Dr. Shein aenda Uingereza kwa ziara Maalum. Swali, kaenda kama nani?

Dr. Shein ni RAIS wa Zanzibar. Kwa huu ujinga wenu wa kukataa kuitambua Zanzibar ni nchi katika muungano ndio moja ya sabau ya zanzibar kutaka kujitenga. Zanzibar ni nchi kama katiba ya Zanzibar inavosema. Na karibuni pia muungano utavunjika kwa kuwa wazanzibari hawautaki muungano feki anymore.
Kama ni hivyo basi wajinga tuko wengi...

  • Duniani kuna nchi 196 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo.
  • U.N. kuna nchi 193 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo.
  • Afrika kuna nchi 54 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo.
Sasa hii nchi ya kufikirika inayoitwa Zanzibar iko bara gani, dunia gani na sayari gani au iko tu kichwani mwa watu kama Falconer. Ni kweli yako maeneo na koloni nyingi tu zisizotambulika kama nchi kama Palestina, Puerto Rico, Scotland na hata England lakini hata huko Zanzibar si mojawapo. Ni kweli Tanzania inaweza kupasuka kama Sudan na nchi mpya ikazaliwa na kuitwa Zanzibar lakini mpaka hilo litokee hakuna, narudia, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar ila kuna sehemu tu ya Tanzania inayojulikana kama Zanzibar. Udhaifu, uzembe na ubabaishaji wa viongozi wa Tanzania ndio unaoupa mwanya uhuni kwa watu kujitangazia uhuru bandia na kujiita nchi...nchi iko moja tu, Tanzania.
 
hivi madokta wa Zanzibar nao wamegoma?
Au wenzetu huko mkiugua mnapeleka mahakamani Nazi Mdondo, Jogoo Mwekundu, Nyungu, chumvi ya mawe, ubani maka, mafuta ya mnyonyo na ushuzi kama huo?
 
Kama ni hivyo basi wajinga tuko wengi...

  • Duniani kuna nchi 196 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo.
  • U.N. kuna nchi 193 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo.
  • Afrika kuna nchi 54 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo.
Sasa hii nchi ya kufikirika inayoitwa Zanzibar iko bara gani, dunia gani na sayari gani au iko tu kichwani mwa watu kama Falconer. Ni kweli yako maeneo na koloni nyingi tu zisizotambulika kama nchi kama Palestina, Puerto Rico, Scotland na hata England lakini hata huko Zanzibar si mojawapo. Ni kweli Tanzania inaweza kupasuka kama Sudan na nchi mpya ikazaliwa na kuitwa Zanzibar lakini mpaka hilo litokee hakuna, narudia, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar ila kuna sehemu tu ya Tanzania inayojulikana kama Zanzibar. Udhaifu, uzembe na ubabaishaji wa viongozi wa Tanzania ndio unaoupa mwanya uhuni kwa watu kujitangazia uhuru bandia na kujiita nchi...nchi iko moja tu, Tanzania.

Umekasirika angalia usijeshindwa kula..

Zanzibar ni nchi, itabaki kuwa nchi, japo ni ngumu kumeza..
 
Waswahili bwana, sasa hapa nikasirikie nini? Katika orodha ya Maraisi wa nchi 193 zinazotambulika na Umoja wa Mtaifa (U.N), Dr. Shein hayupo.

Katika orodha ya Maraisi wa nchi 7 zisizotambulika na Umoja wa Mataifa (U.N.) lakini angalau zinatambuliwa na nchi mojawapo mwanachama wa U.N., Dr. Shein hayupo. Nchi hizo ni pamoja na Raisi wake ni;

  1. Abhkazia - Raisi Alexander Ankvab
  2. Kosovo - Raisi Atifete Jahjaga
  3. Cyprus Kaskazini - Raisi Derviş Eroğlu
  4. Palestina - Maraisi Mahmoud Abbas (West Bank) au Aziz Duwaik (Gaza Strip)
  5. China (Taiwan) -Raisi Ma Ying-jeou
  6. Sahrawi Arab Democratic Republic - Raisi MOhamed Abdulaziz
  7. Ossetia Kusini - Raisi Leonid Tibilov
Katika orodha ya Maraisi wa nchi 4 zisizotambuliwa na nchi yoyote mwanachama wa U.N, Dr. Shein hayupo. Nchi hizo ni;

  1. Azawad
  2. Nagorno-Karaback
  3. Somaliland
  4. Transnitria
Kama mnavyoona wana jamvi, hakuna popote inapotajwa Zanzibar kama nchi/taifa wala anapotajwa Dr. Shein kama Raisi wa nchi yoyote ile. Ningekuwa Dr. Shein katu nisingekubali huu upuuzi wa kuvikwa kilemba cha ukoka eti Raisi...Raisi huwezi hata kutia mguu kikao chochote rasmi cha maraisi duniani. Huo ndio ukweli ingawa mchungu kuumeza.
 
Huko kutambulika kwenye hizo organs ni irrelevant kwasasa..maana Tanganyika(a.k.a Tanzania wanalipia hizo related costs

Anatambulika na wananchi wa zanzibar na ndio anaowatumikia kama rais wao..kwa kutumia katiba yao, bendera yao, wimbo wa taifa..

Muhimu zaidi tumesajili meli 300 tunaendelea kusajili kwa faida ya nchi yetu na wananchi wetu

Mungu ibaraki Zanzibar na Mungu mbariki Rais wetu Dr. Shein
 
kwa kutumia katiba yao, bendera yao, wimbo wa taifa..
Eti bendera yao...ha ha ha haaa! Mbona hawathubutu kuitundika kwenye hizo meli? Huo ugangari wao utaishia jikoni tu na labda sebuleni.

Muhimu zaidi tumesajili meli 300 tunaendelea kusajili kwa faida ya nchi yetu na wananchi wetu
Ahaa, finally Topical...mmesajili meli 300, case closed? Unaota mchana kijana.

Mungu ibaraki Zanzibar na Mungu mbariki Rais wetu Dr. Shein
Ningekuwa wewe ningesema Allah ihurumie Zanzibar.
 
Eti bendera yao...ha ha ha haaa! Mbona hawathubutu kuitundika kwenye hizo meli? Huo ugangari wao utaishia jikoni tu na labda sebuleni.

Ahaa, finally Topical...mmesajili meli 300, case closed? Unaota mchana kijana.

Ningekuwa wewe ningesema Allah ihurumie Zanzibar.

Kutumia bendera siyo issue je meli zimesajiliwa? ndiyo ngapi zaidi ya 300 na tunaendelea kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ya Zanzibar.. kama mna ubavu wa kuja kunyan'anyi bendera tunasubiri kwa hamu..

Allah Ibariki Zanzibar, Allah wabariki wazanzibar na Rais wetu Dr. Shein
 
Roho zinawauma Watanganyika. Haa haaa haaa. Mtaiona hivyo hivyo ZNZ hioooooo. Mtabaki kutawaliwa na Mafisadi, mapapa na manyangumi. Mwishowe mtatupwa Mabwepande kama mizoga. Haa haa haaa. Amkeniiiiiii Daini Tanganyika yenu.
 
Back
Top Bottom