Dr. Salim Ahmed Salim, Jaji Warioba Kuuguruma Kivukoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Salim Ahmed Salim, Jaji Warioba Kuuguruma Kivukoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mashikolomageni, Jul 29, 2011.

 1. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135


  Sasa hivi uzinduzi wa Sherehe ya miaka 50 umeshafanyika muda mchache iliopita na aliyezindua ni Dr. Salim na sasa sikinde wanatoa burudani! Tunategemea Jaji WArioba ambaye yuko hapa baadaye ataongoza Mdahalo mada inahusu MCHANGO WA CHUOCHA KUMBUKUMBU YA MWL. NYERERE KATIKA NCHI YA TANZANIA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Warioba anasema waasisi wa taifa letu walijua Umoja na Mshikamano wa wananchi ndiyo nguzo kubwa ya kuleta uhuru, baada ya uhuru walichukua hatua za kuimarisha,
  kuondoa mianya ya mgawaniko, kama Uchifu, umiliki wa ardhi, sheria za mila na mahakama zilibadilishwa Native court, serikali ilitenganishwa na dini, elimu ilitenganishwa na dini ilikuondoa nmatabaka baada ya kutaifisha mashule pia kiswahili kilifanywa lugha ya taifa
  .
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Maamuzi hayo yalifanywa yalikuwa MAAMUZI MAGUMU, lakini yalifanyika lengo likiwa kuimarisha umoja na mshikamano, Chuo hiki kilitumika kuunda viongozi kwa kuwafundisha itikadi namisingi ya uzalendo. Wakati huo uongozi ulikuwa ni kuonesha njia, na umuhimu wa kuwa na nidhamu. Anasema sasa hivi kuna mapungufu ya nidhamu mfano wananchi kuitwa kwenye mkotano na kiongozi kufika masaa 2 baada ya muda wa awali matokeo yake ni jamii nayo kufuata hiyo
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Anaongelea nidhamu ya BUNGENI, bunge ndiyo iliyokuwa imebaki mfano wa taasisi za nchi iliyo makini lakini sasa huwezi kulisema leo kama taasisi makini, lugha inayotumika, anasema ama wanapindisha kanuni au wanazikiuka.
  MAADILI, anazungumzakuwa viongozi wanazungumza sana juu ya RUSHWA nlakini kati yao nani anaweza kusimama mbele ya MUUMBA wake na kusema alipata uongozi bilan kutoa HONGO, ukweli ni kuwa utapata maelezo ya kwa nini alitoa hongo
  MUHIMU ni kuendelea kukataa hongo na kukemea RUSHWA na UFISADI
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kauli zinazotolewa na viongozi wa seikali zina mashaka kama kweli kuna uwajibikaji
  bunge limekuwa ni mkusanyiko wa watumishi wa vyama vya siasa badala kuwa taasisi ya kitaifa. Hoja nzuri inaweza kuzimwa kwa kutumia vibaya kanuni au misingi ya vyama. Wanachi wanayo haki ya kuangalia na kujifunza kwa wabunge sasa kama migawanyiko baina ya vyama na ndani ya vyama inawagawa wananchi na inahatarisha umoja wa nchi na amani. Kamati za bunge nazo anasema zimekuwa zina toa maagizo tofauti na ya serikali kwenye mashirika ya umma matokeomyake ni kuleta mgawanyiko
   
 6. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Khaa!!
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akihutubia jana jijini Dar es Salaam
  kwenye maadhimishoya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa
  Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kivukoni.
  Alisema kwamba Bunge ni kioo cha wananchi na katika kuimarisha demokrasia, wananchi wataongozwa kwa kuiga mfano wa wawakilishi wao na kwamba kama lugha ya wabunge imejaa kejeli na kubeza, wananchi nao wataiga.

  Aidha, alisema mgawanyo wa madaraka kati ya Serikali na Bunge umeanza kuonyesha mgongano na akasema wakati mwingine Bunge limeonekana kufanya kazi za Serikali.


  Alisema kwa mfano, kamati za Bunge kwa siku za hivi karibuni zimekuwa zikitoa maelekezo kwa watendaji wa serikali.


  “Taasisi za utendaji kama vile Polisi, Takukuru na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wanapewa maagizo ya utendaji bila mpangilio.
  Taasisi hizi zinatakiwa kufanya kazi kwa uhuru kwa kufauata taratibu zake. Lakini siku hizi ni jambo la kawaida kwa taasisi hizi kupewa maagizo kwa msukumo wa kisiasa na kwa sababu hiyo kazi inaweza ikafanywa kwa kulipua,” alisema Jaji Warioba. Jaji Warioba alisema mbali na kamati hizi za Bunge kwenda moja kwa moja kwenye taasisi za umma na kutoa maagizo kwa kivuli cha ushauri, pia zimeanza kwenda nje ya nchi kufanya kazi za kidiplomasia ambazo kwa kweli ni za seikali.


  Aidha, aliviasa vyombo vya habari kuachana na tabia ya kuandika habari za siasa hasa zinazohusu viongozi na malumbano yao badala ya kuandika habari zinazohusu ustawi wa wananchi.

  IPPMedia
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na huyu mkuu Warioba kwamba Bunge sasa linaingilia mambo mengi ya utendaji wa serikali na taasisi zake, na sijui kama kuna sheria za bunge kufanya kazi za serikali juu ya dipolomasia.

  Bunge lilipeleka wajumbe Uingereza juu ya shauri la kurudishiwa change, kwa utaratibu huu wameingilia kazi ya balozi zetu zilizoko huko. Kwa utaratibu huo ni kunyang'anya kazi za sipolomasia za serikali labda sababu ya ulaji kutafuta posho?

  Ujumbe mwingine ulitumwa kufuatilia vitambulisho vya taifa huko mashariki ya mbali, ina maana balozi zetu za ukanda huo hazipo?:
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na Mzee Warioba. Nilikuwa najiuliza hizi kamati za bunge zinatumia mamlaka gani kutoa directions kwa taasisi zilizo chini ya serikali. hii ndio inafanywa mpaka wabunge kuhongwa. Pia kuna hili suala ya wabunge kuwa wanadiplomasia. Kuna wabunge walienda London ku negotiate change ya radar wakati waziri mhusika yupo. Pia wapo wabunge walienda Malaysia kutembelea ile kampuni iliyopewe mkataba wa kutengeneza vitambulisho. Mpaka niabu spika amekuwa diplomat sasa. Kwenye ile video ya kamati ya bunge la Uingereza likiwahoji maafisa wa BAE System kuhusiana na suala la Radar nilimwona Cheyo nae alikuwepo kwenye room. What was he doing there wakati alitakiwa kuwa bungeni Dodoma ku-scrutinise bajeti za wizara mbalimbali? Kuna tatizo hapa.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe bunge limeingia kwenye mfumo wa uvujaji wa pesa wa kitaasisi, ni hii ni njia ya kuchuma pesa baada ya kunogewa na posho sasa wamefikiwa kiwango cha usemi huu: "Zaidi mtu apatavyo ndivyo atamanivyo."
   
 11. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Safari hizo kwenda kwenye Taasisi za umma na hata nje ya nchi ni mpango maalum wa kujilipa posho kwa hawa "waheshimiwa" wabunge, maana hawana ulazima wa kuyafanya hayo
   
Loading...