Dr. Shein amesusia vikao vya cabinet, je wabunge wa Znz nao watasusia bunge la muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Shein amesusia vikao vya cabinet, je wabunge wa Znz nao watasusia bunge la muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Mar 21, 2011.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,782
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  ..Raisi wa Znz, Dr.Shein, amesusa kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri wa serikali ya muungano.

  ..je, huyu anatunisha misuli kwamba Zanzibar hawataki muungano?

  ..je, wabunge wa Zanzibar kwenye bunge la muungano nao watamuunga mkono Raisi wao?

  ..au, kwanini wabunge wa Zanzibar hawajafuata msimamo wa Raisi wa Zanzibar kususia masuala ya muungano?

  ..hivi Makamu wa Raisi, Dr.Bilali, mawaziri toka Zanzibar, na wabunge wao, wakipanda speed boat na kurudi Zanzibar wakisusia shughuli za muungano, what will happen?
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  nini tena mkuu?
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Baba huyu ni kati ya watu wachache sana nchini ambao si lazima wadai heshma kwangu maana siku zote ni mtu mstaaabu sana, mkweli kupindukia, mkali zaidi ya pilipili kichaa, mwadilifu sawa ya Mwalimu Nyerere na Muona mbali zaidi ya mnyama twiga katika siasa za nchi yetu.

  Ukisema kwamba kweli huyu baba HAKUONEKANA TENA KWA 'KUSUSIA' vikao vya baraza la mawaziri chini ya Mhe Kikwete sambamba na Mhe John Pombe Maghufuli basi ujue kwamba hata miongoni mwa wale waliohudhuria zaidi ya nusu wala hali si shwari mle!!!

  Kama kweli ilitokea hivyo basi hilo, kwangu mimi naliona kuwa ni zaidi ya ajali ya kinu cha Nyuklia kule nchini Japana na huenda kishindo chake na mionzi ikafika mbali kuliko kawaida. Laiti ingalukua ni Komando Salmin, Karume au hata Maalim Seif wala nisingegutuka kitu hapa.

  Umesema Dr Shein ... Endapo ni kweli na basi ujue fukuto ndani ya siasa za Muungano ziko pabaya kuliko kawaida hivo.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,782
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  Uwezo Tunao,

  ..Shein anapaswa kula kiapo kabla ya kuhudhuria vikao vya cabinet. je, umeona akifanya hivyo?

  ..anatakiwa aje Ikulu DSM na aapishwe na Jaji Mkuu kuwa waziri asiye na wizara maalum wa serikali ya muungano.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Imekuwa kawaida sasa kwa Rais wa Zenj kutohudhuria vikao vya kabineti...
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  E bwaana we ...!!! Duh!!
   
 7. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Source plz:washing:
   
 8. P

  Pumba Mwiko Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa source plz!!
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Source ni Kibunango
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Source ya nini wakati hakuwepo kweli? Au mlitaka rais wenu hawatangazie kuwa Dr hayupo? la msingi ni kujua muungano ni tatizo.............................
   
 11. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama anahitaji kula kiapo, ni sababu zipi zinamfanya asile mpaka leo?
   
 12. K

  King kingo JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naona wamegundua hivyo vikao havina Tija kwao blah blah zimekuwa nyingi....
   
 13. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Hana njaa!
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Mimi naona amefanya jambo la maana kama ni kweli amefanya hivyo.Kama amesusia kuja kwenye vikao kama waziri asiye na wizara maalum. Hiki ndio cheo alichopewa rais wa Zanzibar kwa sasa katika Muungano au vipi?

  Pia sioni mantiki ya wabunge wa bunge la Muungano kutoka Zanzibar kususia au kupanda boti na kurudi Zanzibar.

  Nafikiri ni vizuri wawepo katika bunge la Muungano ili ikija hoja ya muungano au yale yanayowagusa wao kama Wazanzibari wayasemee au wayatetee.

  Nilifikiri wewe JokaKuu utamuunga mkono Dr. Shein katika hili kwa sababu anasaidia katika kuleta mjadala wa wazi wa Muungano au hatutaki mjadala wa muungano? Au hatutaki Tanganyika?

  Umeileta mada yako leo kwa ushabiki zaidi kulikoni kuangalia uzuri na athari ya anachofanya Dr. Shein.

  Mkuu, Headquarters za AU ziko Addis, za EAC zipo Arusha,Leo headquarters za Muungano wa TZ zipo Dar na Dodoma. Na bado Muungano haujavunjwa rasmi ingawaje unaonekana haupo tena.

  Hata wazanzibari wote wasusie hivyo vikao vya bunge na watangaze hawautaki tena muungano kwa Tamko la upande mmoja, Kikwete ataamuru JWTZ waishikilie Zanzibar.

  Nionavyo ni vyema tuwatie moyo Wazanzibari wakaze kamba ili mjadala wa muungano na katiba mpya uwe wa uwazi ili utengano au ushirikiano uwe wa tija na wa maana kwa pande zote. Sasa hivi kila kitu kimegubikwa na usiri na ubabe na ujanja ujanja. Jambo ambalo linaleta manung'uniko kutoka "bara"(Tanganyika) na pia Zanzibar.
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  100% huyu jamaa siku ukisikia kahamia chadema wala usishangae maana ukipenda haki utaona kinyaa sana kuwa karibu na kina Makamba na mkwere
   
 16. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Muungano wetu huu ipo siku utakuwa Mtengano. CCM hawataki ujadiliwe kwa nini jamani? Japo sijafanya utafiti lakini naamini Watanzania wanataka ujadiliwe na kufanyiwa marekebisho kwa maslahi na ustawi wa pande zote za muungano. Haya mambo ya kuficha hata hilo lihati au limkataba la muungano yataupeleka muungano kaburini ungali hai japo mahututi.
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hana lolote huyo mzee wa mikasi si alikuwa Magogoni kwa miongo kadhaa ni nini kipya atafanya kama sio kuangalia tumbo lake?
   
 18. K

  Kiguu na njia Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  du! Mzee yupi huyo?
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jee upo ulazima wa yeye kuhudhuria iwapo ajenda ni bomoa bomoa inayofanyika Tanganyika?
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naona kwa hili ni droo kwani hata CHADEMA wana kigugumizi.
   
Loading...