Dr. Rajab Rutengwe: Nilinuia kurudisha ujumbe kwa Rais Magufuli

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,595
36,017
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Rajab Rutengwe amesema kuwa ujumbe aliotoa alipokuwa akikabidhi ofisi hivi karibuni aliyeuelwa ni yeye na rais Magufuli pekee.

Dr. Rutengwe anakiri kuwa kabla ya kutoa ujumbe huo hadharani, kulikuwa na mazungumzo ya ujumbe kati yake na rais Magufuli.

"Rais Magufuli alipokuwa akiwaapisha ma-RC wapya alitoa ujumbe kushutumu utendaji kazi wangu na kusema kuwa 'message sent and delivered' wengi hawakuelewa ila ni mimi na rais Magufuli pekee" anasema Dr. Rutengwe.

Aidha Dr. Rutengwe anasema kuwa ujumbe aliotoa wa "Sina pa kushika masikini mie, nimekosa mimi nimekosa mimi nimekosa sana. Rais Magufuli naomba unikumbuke katika ufalme wako" ulinuia kujibu ujumbe fulani aliotumiwa na rais Magufuli ambao hata hivyo hakuutaja.

"Hivi kwa hali ya kawaida mimi naweza kushindwa kujiendesha kweli? Niliwezaje kusoma hadi PhD? " Anaongeza Dr. Rutengwe.

Aidha Dr. Rutengwe anasema kuwa hatarajii na haitotokea kamwe kwa yeye kuwa tena muajiriwa ndani ya serikali ya rais Magufuli kutokana na sababu ambazo anadai kuwa zinajulikana kati yake na rais Magufuli.

Dr Rutengwe hivi karibuni alitoa ujumbe wenye ukakasi unaosomeka "Sina pa kushika masikini mie, nimekosa mimi nimekosa mimi nimekosa sana. Rais Magufuli naomba unikumbuke katika ufalme wako " ujumbe ambao anasema ni wa kifalsafa zaidi.
 
Kujichamba kwingi mwisho kushika mavi!! kadri anavyoongea ndivyo anavyoharibu zaidi
 
Ameyasema wapi hayo?
Maana mkuu wewe kwa habari za uzushi,ni kama Side wa hapa na pale University
 
Mtu akikaa na kuufikirisha ubongo kidogo atauona ujumbe ule ulikuwa na kejeli Fulani yaani satirical
Kutumia kitubio cha kikatoliki cha
"nimekosa mimi *3"
au "mea culpa"*3
Ni ushahidi ametumia fasihi kumkejele MtumbuaMajipu labda kwa hasira ya kuachishwa kazi
 
Sawa, huenda alitumia Falsafa kufikisha ujumbe, lakini kuna haja gani ya kuendeleza malumbano na Rais wakati keshakutema?

Kwa nini usikae kimya na kuacha Falsafa yako ikaeleweka kwa Wanafalsafa?
 
Rutengwe amechanganyikiwa tu

Hapana mkuu. Kama haya kayasema basi sio ajabu kuna jambo la ziada hatulijui. Tatizo la mzee Magu naye anajifanya anataka kuiga vijembe vya mzee wa Msoga wakati fani hiyo inawenyewe watu wa pwani yeye na hayo wapi na wapi?
Ndio dansi limeanza tutasikia single mpya nyingi
 
aise PHD holder ana lialia kama mtoto mdogo duuuu kweli elimu inazidi kupoteza thamani
 
Back
Top Bottom