Dr. Rutengwe afunguka, asema acha watanzania wazungumze (Audio)

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Dr. Rajab Rutengwe (PhD) aliyekua Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye hajateuliwa katika uteuzi mpya wa wakuu wa Mikoa, amezungumza kwamba watanzania waachwe waongee ila yeye yuko kijijini akiendelea na shughuli mbalimbali za kilimo na ikumbukwe kuwa sasa ni msimu wa kuandaa mashamba.

Ikumbukwe Dr. Rajab Rutengwe aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro hivi karibuni alidai toka aachishwe kazi amepoteza mwelekeo na amekuwa tegemezi kwa familia yake maskini.

Rejea video hii

Pia Dr. Rutengwe alidai haelewi amekosea wapi mpaka amefutwa cheo na hitimisho lake ni kuwa wasaidizi wake ngazi za chini wamechangia anguko lake.

Wakuu nimeambatanisha na sauti yake.
 
Attachments

  • Dr. Rutengwe.mp3
    770.4 KB · Views: 77
Habari wanaJF,

Dr. Rajab Rutengwe (PhD) aliyekua Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye hajateuliwa katika uteuzi mpya wa wakuu wa Mikoa, amezungumza kwamba watanzania waachwe waongee ila yeye yuko kijijini akiendelea na shughuli mbalimbali za kilimo na ikumbukwe kuwa sasa ni msimu wa kuandaa mashamba.

Nimeambatanisha na sauti yake.
Movie inaendelea, time will tell
 
ahahahaha Rutengweeee!!! haya baba andaa shamba na mvua zenyewe za mwaka huu mbona utaomba mahindi desemba!!!!ahahahaa dokta mzima nilitegemea ungekua ata unaandaa kitabu uwiii what a failure
 
Usikute wewe hapo hata buku huna mfukoni......maana unaemtegemea yupo njia kuu.
 
Nyoooo!! nianze tu kukosa pesa....wewe atakua nduguyo mnaetoka kijiji kimoja mnafichiana siri...nyie elimu haijawakwamua...sio sifa yenu kusoma!! elimu mtuachie sie ahahahahha tenaaa
 
Mbona unabwabwaja mdomo we nyumba ndogo ya GWANOMBO tulia bhasi acha kiherehere we una nini cha MAANA hapo mpaka umdiss DR .....we sifa yako si kuwa mchepuko Wa MTU najua hizo Ni akili za u mchepuko.....endelea kuishi LODGE mwenzio kapewa mjengo Wa MZIMA Wa milioni 250/=
 
Kuna watu wachache kizazi hiki wenye uthubutu wa kukubali mapungufu yao na kisha kuomba msamaha kwa wale wanaoamini kwamba waliwakosea. Pengine kosa kubwa la huyu Dr ni ndilo hilo.

Lakini pia tunapomhukumu tujiulize hiyo migogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Morogoro ilianza kipindi cha uongozi wake au nae aliikuta ikiwa imeshaota mizizi na yeye kushindwa kuitatua katika kipindi "kifupi" alichokuwa hapo mkoani kama mkuu wa mkoa? Pia tujiulize katika utumishi wake alikuwa ni mwadilifu kiasi gani kwa sababu hiyo "lia njaa" yake ndani ya kipindi kifupi baada ya kuukosa ukuu wa mkoa inaweza kuwa imechangiwa na uadilifu wake kazini.

Kingine tukumbuke kwamba uwa kuna kundi la watu uwa wanapenda kulia njaa, kwamba hawana kitu mbele ya watu wengine lakini kumbe akaunti zao zimenona na pengine huyu Dr naye yuko katika kundi hilo.

Nadhani tunapomchambua huyu Dr na kumwona kama kachemka kupitiliza sisi binafsi tunapaswa kujiuliza tumejiandaa kiasi gani ili kukabiliana na changamoto za maisha mara baada ya ukomo wa ajira (kustaafu, ulemavu, maradhi n.k), kukosa ajira kwa sababu mbalimbali, kuanguka kwa biashara zetu, anguko katika kilimo n.k. na hivyo kuendelea kuhudumia extended families zetu?

Mwisho niwaombe watanzania wenzangu wasomi na wasio wasomi kumchukulia huyu mkuu wa mkoa mstaafu kama reflection ya hali halisi ya mfumo wa elimu wa Tanzania ambao kwa kiasi kikubwa unamuandaa mtanzania kuajiriwa badala ya kujiajiri na kuajiri wengine na hivyo kutafuta njia muafaka za kuondoa hali hiyo miongoni mwa wasomi wetu na jamii kwa ujumla.
 
Uko sahihi inabidi tujifunze
 
ahahahaha Rutengweeee!!! haya baba andaa shamba na mvua zenyewe za mwaka huu mbona utaomba mahindi desemba!!!!ahahahaa dokta mzima nilitegemea ungekua ata unaandaa kitabu uwiii what a failure
Nyang'au Kweli Wewe. Kwani Wakati Anaendelea Na Kilimo Hawezi Kuandika?
 
Back
Top Bottom