LazaroSMtindi
Senior Member
- May 6, 2008
- 100
- 5
Washikaji nawaomba mjue kupambanua kati ya pumba na mchele! Watu wasimzulie JK majambo kwa sababu zao finyu za kisiasa. Anambaguaje Shein? Tunaomjua Shein tunasema, Shein si mtu wa jukwaa, si msemaji. Kama ni kutoonekana kwake, basi ni kutokana na tabia yake mwenyewe ya kukaa nyumanyuma. Msimsingizie JK wala Pinda kwa hili. Kama ni urais wa 2015, nani aliwaambia Shein anafaa? LazarosLeo kuna habari inaeleza kuwa Ris Jakaya amekuwa anamtenga Shein na kumpendelea Pinda kwa nia ya kumwandaa kuwa Rais wa 2015. Nini maoni yenu kuhusu hili? Mimi naona hii habari kama yakichochezi hivi na ina nia ya kuchonganisha Wazanzibari na Wabara.