Dr Salim Abdulla akamatwa kwa kosa la Ugaidi ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Salim Abdulla akamatwa kwa kosa la Ugaidi ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Feb 17, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nimepewa habari hii na ndugu Ushirombo ikiwa na mada haya .Natafuta ukweli na kama kuna mwenye kuujua ukweli basi tuungane .Waandishi wa habari najua mnapita hapa tafadhali msiishie kwa Bush pekee saidieni kujua ukweli wa haya madai.

  Dear Bro

  Bwana kuna watanzania wamekamatwa na wanaojiita usalama wa taifa ati kuhusishwa na ugaidi wakati wa maandalizi ya kuja Bush Tanzania. Watu ninaofahamu nani uhakika nao mmoja wao ni Dr Salim Abdulla alikuwa ni mkuu wa kituo cha utafiti Bagamoyo Research and Training Unit (BRTU) ambacho kiko chini ya Ifakara Health Research Center. Dr Salimu amekamatwa wiki iliyopita kwa kuhusishwa na ugaidi, juhudi zimefanywa hadi kwenda kwa IGP na raisi lakini JK amesema ni issue ya FBI. Mkewe amehojiwa na ndugu wote lakini Dr Salim ameendelea kuwa rumande ..sijui kama sheria ya ugaidi ipo Tanzania pia? Kuna jamaa mwingine yeye anafanyia Ifakara Center anaitwa Fereji Mehboob pia alishika na kuhojiwa kwa masaa mengi na kuachiwa sasa sijui kwanini hawajamaa wanafanyia watu ukatili huo? Hizi ni habari nimeambiwa na jamaa waliokuwa wanafanya kazi bagamoyo na Dr Salimu Bagamoyo, ila kifupi kuna watu kibao wako ndani hadi Bush atakapoondoka Tanzania....kama unaweza fatilia itakuwa poa

  Ushirombo
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe Lunyungu acha sensationalise story yaani hicho kichwa cha habari ulivyokiweka kila mtu atajua ni Dr Salim Ahmed Salim!

  Unaandka habari kama gazeti la ijumaa kichwa cha habari "Rais auawa!" ukisoma ndani Rais wa chama cha vinyoya!

  Grow up mkuu u r bigger than that...
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Feb 17, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Aaaahh...hiki kichwa cha habari si kizuri...kimekaa ki-tabloidish. Niliposoma mi nikadhani ni yule Dk. Salim tuliyemzoea....
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hii mpya- kwani Dr. Salim Abdulah anajihusisha na ugaidi? Ila kweli kuna tetesi Ifakara wana upendeleo kuajiri kwa misingi ya dini zaidi!

  Huyu jamaa nimeangalia machapisho yake- ya kisayansi ni mengi!

  Mwenye habari zaidi atujulishe!
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Masatu
  Huyu naye si ni doctor Salim jamani ?Haya nisemehe maana naona unanichukia ghafla .
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni kweli huyo msomi amekamatwa zaidi ya wiki moja sasa. Hajafunguliwa mashtaka na wenzake katika kituo cha Ifakara wanadhani kuna uhusiano na ziara ya rais Bush.
   
 7. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2008
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Lunyungu or Jasusi

  Could you please give me the full name of the said Dr. so that I can change the heading.
   
 8. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2008
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  mmhhhhhhh! interesting!
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..jasusi,

  ..moja ya wafadhili wa ifakara ni u-swiss. ina maana hawa wazungu wanafadhili ugaidi bila kujua?

  ..hao jamaa wengine kina nani?
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Dr.Salim Abdullah .Ole now you have the name
   
 11. C

  Chuma JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzalendo halisi madai yako ni uzushi unless utuwekee hapa wote waliajiriwa hapo IFAKARA wote...

  MzalendoHalisi..bora ubadili jina lako uweke MKEREKWETWA(DINI YAKO)HALISI .....ila mjue nchi mnapoipeleka Pabaya...
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyu nae alikuwa anataka kumripuwa kichaka?
   
 13. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Chuma,

  Heshima Mkuu!

  Wewe umeangalia management ya Ifakara? Well kama siyo concidence Waislam kupewa kipaumbele kwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ni Mwislamu kwa kweli sijui! Ila ukweli ni kuwa kuna tetesi za ajira za upendeleo!

  Angalia hata hizi tuhuma za Dr. Salim Abullah hukusishwa na ugaidi!

  Ni watu wanasema mitaani mzee! Sasa utawazuia watu wasiseme? Lisemwalo lipo- sina ushahidi zaidi!
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  si kila lisemwalo lipo mkuu, mpaka tuthibitishe kuna watu wanasema kuna mungu na wengine wanasema hakuna sasa yote mawili yapo?


  halafu ss wanasayansi tunasema tetesi hazifanyi kitu kuwa kweli.

  na ndio wengine wakafika kusema no research no right of saying.
   
 15. C

  Chuma JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzalendo hivi mwislam kuwa Mkurugenzi ni UDINI?..tueleze hao walipo huko ni wamependelewa au haki yao?

  Kama nilivyokueleza awali waambie walokutuma waweke AJIRA ya watu wato wote walioajiriwa hapo IFAKARA...au kama umefanya utafiti binafsi basi uweke hapa..usilete uzushi ukaipeleka Nchi Rwanda
   
 16. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mtu wa Pwani nakubaliana na wewe kabisa, haiwezekani kila lisemwalo likawepo! Na mfano uliotoa ni mzuri sana. Kama kuna watu wanakuja na hypothesis kuwa ajira za hiyo taasisi zinatokana na udini, wafanye utafiti kweli wa kisayansi ku-test hypothesis hiyo na kama ni ya kweli inaweza kuwasaidia wahusika feedback namna ya kuimarisha taasisi yao. Kama ni za uongo basi ikithibistishwa ni uongo itawasaidia kutunza jina lao zuri. Lau kama hakuna mwenye uthibitisho huu, basi watu WAKAE KIMYA na waache kutuletea conclusion za kuzua. Mie sifahamu undani wa hiyo Ifakara Centre, lakini napingana na conclusion zinazotokana na habari za Udaku, tetesi, ati "watu wanasema"! Watu watasingiziwa mengi sana kwa mtindo huu. Lakini kama kuna mwenye ushahidi atuwekee hapa, tunao uwezo wa kuuchambua na kung'amua kuwa huu kweli udini au siyo.

  Wenye details za hiyo kesi ya huyo Dr Salimu Abdulla naomba pia watupatie. Alikuwa anajihusisha na utafiti wa mambo gani? Inawezekana hayo aliyokuwa anatafiti ndiyo yamemtia matatani.
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Chuma,

  Acha hasira- sisi Watz mambo ya Rwanda wewe ndo unasema! Watu wanasema kuna upendeleo ajira Ifakara kwa misingi ya dini---sasa this is a message!

  Mbona tumeongelea kwa kina ukabila, upendeleo Ikulu, BoT N.k?? What is so special na Ifakara? Yet bahati mbaya Ifakara wameshatuhumiwa tayari kwa ugaidi..sasa nani unalaumu?

  Kama ndo unapofanyia kazi basi rekebisheni mambo huko.. ni changamoto.. tujadili and we movefoward.. na sii kusema mambo ya kutumwa!

  Sasa Hili za Salim Abdullah je ni mimi pia nimemsingizia?

  Let us discuss beyond the box!

  Ufsadi sii wizi tu wa mali ya uma ni pamoja na upendeleo kwa misingi ya rangi, dini n.k
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna uwezekano kuwa huyu jamaa kabambikiwa kwa huo huo udini? au haiwezekani? Maana Ifakara na ugaidi duhh!
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Waungwana,

  Sasa kama jamaa kakamatwa na kuhusishwa na ugaidi, mnataka serikali ifanye nini?

  Hili jambo pelekeni mahakakama kuu na kama hakuna ushahidi wala hana case basi ataachiwa. Mbona huyo mwingine inasemekana kaachiwa?

  Kama kweli ni gaidi mnataka serikali isifanye kazi yake mpaka nchi ilie?

  No compromise kwenye issues za usalama wa raia na wageni wetu.

  Lazima mujue hata magaidi wanaweza kuwa ndugu zetu, marafiki zetu na watu tunaoshinda nao kila siku.
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na maneno yako moja kwa moja na sina la kupinga .Kila siku US watu wanauwa watu kwa ile kitu inaitwa Spree shooting baadaye wanasema watu wale ni wapole sana na hawakuwa na dalili za ukorofi akina Mohammed Atta and the likes.So huyu mwacheni akae itajulikana tu .
   
Loading...