Dr Prof Kikwete kafuta makosa yake yote amesamehewa atauona ufalme wa Mungu

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,883
31,049
Heshima kwenu wanajamvi,

Dr Prof Kikwete anatarajiwa kukabidhi hatamu za uongozi wa taifa mwezi October 2015 kwa kiongozi either kutoka chama chake anachokiongoza CCM au kutoka ile kambi maarufu "UKAWA".

Mchakato wa kutafuta atakayempokea hatamu za uongozi kutoka chama chake cha CCM ulikuwa mgumu sana si kwasababu mgombea msumbufu Edward Elowassa Ndossy alikuwa na nguvu kubwa au alikuwa mgombea madhubuti la hasha bali udhaifu wa CCM katika kukabiliana naye ndio sababu kuu ya kusumbuliwa.

Ifahamike Elowassa alianza usumbufu tangu mwaka 1995 kama si uwepo wa Baba wa Taifa Mwl Nyerere Mzee Ruksa alishashindwa kumdhibiti.Ni Mwl Nyerere aliyewaambia wajumbe wa Halmashauri kuu waache uhuni baada ya wajumbe kupiga kelele kama watoto wadago baada ya jina la Edward Ndossy kukatwa.

Benjamin W Mkapa alipopewa hatamu za uongozi alimrejesha tena Lowassa katika baraza la mawaziri jambo ambalo hata Mwl Nyerere alllishangaa baada ya kupewa taarifa na msaidizi wake Mzee Kasori kwamba Lowassa kateuliwa kuwa waziri wa Ardhi.Kosa la kwanza lilianza wakati wa Mkapa hakutakiwa kumrejesha Lowassa katika baraza la mawaziri.Tuhuma zote zilizotolewa na Mwl Nyerere kwa wajumbe wa halmashauri kuu zilionekana hazina nguvu au ulikuwa ni usanii wa kumkosesha lowassa nafasi ya kugombea urais wa JMT.

Dr Prof Kikwete alikosea sana kumteua Lowassa Ndossy waziri mkuu wa JMT huku akijua alikuwa akienda kinyume na matakwa ya wazee wa CCM ambao tayari walimwonya lakini akawakataliwa na kudai yeye ndio Rais anawajibu wa kuchagua timu yake ya uongozi.Katika kipindi cha miaka miwili alichofanya kazi na Lowassa zilikuwepo taarifa za mitafaruku mikubwa baina yao kashfa ya RICHMOND ilikuwa fursa pekee ya Dr Prof Kikwete kumtema Elowassa Ndossy.

Elowassa Ndossy nje ya mfumo wa serekali alianza kutengenza mtandao wake uliojaa wafanyabiashara,wanasiasa wachafu na mtu yoyote au taasisi yoyote iliyokuwa na ugomvi na serekali ya Dr Prof Kikwete.Kuwataja wachache sana A Chenge,Rostam Aziz,Nazir Karamagi,Ole Medeye, Nabii & Mtume Askofu Mkuu Gwajima..... .Katika mchezo wa siasa si vyema kuishi au kushirikiana na watu wachafu ikiwa una nia ya kushika uongozi wa nchi.

Dr Prof Kikwete katika utawala wake amefanya mengi mazuri na pia ameshindwa kufanya mengi mazuri (mabaya).Amejitahidi kusimamia ujenzi wa barabara sehemu mbali mbali za nchi,amejitahidi kusambaza elimu (shule za kata) maeneo yote ya nchi,amejitahidi katika kusimamia uhuru wa habari ingawa mwisho mwisho amekuja na sheria mbaya.Kuna mambo mengi ya hovyo ambayo serekali yake imeshindwa kuyasimamia ikiwa ni pamoja na wizi wa fedha umma kupitia mikataba mibovu ESCROW,EPA,MEREMETA,RICHMOND............Ifahamike kupitia miradi au mikataba hii nchi imepoteza fedha nyingi sana.Mikataba ya migodi ya dhahabu na sasa mikataba ya gas nayo pia imeshindwa kulisaidia taifa kwakuwa haikuzingatia maslahi mapana ya taifa na badala yake washiriki wa mikataba hii sasa hivi wamekuwa mabilionea huku nchi na wananch wake wakizidi kuzama katika umasikini mkubwa huku rasilimali zake zikinufaisha wachache.


Binafsi natambua uwepo wa UKAWA nawaombea Mungu waendelee kuungana na ikiwezekana watuletee kiongozi atakaye kubalika na wapiga kura wote Tanzania.Nawaombea Mungu UKAWA washinde pia majimbo mengi ya ubunge na ikiwezekana 75% ya bunge lijalo liwe chini ya UKAWA.

Katika ushindani kuna kushinda na kushindwa Pombe Magufuli anaweza kushinda au kushindwa yote mawili yanawezekana katika mazingizira ya sasa.Itategemea UKAWA watafanya nini na CCM watafanya nini.Iwapo Magufuli atashinda kwangu mimi sawa iwapo UKAWA watashinda nitafurahi zaidi.

Kwanini nampongeza Dr Prof Kikwete.Nina sababu moja kubwa nayo ni mgombea wa CCM katika utamaduni tuliouzoea ndie Rais mtarajiwa.Iwapo CCM ingemweka mgombea mchafu kulikuwa na uwezekano wa kumpata rais mchafu (Edward Ngoyai Ndossy).Hapa nachukulia sifa za wapiga kura Tanzania ukiwa na fedha ni rahisi sana kuwanunua.Tumeona wajumbe wa kamati kuu,halmashauri kuu walivyonunuliwa,tena hawa wengi wana uelewa mkubwa wa masuala mengi,wana uwezo wa fedha (hali na mali) sembuse wananchi wa vijijini wasiokuwa na uhakika wa milo mitatu kwa siku !,Nadhani hawa ingekuwa kazi rahisi sana kuwanunua kwa gharama ndogo sana.

Nampongeza Dr Prof Kikwete kwa kuhakikisha bingwa wa kununua uongozi Tanzania na kusini mwa jangwa la Sahara pamoja na fedha zake Bwana Edward Ngoyai Elowassa Ndossy ameangukia pua.Natambua Dr Prof Kikwete amefanya makosa mengi kwa taifa lake kama kiongozi lakini hili la kumchinja fisadi mkuu limefuta dhambi/makosa yake yote na ana uhakika wa kuona ufalme wa mbinguni kwa muijibu wa dini yake na kitabu chake kama ikiwa ni kukutana na wale mabikira 72 sawa au ikiwa kuna ahadi nyingine kubwa zaidi ya wale mabikira 72 sawa zote zina msubiri amelitendea vyema taifa lake.

Naomba kuwasilisha.

attachment.php


Urafiki baina ya Elowassa na Kikwete umeanza mbali "hawakukutana barabarani"
 
Prof Ngongo nasoma hii bayana yako na kuifuatilia kwa karibu mno tarudi baadae kuchangia kiduchu.

Regards

Ritz
 
Last edited by a moderator:
Mtu pekee anayeweza kuongeza kura nyingu kwa mkupuo na kusumbua CCM ni ZZK ndani ya UKAWA achukue kiti cha mwenyekiti wa chadema..hiyo itampa nguvu sana mgombea atakayeteuliwa na UKAWA.
 
Umemsamehe wewe na mafisadi wenzako mnafaidi rasilimali za wavuja jasho wa tanganyika.
 
Ndugu Mmawia soma tena na tena bandiko langu labda haujanielewa si makosa yako hili ni tatizo kubwa sana katika jamii ya kitanzania mtu unaweza kujibu kitu ilihali swali hujalielewa.

Umemsamehe wewe na mafisadi wenzako mnafaidi rasilimali za wavuja jasho wa tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Mtu pekee anayeweza kuongeza kura nyingu kwa mkupuo na kusumbua CCM ni ZZK ndani ya UKAWA achukue kiti cha mwenyekiti wa chadema..hiyo itampa nguvu sana mgombea atakayeteuliwa na UKAWA.

Zzk kakataliwa kwao mwandiga ndio umkaribishe kwenye kundi la viongozi wasafi kama ukawa?
 
Ndugu Mmawia soma tena na tena bandiko langu labda haujanielewa si makosa yako hili ni tatizo kubwa sana katika jamii ya kitanzania mtu unaweza kujibu kitu ilihali swali hujalielewa.

Asante sana mkuu ngongo,narudia kusoma bandiko lako kwa ruksa yako!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu RockSpider nimesoma bayana zako nitarejea kuzijadili moja moja lakini kubwa zaidi tuelewe hatuchagui malaika bali wanadamu ambao si wakamilifu.

Ahsante kwa mchango wako mengi nilikuwa siyajui lakni bado hajamfikia Edward Ngoyai Elowassa Ndossy.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu RockSpider naanza na number # 11.

Naona kama tuhuma imekaa kimajungu majungu.Umeshindwa kusema alianza kumshughulikia vipi eg aliuza nyumba yake,alimwiba mke wake,alimfilisi mali zake na nk.Umesema alianza kumshughulikia lakini namna alivyomshughulia umeshindwa kusema ni wazi haya ni majungu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom