Dr. Shein aapishwa kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.

Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini Dodoma.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

02 Mei, 2016
 
Duhh ndio maana Maalim Seif alinyimwa Urais maana angekuwa akijua siri zao ......Mbona Komandoo na Karume hawakuwahi kuapishwa ? Rais wa ZNZ anatajwa kwenye Katiba kama mjumbe kwa urais wake wa ZNZ kama alivyo Makaumu wa Rais , Mbona Makamu hakuapishwa ? Huyu kala kiapo cha utii kwa rais wa Muungano so yeye ni sawa na Mawaziri? hadhi na heshima ya Urais wa ZNZ iko wapi?
 
Nchi hii!
 
Hapo kwenye kuchukua nafasi ya ujumbe wa baraza la mawaziri kutokana na cheo cha uraisi wa SMZ ndipo alipokuwa anaogopwa Maalim Seif.
Tumeona kumbe dili zote kubwa na mbovu za kitaifa zilikuwa engineered ndani ya baraza sasa ingekuwaje kama Maalim yupo humo?
 
Duhh ndio maana Maalim Seif alinyimwa Urais maana angekuwa akijua siri zao ......Mbona Komandoo na Karume hawakuwahi kuapishwa ? Rais wa ZNZ anatajwa kwenye Katiba kama mjumbe kwa urais wake wa ZNZ kama alivyo Makaumu wa Rais , Mbona Makamu hakuapishwa ? Huyu kala kiapo cha utii kwa rais wa Muungano so yeye ni sawa na Mawaziri? hadhi na heshima ya Urais wa ZNZ iko wapi?

Kiapo cha Utii kwa Rais huwa unaapishwa na Rais mwenyewe sio Jaji Mkuu na Dr.Shein kaapishwa na Jaji Mkuu, Rais wa Zanzibar akiingia kwny Cabinet bila ya kuapa atakuwa kaingia kwa mfumo upi kwa kuwa kwny kiapo cha Urais wa Zanzibar hakuna sehemu inayozungumzia ujumbe wake kwenye Cabinet ya Muungano?.
Rais wa kweli wa Zanzibar aliethubutu kupigania haki ya Zanzibar kwa vitendo ni Aboud Jumbe pekee aliefikia utayari wa kupoteza Urais wake Dodoma kuliko ku withdrwa mswaada wa kutaka serikali tatu January 1984 wengine wote magumashi tu kama kina Karume Jr wanakumbuka hilo wakishastaafu na Seif aliekumbuka alipofukuzwa chamani.
 
Hiyo ni mojwapo ya KERO za Muungano na pia ilikuwa sababu MUHIMU ya kumpoka Maalim Seif ushindi wake.
 
Kwanza , Kaapa ....Badala ya kutamka.....

Pili, ile mizinga 21 kwisha habari yake , ........
 
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwakawaida uapishwa na Mwenyekiyi wa Baraza hilo - Raisi. Jaji Mkuu anatokea wapi kwenye hili?
 
Mtajiuliza maswali Na kujijibu wenyewe Na mtaishia kuzungusha mikono , lkn haitazuia kitu jamaa ndo kaisha apishwa
 
Kwenye setup ya Muungano, Rais wa Zanzibar angalau ni waziri asiye na wizara maalum huku bara, lakini Waziri Mkuu wa JMT ni Waziri Mkuu wa JMT jina tuu, lakini kiukweli ni Waziri Mkuu wa Bara tuu, he is nobody in Zanzibar!.

Mbadiliko ya katiba ya JMT yaliyomuondoa rais wa Zanzibar kutokuwa makamo wa rais, ni mabadiliko batili, kinyume cha mkataba wa muungano!.

Ili kuudumisha huu muungano, lets go back to the basics, Zanzibar na Tanzania bara zika equal status zenye haki sawa kabisa, ila kiukweli mmoja amemkalia mwingine akimburuza!.

Tuitendee haki Zanzibar!.

Pasco
 
Shauri yao....inatia huruma.Cabinet yote ni wabunge kule Dom na hata Mh.Rais ni sehemu ya bunge...sasa vipi kuhusu Rais/Waziri Dr Shein atakuwa mbunge wa Dom pia....
 
Back
Top Bottom