendaji na ana nguvu sana lakini Makamu wake anakuwa ni symbolic na pengine yuko kama reserve ili kusiwe na power vacuum in case akisafiri, kuugua au vinginevyo. Waziri Mkuu anabaki kuwa mtu wa jikoni zaidi maana ni msimamizi wa kazi za kila siku za serikali na ni kama kiranja wa mawaziri wote. Kwa sababu hiyo naona siyo haki kusema kuwa JK anampendelea Mizengo at the expense of Shein. Ukweli ni kuwa ukimwondoa Sumaye ambaye alikuw ayes man zaidi, mawaziri Wakuu karibu wote waliopita walikuwa powerful. Ukianza na Sokoine, Salim, Waryoba, Malecela na hata Lowassa.
 
Hii ishu jamani mbona inakaundani hivi ndani yake ni wazi Shein urais hauwezi na kama mnavyo ona umakamu wenyewe ukiangalia kiundani kama analazimishwa hivi..ngoja tusubili tuone jaribuni kufikiri jamani...
 
mimi naona kama waziri mkuu anaweza kutetea hoja za serikali kama inavyotakia na ni mtu anayefuatilia kila kitu na yuko makini siyo wa kwenda na kusoma maneno yalioandikwa na watu basi apewe nafasi ya kuonyesha jinsi inchi yetu inavyoweza kujiendesha kupitia watu wake...wenyewe mmeona aliyoyafanya Misri yani anamuakilisha raisi mpaka kila mtu anakubali
I suggest aendelee kupewa nafasi nyingi zaidi ya hapo.....that Guy z very Smart
 
kama ni kweli jk anafanya hayo uliyokwisha yandika na munga mkono kwani shein he just one of these useless katika wakubwa hapa Tanzania anaonekana ni mtu wa kusukumwa sukumwa kama tangi
 
Makamu wa Rais ni cheo cha kuwaridhisha wapemba kwamba nao ni watu.Zaidi ya hapo ni kama mtu asiye na kazi maalum,amekaa kwa ushawishi na manufaa ya kisiasa.

Jimbo analotoka halina mbunge wala diwani wa CCM.Kuchaguliwa kwake ni kubebwa na JK na CCM ili matakwa ya kisiasa yaweze kufikiwa kwa kisiwa cha Pemba.

Mwiba wa Pemba bado uko kooni kwani Shein haheshimiki kwao anaonekana kama msaliti wa jamii ya watu wa Pemba.

Kwa kuwa amewekwa hapo kama kigezo cha CCM kujali wapemba,kazi anazozifanya hazina hadhi inayoendana na cheo hicho.Kwa hiyo hathaminiki kwao kwa sababu hata akigombea udiwani hataupata,na hana thamni kitaofa kwa sababu madhumuni ya kuwepo kwake yana lengo maalum.
Ndiyo sababu alipofariki Omar Ali Juma ilibidi atafutwe mpemba mwingine ili kuendeleza tashwishi za kisiasa.
Kwa hiyo yupo kama sanamu tu.
 
Leo kuna habari inaeleza kuwa Ris Jakaya amekuwa anamtenga Shein na kumpendelea Pinda kwa nia ya kumwandaa kuwa Rais wa 2015. Nini maoni yenu kuhusu hili? Mimi naona hii habari kama yakichochezi hivi na ina nia ya kuchonganisha Wazanzibari na Wabara.


..ni hisia tu ..hakuna uwezekano wowote wa mizengo kayanza peter pinda kuja kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania...nafasi ya uwaziri mkuu is the peak of his perfomance ...hata awe mzuri vipi...pia hata huyu pinda hakuwa mtandawo..huyu alikuwa akipigiwa chapuo na mzee mkapa na watu wa usalama tangu hiyo 2005
 
Hii habari kama noi kweli au uongo hilo mimi silioni la msingi - The guy deserve it - Waswahili wanasema abembwae hujikaza lakini Shein yeye yupo tu, anaona zari limemuangukia basi ndio hivyo. Kama kweli Muungwana anamtenga au ameshajua uwezo wale basi ni sawa tu.

Mwenzake marehemu Dk. Omar hakuwa hivyo na yeyote alomjua alijua kuwa anaweza kushika madaraka ya nchi ikiwa lolote lingetokea kwa Mkapa, lakini Shein hata hiyo mikasi nafikiri hajui upi ni upi ni lazima achaguliwe licha ya uzoefu alonao katika nyanda hiyo.
 
Makamu wa Rais ni cheo cha kuwaridhisha wapemba kwamba nao ni watu.Zaidi ya hapo ni kama mtu asiye na kazi maalum,amekaa kwa ushawishi na manufaa ya kisiasa.Jimbo analotoka halina mbunge wala diwani wa CCM.Kuchaguliwa kwake ni kubebwa na JK na CCM ili matakwa ya kisiasa yaweze kufikiwa kwa kisiwa cha Pemba

Kuna haja gani ya wapemba kulalama kwa kupewa nafasi chache za wawakilishi?,ikiwa mpemba(shein) kapewa nafasi tena ya juu sana,lakini wanaibeza?,wakati wanapashwa kumpa pongezi JK,na kudai nafasi nyinginezo nyingi zaidi.Kuwe au kusiwe na CCM pemba,sikigezo cha kutoachaguliwa mtu wa huko kuwa kiongozi.

Mwiba wa Pemba bado uko kooni kwani Shein haheshimiki kwao anaonekana kama msaliti wa jamii ya watu wa Pemba.

Wasaliti ni ninyi mnaotaka kujitenga,then mujiunge na mtandao wa kiarabu.
Watu wengine bwana,wamesahau ushenzi aloufanya mwarabu ndani ya nchi yetu wakati wa ukoloni,lakini bado yanampigia magoti.

Kwa kuwa amewekwa hapo kama kigezo cha CCM kujali wapemba,kazi anazozifanya hazina hadhi inayoendana na cheo hicho.

Aliwekwa hapa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania,hakuna cha kuwaridhisha wapemba,kwani ninyi wapemba ni akina nani hasa ndani ya Tanzania?

Kwa hiyo hathaminiki kwao kwa sababu hata akigombea udiwani hataupata,na hana thamni kitaofa kwa sababu madhumuni ya kuwepo kwake yana lengo maalum.

Agombee udiwani wa nini hasa?kesha kuwa makamu wa rais,udiwani wa nini?mukae na mujue Pemba ni sawa na kijiWilaya tuu cha hapa Tz,sioni mantiki ya makamu wa rais kugombea hata ubunge huko kwenu.

Ndiyo sababu alipofariki Omar Ali Juma ilibidi atafutwe mpemba mwingine ili kuendeleza tashwishi za kisiasa.

Sifa zake + kutopenda agenda zenu wapenda hasa za kubaguana,ndio kigezo pekee kilichomuweka hapa,aliko.

Kwa hiyo yupo kama sanamu tu.

Hata kidogo huyu Mh. si sanamu ndani ya nchi ya Tanzania na dunia nzima.Ninyi ndie mtabakia kuwa masanamu ndani ya nchi ya Tanzania + Dunia nzima,mkiendelea na siasa zenu za kujitenga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom