Dr Salim Abdulla akamatwa kwa kosa la Ugaidi ?

Waungwana,

Sasa kama jamaa kakamatwa na kuhusishwa na ugaidi, mnataka serikali ifanye nini?

Hili jambo pelekeni mahakakama kuu na kama hakuna ushahidi wala hana case basi ataachiwa. Mbona huyo mwingine inasemekana kaachiwa?

Kama kweli ni gaidi mnataka serikali isifanye kazi yake mpaka nchi ilie?

No compromise kwenye issues za usalama wa raia na wageni wetu.

Lazima mujue hata magaidi wanaweza kuwa ndugu zetu, marafiki zetu na watu tunaoshinda nao kila siku.

Mtanzania kumbuka huu si wakati wa Mwalim Nyerere mtu akikamatwa basi watu haturuhusiwi kuhoji. Lazima tuhoji...
Pia Jua Hapa tanzania ni sehm moja wapo Bill ya Ugaidi imepitishwa..(FISADI wenu MKAPA alitetea hii ktk the so called Hotuba za Rais)..ni BIll ya Uonevu ambayo amerika amefanya Kuhonga kupitishwa. Kama utawala wa kuzingatia HAKI za KIBANAADAMU kama mtu anahusika na ugaidi wampeleke MAHAKAMANI na si kukaa nae chemba then apelekwe Guantanamo...

Bahati Mbaya tangu Bill hii ipitishwe Victims wamekuwa Muslim proffessionals. Kenya wenzetu ni uonevu kwenda mbele. Tanzania tumeshuhudia Masheikh wakikamatwa na hili kitu ugaidi...eti mtu akishukiwa tu..Polisi wanaweza kukupiga Risasi hii sheria au uonevu? Iweje mtu akushuku tu...? Ndio pale tunapo muhoji MKAPA na askari wake ktk suala la mwembechai..eti kijana Chuki ATHUMAN kapigwa risasi eti ameonekana na Makaratas ya Uchochezi....Hayo makaratasi mlioyaona mkayasoma remotely?...

Waliomkamata wanatakiwa wamfikishe mahakamani...sio kukaa nae KUSIKOJULIKANA...is it? this is rule of Law?...

Tunaiomba Serikali yetu watoe Taarifa Maalum ya KUNAKULIKANA KWA Dr. Salim Abdulla...

Wengine jueni kuwa kazi alizokuwa anafanya ni proffessionals ya utafiti. na inajulikana Taasis ya Ifakara kwa muda mrefu imekuwa ina lead ktk reseach zake hasa ktk Tafiti za Ugonjwa wa Malaria.
Inavyoonekana ni kikundi cha watu chenye HUSDA baada ya kuonekana Dr. Salim anaoongoza taasis hio isio na UFISADI kama BUZWAGI, BOT na kwingineko.
 
Kuna uwezekano kuwa huyu jamaa kabambikiwa kwa huo huo udini? au haiwezekani? Maana Ifakara na ugaidi duhh!

Jamaa hajabambikiwa, ana mahusiano ya karibu sana na shemeji yake toka Mombasa ambaye ni alkaeda mkuu!, Huyu Dr, alisha hojiwa huko nyuma na Polisi na kuonywa uhusiano wake na shemeji yake huyo, na kwa kisngizio cha ghasia za Kenya shemejiye kwa sasa kahamia kwake, kwahiyo kuna uhusiano mkubwa ama wa moja kwa moja ama wa kimazingira unao muhusisha Dakitari huyu na ughaidi.

Mkurugenzi wa kituo cha Ifakara ni Dr. Hassani, huyu Dr. Salim ni wa wa Ifakara ila Kitengo cha Bagamoyo.
 
Ni mara ya kwazwa Tz kupata hizi tuhuma.. ni aibu sana kwa wataalamu wetu kuusika na haya mambo ya aibu... tuombee Mungu mambo yawe poa..ila tayari jina la Ifakara limechafuka tayari over terorism.. hii sii poa kwa nchi yetu!
 
Jamaa hajabambikiwa, ana mahusiano ya karibu sana na shemeji yake toka Mombasa ambaye ni alkaeda mkuu!, Huyu Dr, alisha hojiwa huko nyuma na Polisi na kuonywa uhusiano wake na shemeji yake huyo, na kwa kisngizio cha ghasia za Kenya shemejiye kwa sasa kahamia kwake, kwahiyo kuna uhusiano mkubwa ama wa moja kwa moja ama wa kimazingira unao muhusisha Dakitari huyu na ughaidi.

Mkurugenzi wa kituo cha Ifakara ni Dr. Hassani, huyu Dr. Salim ni wa wa Ifakara ila Kitengo cha Bagamoyo.

Rwagubiri..ahsante kwa taarifa...kutokana na Ghasia za Kenya wenye ndugu wengi tu wapo Tanzania...Mbona hawafuatwi? Hata wewe kaa ungekuwa na ndugu huwezi kukubalia ateseke nawe fursa unayo.

Ndio maana nikasema hii sheria ya Ugaidi si sahihi na ndio maana Tunampinga Shetan Bush. Huyo Ndugu yake kwa kuwa mwislam basi gaidi..is it? Kwanini Polisi kama wana ushahidi wasimchukue huyo Nduguye pekee? na pia bado hakuna ushahidi wa namna hio na tuhuma ambazo wanataka kumpakazia..ila Jueni ipo siku HAKI itakuwa wazi.
 
Chuma poleni!

Nchi yetu hutawaliwa kwa misingi ya sheria!

Issue kama Salim Ablllah anatuhumiwa kwa tetesi za ugaidi.. basi apelekwe mahahamani..sheria ichukiwe mkondo wake!

Sina data zaidi sijui kama kumsingizia Salim..ila hii ni aibu kwa watafiti wa nchi yetu!

Pole Dr. salim abulah!
 
Nimepewa habari hii na ndugu Ushirombo ikiwa na mada haya .Natafuta ukweli na kama kuna mwenye kuujua ukweli basi tuungane .Waandishi wa habari najua mnapita hapa tafadhali msiishie kwa Bush pekee saidieni kujua ukweli wa haya madai.

Dear Bro

Bwana kuna watanzania wamekamatwa na wanaojiita usalama wa taifa ati kuhusishwa na ugaidi wakati wa maandalizi ya kuja Bush Tanzania. Watu ninaofahamu nani uhakika nao mmoja wao ni Dr Salim Abdulla alikuwa ni mkuu wa kituo cha utafiti Bagamoyo Research and Training Unit (BRTU) ambacho kiko chini ya Ifakara Health Research Center. Dr Salimu amekamatwa wiki iliyopita kwa kuhusishwa na ugaidi, juhudi zimefanywa hadi kwenda kwa IGP na raisi lakini JK amesema ni issue ya FBI. Mkewe amehojiwa na ndugu wote lakini Dr Salim ameendelea kuwa rumande ..sijui kama sheria ya ugaidi ipo Tanzania pia? Kuna jamaa mwingine yeye anafanyia Ifakara Center anaitwa Fereji Mehboob pia alishika na kuhojiwa kwa masaa mengi na kuachiwa sasa sijui kwanini hawajamaa wanafanyia watu ukatili huo? Hizi ni habari nimeambiwa na jamaa waliokuwa wanafanya kazi bagamoyo na Dr Salimu Bagamoyo, ila kifupi kuna watu kibao wako ndani hadi Bush atakapoondoka Tanzania....kama unaweza fatilia itakuwa poa

Ushirombo

Lunyungu na Ushirombo,

Mimi hapa naingiwa mashaka kidogo na "heading" yako.

Huyu Dk Salim amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi au amekamatwa kwamba tayari ametenda kitendo cha ugaidi naomba ufafanuzi.

Nafikiri unaelewa tofauti kati ya tuhuma na hatia (kukiri/ kukataa kosa) na hatimae kuhukumiwa.

Au kakamatwa kwa kosa la kukimbia?
 
Chuma poleni!

Sina data zaidi sijui kama kumsingizia Salim..ila hii ni aibu kwa watafiti wa nchi yetu!

Pole Dr. salim abulah!
Mzalendo samahani...statement yako naona umeirudia kuwa Hii ni aibu kwa watafiti wetu...as if Huna HAKIKA KUWA JAMAA ANAHUSIKA...Na kama huna hakika basi ifute hii kauli...

Dotori...Kama umesikia ulishawahi kuhoji udini upo sehem gani? kwa utafiti wangu wa hapa JF na huko nyuma before JF, ni kuwa; kama kitengo kitaongozwa na Mwislam basi hapo Kuna UDINI. Kama hivi ndivyo uoni wa wengi basi Mwislam hata kama anafaa basi nafasi ya Juu Hapaswi kuwepo....Kwa utaratibu Huu nchi mnapoipeleka kubaya. Dotori, Mzalendo na wengine hebu wekeni basi registered employee wote wa Hichi kitengo cha Utafiti kwasababu wakija wengine nao wakisema tunasikia bila utafiti maana yake uvumi unaeenea na wakija Guest hapa JF..ataenda kusema kwa 100% confidence kuwa IFAKARA Health reseach center kuna UDINI wakati zoote ni Majungu.

...Mie naamini vipo vitengo vingi ambavyo ukimkuta mwislam basi muhudum wa chai, Messenger au Dereva. au hiz ndio kazi mlizowachagulia waislam?
 
List ya wanayasayansi wa IFAKARA RESEARCH CENTER ambayo nadhani ina tawi Bagamoyo inaposemekana alipo Dr Salim.

Source:

[media]www.indepth-network.org/dss_site_profiles/Ifakaraprofile.pdf[/media]

4.4 List of Scientists
1. Dr. Hassan Mshinda - PhD Molecular Biology
2. Dr. Salim Abdulla - MD, PhD Epidemiology
3. Dr. Rose Nathan - PhD Demography
4. Mr. Charles Mayombana - MSc Community Health (PhD student)
5. Mr. Kefas Mugittu - MVM (PhD student– Molecular Biology)
6. Mr. Honorathy Urassa - MSc Medical Microbiology
7. Mr. Oscar Mukasa - MSc Medical Informatics
8. Mr. Abdallah Mkopi - MSc Epidemiology and Biostatistics
9. Mr. Honorati Masanja - MSc Medical Statistics
10. Dr. Boniface Idindili - MD, MPH
11. Dr. Abdulnoor Mulokozi - MD.
12. Mr. Hadji Mponda - Advanced Diploma in Marketing (MSc student)
13. Mr. Allen Malisa - MVM
14. Ms Modesta Ndejembi - BSc (PhD student – Molecular Biology)
15. Mr. Ahmed Makemba - MPH
16. Mr. Joseph Mugasa - MSc. Molecular Biology
17. Mr. Hezra Mrema - MSc. Environmental Science
18. Mr. Rashid Khatib - MA Sociology
19. Mr. Mwifadhi Mrisho - MA Demography
20. Mr. Godlove Stephen - MA Economics
21. Mr. Joseph Njau - MA Economics
22. Mr. Sosthenes Charles - MSc Medical Statistics
23. Ms. Fatuma Manzi - MSc Economics
24. Ms. Valeriana Mayagaya - BSc. Biology
25. Ms Sally Mtenga - Bsc. Community Development
26. Mr. Paul Mahunga - BA Statistics
27. Mr Suleman Mbuyita - BSc. Agriculture Science
28. Mr John Rutaihwa - BSc
29. Mr Denis Kamugisha - BSc
30. Ms Emmy Meta - MA sociology
31. Ms June James - MA Sociology
32. Ms Angela Kimweri - MA Sociology

Nimepata hiyo report ktk net nadhani ni ya mwaka 2003-2004 haijaandikwa ila nimekisia kwa kuwa zipo publication katika list za mwaka 2003. Wapembuzi wapitie tuangalie udini ktk taasisi hii nadhani majina yatosha kutoa picha halisi.
 
Chuma,

Muhimu kama wapo Watz wanajihushisha na ugaidi basi wakamatwe na wapelekwe mahakamani.. mimi simtetei Mtz yoyote ambae ana tuhuma kama hizi!

Ndo maana nasema ni aibu kwa Ifakara na nchi yetu! Tz tumekuwa tunaishi kwa amani siku zote.. tunapendana Waislamu kwa wakristo! Na ibakiae hivyo!
 
List ya wanayasayansi wa IFAKARA RESEARCH CENTER ambayo nadhani ina tawi Bagamoyo inaposemekana alipo Dr Salim.

Source:

[media]www.indepth-network.org/dss_site_profiles/Ifakaraprofile.pdf[/media]

4.4 List of Scientists
1. Dr. Hassan Mshinda - PhD Molecular Biology
2. Dr. Salim Abdulla - MD, PhD Epidemiology
3. Dr. Rose Nathan - PhD Demography
4. Mr. Charles Mayombana - MSc Community Health (PhD student)
5. Mr. Kefas Mugittu - MVM (PhD student– Molecular Biology)
6. Mr. Honorathy Urassa - MSc Medical Microbiology
7. Mr. Oscar Mukasa - MSc Medical Informatics
8. Mr. Abdallah Mkopi - MSc Epidemiology and Biostatistics
9. Mr. Honorati Masanja - MSc Medical Statistics
10. Dr. Boniface Idindili - MD, MPH
11. Dr. Abdulnoor Mulokozi - MD.
12. Mr. Hadji Mponda - Advanced Diploma in Marketing (MSc student)
13. Mr. Allen Malisa - MVM
14. Ms Modesta Ndejembi - BSc (PhD student – Molecular Biology)
15. Mr. Ahmed Makemba - MPH
16. Mr. Joseph Mugasa - MSc. Molecular Biology
17. Mr. Hezra Mrema - MSc. Environmental Science
18. Mr. Rashid Khatib - MA Sociology
19. Mr. Mwifadhi Mrisho - MA Demography
20. Mr. Godlove Stephen - MA Economics
21. Mr. Joseph Njau - MA Economics
22. Mr. Sosthenes Charles - MSc Medical Statistics
23. Ms. Fatuma Manzi - MSc Economics
24. Ms. Valeriana Mayagaya - BSc. Biology
25. Ms Sally Mtenga - Bsc. Community Development
26. Mr. Paul Mahunga - BA Statistics
27. Mr Suleman Mbuyita - BSc. Agriculture Science
28. Mr John Rutaihwa - BSc
29. Mr Denis Kamugisha - BSc
30. Ms Emmy Meta - MA sociology
31. Ms June James - MA Sociology
32. Ms Angela Kimweri - MA Sociology

Nimepata hiyo report ktk net nadhani ni ya mwaka 2003-2004 haijaandikwa ila nimekisia kwa kuwa zipo publication katika list za mwaka 2003. Wapembuzi wapitie tuangalie udini ktk taasisi hii nadhani majina yatosha kutoa picha halisi.

Chuma

Binafsi sioni udini ktk haya majina.. ila sijui hizi tetesi mitaani za udini Ifakara zinasababishwa na nini! Naona kama 35% ni Waislamu na 65% ni Wakiristo! Naona kama Waislamu bado ni wachache kuliko Wakristo! Well kama ajira ni qualifications basi whoever qualifies na ni Mtz haina neno!

Taabu haya mambo ya udini Ifakara watu wanaongea mtaani sijui ni kwa nini..sasa naona sii kweli! Na sijui kwa nini watu bado wanasema!
 
Udini ni nini?
Maana kutokana na logic iliyotengenezwa hapa, ukiangalia list hiyo, mwislamu anaweza kusema kuna udini. Au udini ni pale tu waislamu wanapozidi?
 
Huwezi kutambua udini kwa kuangalia majina ya watu. Pia huwezi kutambua udini hata kama utazijua takwimu za asilimia za watu wa kila dini kwenye sehemu fulani. Udini huwa ni SERA (ya wazi au ya kificho) ya kuwapa watu wa dini fulani manufaa fulani kwa upendeleo dhidi ya watu wa dini nyingine. Aina zote za ubaguzi ziko hivyohivyo. Haihusiani na suala la idadi ya watu wa dini fulani kwenye hiyo sehemu hata kidogo. Mifano rahisi ipo: Kule Rwanda baada ya 1994 serikali iliundwa ya "mseto" ikichanganya watusi na wahutu. Ungehesabu idadi ya wahutu kwenye serikali kweli walikuwa wengi zaidi (Rais na Waziri Mkuu pia walikuwa wahutu), lakini watusi wachache ndio waliokuwa na nguvu na mamlaka hadi leo. Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kusimulia jinsi alivyotuhumiwa udini enzi za utawala wake, tena tuhuma zilienezwa kuwa si tu kwamba anapendelea wakristo kwenye baraza la mawaziri, bali walisema anapendelea wakatoliki. Kuonesha kuwa hakuwa na upendeleo akaitisha idadi ya viongozi na dini zao, akagundua wakatoliki walikuwa yeye na George Kahama tu (tena akadai Kahama "hakuwa mkatoliki" kwani alikuwa ameoa mke wa pili, kinyume na ukatoliki!) Lakini bado nasema mimi kuwa idadi ya watu si jibu. Sina ushahidi kuwa Nyerere alikuwa na udini au la, lakini njia aliyotumia kujibu kuwa hakuna udini haikujibu tuhuma kikamilifu (labda kama waliolalamika walizungumzia "idadi" ya wanaoteuliwa, na si sera ama utaratibu wa uteuzi ama nguvu za hao wateuliwa).

Kadhalika sina uwezo wa kusema kuwa huko Ifakara kuna udini au la (kwanza silijui hilo shirika kwa undani), lakini jibu lililotolewa la idadi ya watu halitusaidii kujua kuwa hilo shirika la Ifakara kuna udini au la! Kwa kuangalia tu hayo majina na hata ukijua dini zao wote, bado hutaweza kusema kuna udini!

Sisi tusiofahamu hilo shirika tungeweza kuamini kweli kuna udini au la iwapo masuali yafuatayo yangejibiwa:
a) Je katika shirika hilo dini ya mtu ndio kigezo cha mtu kupewa manufaa ambayo wasiyo na dini hiyo wanayakosa kwa sababu tu ya dini?
b)Je Katika shirika hilo dini ya mtu ndio kigezo cha yeye kusikilizwa au kukubaliwa mapendekezo ama maoni yake?
c)Je Katika shirika hilo kuna watu wanaotengwa ama kunyanyaswa kwa sababu ya dini zao?
d)Je Katika shirika hilo kuna watu wa dini yoyote ambao mahitaji yao ya msingi ya kidini (ambayo kiserikali yanakubalika) wananyimwa ama kuzuiwa? (Hali inayoweza kumfanya mtu aone kufanya kazi hapo huku ukiwa na dini hiyo ni mateso?) Mfano kumshurutisha mfanyakazi mambo ambayo ni kinyume na maadili ya dini yake na hata sheria za nchi, na hayo kumfanyia wa dini fulani tu (watu wa dini fulani sikukuu zao wanashiriki vizuri, wale wa dini nyingine sikukuu zao zikifika wanapangiwa majukumu, mfano). Je kuna mambo yanayofanana na hayo?
e) Je katika shirika hilo mamlaka (si madaraka) aliyo nayo mtu yanategemea dini yake?

Katika yote niliyotaja (a) hadi (e) hapo juu utagundua kuwa idadi ya watu si muhimu, muhimu ni kwamba hao waliopo wanatendewaje?

Kwa ujumla, tupewe ushahidi wa ki-SERA (ya kificho, isiyoandikwa, au hata ya wazi) unaoonesha upendeleo wa watu wa dini moja dhidi ya nyingine, huo ndio utakuwa udini. Idadi au majina si hoja. Mpaka sasa hakuna aliyetuthibitishia madai hayo ya udini dhidi ya Ifakara Research, na wala hakuna aliyetuthibitishia kuwa hakuna udini. Kilichokosekana ni utafiti. Kuwepo kwa udini hapo kwenye shirika inaweza kuwa tuhuma ni ya kweli ama ni ya uongo. Lakini kwa kuwa shirika hilo msingi wake si wa udini, ni busara a haki kuamini hakuna udini, hadi hapo ushahidi utakapoonesha vinginevyo. Mimi silifahamu hilo shirika, sijui kama kuna udini au la, lakini kwa kuwa udini ni tuhuma ya ubaguzi na ni mbaya, napenda kulitendea haki hili shirika (tuite natural justice, kwamba they are innocent unless there is evidence to the contrary). Kama evidence hiyo hakuna, ni aibu kwa watu wazima tena wasomi kujadili jambo kwa misingi ya "nasikia hivi, nasikia vile!" huo utakuwa udaku.
 
Very low of u discussing issues without any credible evidence.

Shame on you! Acheni udini!
 
Shame on you! Acheni udini!

Shame on you kuacha watu wapige majungu ya udini zinapokuja data ndio unakuja na statement kama hizo.

Udini ni nini? = Kwa Tanzania udini unakuwapo pale tu idadi ya waislam ngazi za juu inakuwa kubwa kuliko wakristo.

Tusiyeyushane wazee, sote ni watu wazima, ushahidi upo mwingi wa hayo na hii nchi yetu sote!
 
Nadhani tuachane na udini tuangalie tatizo lililopo pana watu sensitive maana kusikia amekamatwa wameanza kuangalia vigezo ambavyo hawavipendi jina lake dini yake etc, unapotetea haki usiangalie jina wala dini ya mtu, cha muhimu ni kupembua je DR salim ni amekamatwa kwa ugaidi kweli au ni mabavu ya serikali yetu, nimesoma pia wana JF wameanzwa kufuatwa fuatwa na watu wanaojiita wanausalama je nao ni kwa sababu zipi? tatizo nchi yetu haina uhuru, uhuru wa lolote ingawa tunaambiwa pana uhuru wa kuongea, etc

Mimi binafsi nadhani ni vema hasa kujadili Je Dr salim amehusishwaje na ugaid, ni kwa vile anashemeji yake ambaye nasikia anahusika na ugaidi mombasa?! au na yeye alitaka kumripua kichaka??? kama ni kwa ajili ya shemejie inamaana ukiwa na ndugu jambazi nawe jambazi, hata ukikutana nae usimsalimie kwa kuwa jambazi, huyo gaidi wanaemuita gaidi mkuu Osama bin Laden anafamilia, anawake na watoto wanaishi huru na wanatumia fedha na makampuni hayo hayo ya bin Laden family kuendesha maisha yao je wote wawekwe ndani, huu ni uonevu kama hiyo ni sababu na huu ni unyenyekevu na nidhamu ya woga kwa ajili ya ujio wa bwana mkubwa kichaka,

Nadhani magaidi wabaya kwa nchi yetu ni hao wanaotumia rasilimali kwa manufaa yao binafsi kama lowassa na wenziwe ambao ndio wanasababisha hali ya maisha kuwa mbaya na kuendelea kutegemea misaada ya akina bush kichaka na kuendeleza nidhamu za woga na kutowatendea watu haki zao, na kama Dr salim kweli anahusika basi sheria ichukue mkondo wake na sio kumficha pasipo julikana na kufanya issue kuwa ni siri!!!

INATISHA na KUOGOPESHA,
 
Shame on you kuacha watu wapige majungu ya udini zinapokuja data ndio unakuja na statement kama hizo.

Udini ni nini? = Kwa Tanzania udini unakuwapo pale tu idadi ya waislam ngazi za juu inakuwa kubwa kuliko wakristo.

Tusiyeyushane wazee, sote ni watu wazima, ushahidi upo mwingi wa hayo na hii nchi yetu sote!

Nungunungu,

Sikuwa nimeona hii thread toka mwanzo. Data zipi zilizoletwa?, mzee tulia tafakari kwanza. Hizo unazoita wewe "data" ni za mwaka 2003/2004. Leo ni 2008, Amka bro/dada acha kulala. Chadema wamekataa kulala, CCM tunasema maisha bora kwa kila mtz.

Ninachozungumzia ni kuwa zije "data" au "Facts" I DONT CARE.

SIMPLY PUT, ACHENI KUTUMIA UDINI KAMA VIGEZO.
 
Rwagubiri..ahsante kwa taarifa...kutokana na Ghasia za Kenya wenye ndugu wengi tu wapo Tanzania...Mbona hawafuatwi? Hata wewe kaa ungekuwa na ndugu huwezi kukubalia ateseke nawe fursa unayo.

Ndio maana nikasema hii sheria ya Ugaidi si sahihi na ndio maana Tunampinga Shetan Bush. Huyo Ndugu yake kwa kuwa mwislam basi gaidi..is it? Kwanini Polisi kama wana ushahidi wasimchukue huyo Nduguye pekee? na pia bado hakuna ushahidi wa namna hio na tuhuma ambazo wanataka kumpakazia..ila Jueni ipo siku HAKI itakuwa wazi.

Ndugu Chuma,
Huyu jamaa si kwamba kafatwa kwa vile nduguye toka Mombasa yupo, kama nilivo eleza hapo nyuma, amekuwa na mahusiano na huyo shemejie siku nyingi hata kabla ya machafuko huko Kenya, kiasi kwamba alisha kamatwa na kuhojiwa juu ya tuhuma hizi. Kwa hiyo kukamatwa kwakwe sasa hivi si mara ya kwanza, pamoja na huyo nduguye kuja kwake sasa hivi lakini mazingira na historia ya tuhuma za kuhusika kwake ni za muda sasa!

Tusubilie matokeo badala ya kujenga dhana kwamba anaonewa, kama si kweli ataachiwa kama alivo achiwa alipo onywa juu ya mahusiano hayo. Kwani naamnini alipo hojiwa mara ya kwanza haukuwa mwisho wa kuendelea kumchunguza mwenendo wake. na pengine kukamatwa kwake sasa ni matokeo ya uchunguzi ulio kuwa ukiendelea.
 
Rwagubiri...Tusubiri hayo matokeo...Kinachotia shaka ni kuwa kwanini wamfiche? waweke wazi?

Unajua nini amerika ameambiwa juu ya watuhumiwa wale wa Guantanamo? Watu wapelekwe mahakamani.kitendo cha kumhusisha mtu Gaidi bila ushahidi anytime anyperson anaweza husishwa. Kama watu JF hapa hatupingi hili eti tu kwa kuwa limetokea kwa Fulani...tutashindwa tu siku za Usoni.

Kithuku kwa maelezo uloyaweka yangetosha kuhitimisha mijadala mingi iliyoanzishwa
 
Back
Top Bottom