Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ndio wanaingia sasa katika kikao na kwa sasa upepo wa Dk. Shein unaelekea kumng'aria ila kwa CCM lolote linaweza kutokea

MATOKEO:

Shein kura 117
Bilal kura 54
Nahoda kura 33

b669l3.jpg
 
Napigiwa simu na mtu wa karibu na RA anasema, "Hakuna tena wa kumzuia Bilal kama walivyomshindwa JK 2005, tayari anasubiri kupitishwa kuwa mgombea wa CCM Zanzibar"
 
mkuu katika muda usiofikia saa moja mambo yameshageuka? Anyway, pamoja na ubaya, udhaifu na upungufu wa CUF bado wanaweza kuiengua CCM Zenji.
 
Napigiwa simu na mtu wa karibu na RA anasema, "Hakuna tena wa kumzuia Bilal kama walivyomshindwa JK 2005, tayari anasubiri kupitishwa kuwa mgombea wa CCM Zanzibar"
RA mpaka Zenji napo.....mbona tutakwisha! JK hapa lazima atumie mbinu ya Nyerere tu! wakimpa Bilali tu wamekwisha!
 
RA mpaka Zenji napo.....mbona tutakwisha! JK hapa lazima atumie mbinu ya Nyerere tu! wakimpa Bilali tu wamekwisha!

Kule kuna wese la kumwaga ndo maana watu wamerusha kete kwa mtu wa Ndio baba.
Sielewi jamaa akipita maeneo kama ya Mchamba wima, Kibanda Maiti atayaboresha au kutabaki magofu tu.
 
Kule kuna wese la kumwaga ndo maana watu wamerusha kete kwa mtu wa Ndio baba.
Sielewi jamaa akipita maeneo kama ya Mchamba wima, Kibanda Maiti atayaboresha au kutabaki magofu tu.
Mwaka huu Bilali akitoswa tena lazima awafanyie kitumbaya jamaa....
 
Kuna mambo ambayo kwa kweli yanatisha, nchi yetu kwa kweli imekua ikiendeshwa KIMAFIA.... bora sijaenda Dodoma nimejichimbia huku mbali
 
Kama wenye chama hawataki atawafanya nini? Sana sana wanaweza kuchimba madhambi amba"yo anadhani kwamba hawayajui lakini huwa yanatumika pale panapohitajika "zana nzito"
 
ole wenu ccm mmpe bilal kumbukeni huyu akiwa waziri kiongozi serikai ya zanzibar ilishindwa kulipa mishahara ya watumishi wake
 
zisi is vere interestingi:

There are currently 43 users browsing this thread. (17 members and 26 guests)

Obuntu,Muzii,Awo,Akili Unazo!,Kiazi Kikuu,Halisi,jethro,Chiluba,kichenchele,KGM,SMU,Kaitaba,Mathias,Nyuki,Who Cares?,Kyachakiche,Chimunguru,
 
Jamani leo watu hata lunch tunataka kusahau sababu ya kusubiri........
 
Haya mapambano ya Madokta wa Zanzibar mmoja wa physics [Bilal] na wa pili wa Biochemistry[Shein] yanafurahisha. Kati yao hakuna hata mmoja aliyesomea political science - sasa tutaona mapya huko Visiwani mmoja wao akipitishwa na kushinda kura hapo October 2010. Utawala wa kisayansi unaingia huko visiwani. Wote wawili wamekulia na kufanya kazi bara kwa hiyo sidhani kama Muungano utaathirika mmoja wao akipata.
 
Jamani leo watu hata lunch tunataka kusahau sababu ya kusubiri........

Teh Teh Teh Teh Mkuu inabidi wategemea kweli kuna kula kweli leo maana twangojea kwa hamu sana kujua ni Kiongozi yupi atatukwamua huko Zenji.

Kweli twahitaji kiongozi shupavu mwenye busara hekima na msikivu kwa wanchi wa Zenji na Bara pia twahitaji mabadiliko na maendeleo sasa nadhani katika vuguvugu hili CCM wanapaswa kujipanga vyema kuboresha Chama nadhani mambo yako wazi nyakati hizi, watu wasikimbilie Uongozi bora uongozi twahitaji viongozi wawajibikaji

Tupeni Detailz pindi mpatapo kutoka DOM.

Eeeeh kwli nimesikia Ati Mr.Sitta Ameiuliza serikali ya CCM kama inadhamira ya kuhamia DOM na anashangazwa kuwa serikali yaendelea jenga nyumba za Mawaziri Dar?

Kwanini Hili laendelea CCM wanashindwa timiza sera hiyo toka 1980's kweli ?????? hiii napenda iende kwa vijana kama wakina January Makamba wanao sema wanakuja na chachu na kutaka kurekebisha MUSTAKABALI WA NCHI HII

 
Back
Top Bottom