Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

KAZI TU Chakaza Rafikiangu upoooo
Nipo ndugu yangu MOTOCHINI na hongera kwa mtu wako kutangazwa mshindi (sisemi kushinda). Yote sawa tuu na maisha yatasonga kwa slogan hiyo ya Hapakazituu.
ila uchaguzi huu ulikuwa na mambo ambayo huwezi kuamini hasa katika majumuisho ya kura. Kuna mambo mie nilishika mdomo sikuamini kuwa yanaweza kutokea. Mie nilidhani ni huu ushabiki wetu tuu wa ki JF kumbe kuna mambo makubwa mno. Wewe ni pm nikujulishe maana siwezi kuyaandika humu, ni mazito.
 
Last edited by a moderator:
Hakika kilichofanyika Zanzibar na Tanganyika ni "Mapinduzi" ya Maamuzi sahihi ya Wananchi..Naam,Maamuzi mujarab ya Watanzania yamepinduliwa tena kwa kile kinachotafsiriwa kuwa ni demokrasia ilihali ni ubakwaji mkubwa wa HAKI kwa kupiga mikwara vyombo vya habari,kuvamia Kituo cha Haki za Binadamu,Kuwapora Wapinzani vifaa vya kukusanya takwimu na kukataa Maamuzi sahihi ya Wananchi katika sanduku la kura!!!Dhambi hii haitoishia hapa,tumepanda mbegu hatari ya kutufarakanisha,yumkini isiwe leo..Ila siku itakapofika ukimya huu wa Walioporwa haki utageuka kuwa uchungu mkubwa sana ambao haujawahi kutokea!!!..Najaribu kutafakari kwa sauti!!!
 
Tatizo mnaleta hoja zilizokufa.

Wenzenu wanaangalia ni namna gani JPM ataunda serikali itakayosaidia kutatua kero za wananchi.
Yaani unawaza namna ambavyo JPM ataunda serikali? Mbona liko wazi kabisa kwamba ataunda kwa kuteua waziri mkuu na mawaziri kutokana na wabunge wa chama chake waliopo? Huo si ndio utaratibu wa siku zote wa kuunda serikali? Hilo nalo ni la kuwaza?
 
Kwa mara ya kwanza kabisa Tanzania, tumeshuhudia mioyo ya Wanzania wengi ikiinama na kuhuzunika sana, Lakini ni kwa mara nyingine tena Mungu akijibu maombi ya Watanzinia, Kwani tuliomba Amani,na Mungu akatupa Amani, Lakini tulisahau kumuomba Mungu HAKI itendeke Tanzania. Tuliona na kusikia watu na watumishi wa Mungu wakisema waliyoonyeshwa na Mungu kuhusu uchaguzi na waliyoonyeshwa yalikua machafuko, wengine wakamtaja Mbowe ili aombewe na watu walifanya hivyo na Mungu akatusikia maombi yetu na kutupa Amani. Tunapaswa Kufanya haya
(1) Watu wote kwa imani zetu tumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yetu ya kutupa Amani na tutoe sadaka ya shukurani.
(2) Watu wote kwa Imani zetu Tumuombe MUNGU atupe HAKI yetu kwa Amani kwani haki huinua Taifa na MUNGU atatupa HAKI hiyo haraka, kumbuka kilio cha wana wa iziraeli MUNGU alikisikia na akawaokoa kutoka kwa farao kwa mkono wake wenye nguvu, farao alikua na majeshi, bunduki na magari ya deraya,wana wa Iziraeli walikua hawana chochote mikononi mwao,wala hakuanzisha vita wala maandamano, lakini haikuzuiya Mungu kuwapa haki yao ya kua huru, Aberinego na wenzake MUNGU aliwapa haki yao kwa kuwakomboa kutoka kwa mfalme nebkadreza, na watanzania hawana majeshi, bunduki wala magari ya deraya bali kwa maombi yetu MUNGU atatupa haki yetu kwa amani. Mungu hachelewi wala hawahi bali siku zote ni Mtimilifu na mkamilifu
(3) Kwa Sababu sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU na kwa sababu aiyepata kura nyingi ndio chaguo la Mungu je Mungu hatasimama na kujichukkulia utukufu wake mwenyewe, je Mungu hatasikia maombi ya watanzania na kuwapa HAKI yao ili nchi yao inuke? je MUNGU atamwacha shetani achukue utukufu wake mbele ya watu wake?
(4) Tuwashirikishe watumishi wa MUNGU, marafiki, waombaji ndani na nje kwa MAOMBI ya Tanzania na watanzania Kupata HAKI Yao ili nchi yetu iinuke, tukiacha kumwambia Mungu mioyo ya Watu wengi ikaendelea kuinama, nchi nayo inainama na hatutakua na maendeleo, kumbukwa furaha ya watanzania iliyokua kipindi cha serekali ya awamu ya pili, baada ya uchaguzi wa mwaka 1995, Watanzania mioyo yao ilinama na mpaka sasa mioyo yao hakuinuka, na nchi ilinama na mpaka sasa haijainuka kwani kila siku watu hawana furaha ni malalamiko tu, uchumumi hauendi mbele, serekali haiwezi kutusaidia, bali Mungu anaweza yote. Tuingie kwenye Maombi ya watanzania kupata HAKI yao iliyopokwa na Shetani na tutaona mkono wa Mungu ukitoa HAKI ya Watanzania, Amen.
 
Hebu tufanye prediction kidogo ya mambo yatakayoongewa au kugusiwa sana sana na rais wetu mteule siku atakapokua anaapishwa au kufungua bunge au sehemu yoyote kama speech yake ya kwanza kama rais..,,
 
Hebu tufanye prediction kidogo ya mambo yatakayoongewa au kugusiwa sana sana na rais wetu mteule siku atakapokua anaapishwa au kufungua bunge au sehemu yoyote kama speech yake ya kwanza kama rais..,,

Wewe bhana hiyo Id yako mimi naiogopa usije ukamdhuru rais wetu.
 
Nipo ndugu yangu MOTOCHINI na hongera kwa mtu wako kutangazwa mshindi (sisemi kushinda). Yote sawa tuu na maisha yatasonga kwa slogan hiyo ya Hapakazituu.ila uchaguzi huu ulikuwa na mambo ambayo huwezi kuamini hasa katika majumuisho ya kura. Kuna mambo mie nilishika mdomo sikuamini kuwa yanaweza kutokea. Mie nilidhani ni huu ushabiki wetu tuu wa ki JF kumbe kuna mambo makubwa mno. Wewe ni pm nikujulishe maana siwezi kuyaandika humu, ni mazito.
Hahahaha Chakaza nduguyangu hapakuwa na jinsi, vyovyote kubwa kununua ikulu ishindikane lowassa hana hata chembe ya kuingia ikulu tuyaache niwakati wa kufanya kazi sasa
 
Last edited by a moderator:
Sasa kulalamika kwako mitandaoni kunakusaidia nn? Walio wenngi wameamua!
Wezi wa kura ndio walioamua, sio walio wengi. Unaniuliza kulalamika kwangu mtandaoni kunanisaidia nini, kwani wewe kunijibu mtandaoni kumekusaidia nini?
 
Mimi huku niliko ni shangwe tu...

Watu wanaimba 'Lowassa.....Tumemkataa'
Lazima utakuwa Mirembe Dodoma....

Pamoja na maneno yako pita pita ako kwa sasa utakuwa ushakiri maneno yangu....


''Bala Always in Dodoma''

Raisi wa CCM muhahahahahaha
 
Hapo hawajaiba wangeiba hata hzo m6 asingezifikisha bubu wenu, unaenda tongoza huna maneno ya kuvutia unategemea nn? Hahaa Lowasa dhoofu "mbowe 2015
 
Hii awamu ya urais ambayo Magufuli ndiye Rais wake ina maswali mengi ya kujiuliza.Kwamba ni ya tano sio tatizo sana.Tatizo labda ni huyo mtu anayeongoza kwa kuwa anaapishwa tarehe 5,namba ambayo inajirudia.Awamu ya 5 inayoapishwa taehe 5.(?) Cha kushangaza zaidi awamu hiyo inaapishwa tarehe 11 ambaye ni "signature" ya Freemason(wanaojua wanajua).Tena anaapishwa akiwa na umri wa miaka 56(5+6=11).Namba 11 inajitokeza tena.Lakini ukiangalia umri wake utagundua pia kwamba kuna namba 5 na 6.Namba hizi ni muhimu sana kwa Freemason(Wanaojua wanajua).Pia symbol ya campaign yake ina maswali mengi.Nayo ni symbol ya Freemason(mkono ulioshika mwenge katikati ya M).

Swali la kujiuliza ni kwamba hii, ni coincidence au JPM anajua kinacho endelea?
Dr. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya 5 baada ya kuongoza kwa kupata kura 58.46%.

attachment.php


Lubuva: Kwa kuwa mheshimiwa Dr. Magufuli, John Pombe Joseph wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35(e), 35(f) na 81(b) vya sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343.

Ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi ya urais wa mwaka 2015 kwamba

  1. Mheshimiwa Magufuli John Pombe Joseph amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
  2. Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Asanteni kwa kunisikiliza.



 
Last edited by a moderator:
Majizi makubwa haya.....Mungu ayalaani !

Hivi unajisikiaje, hasa pale unapogundua kiuhalisia kuwa mkeo au mmeo hakukubali, hakupendi, ila basi afanyeje hawezi kuondoka maana umemuwekea walinzi wa kumzuia asiondoke kwako.
Kwa hali kama hiyo unapotoka na kurudi hapo kwenu; unafurahi kumkuta yupo? Au je yeye anafurahi kukuona umerudi kwake?

Nikijielekeza kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika sasa; fikara yenye kufanana na mfano huo halo juu ilipita akilini mwangu.
Kuwa ccm hii yenyewe inajua fika kama haikuwalazimisha watanzania kuendelea kuwa nayo! Kama vile watanzania walio wengi wanavyojua ndani ya nafsi zao mapenzi yao kwa chama tawala kwamba ni ya hiyari au ni ya lazima!

Aghalabu ni vyepesi kama nini kuwadanganya watu wengine kuliko kufanya hivyo kwa nafsi yako mwenyewe.
Ndiyo maana baada ya uchaguzi huu unaweza kukuta mtu anashangilia nje lakini kwa ndani nafsi yake inamkanya ikisema muongo wee!

Mungu ni shahidi mwaminifu amina!

Tunataka viwanda, dawa, elimu bure mpaka form 4 though elimu mpaka hapo... maji yawe historia kama alivyoahidi.

Kwani wewe hukujua kwamba kupiga kura bila katiba huru ni kupoteza muda.Usirudie kosa hilo tena.


ni jf wamekosea au ni nec na calculator zaooooo?????
mimi ni mwana ccm ila sipendi unafiki nimekunywa pombe hapa lakini hizi data.........


""Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 23, 161, 440, waliopiga kura ni 15, 589, 639 sawa na asilimia 67.31 ya wapiga kura wote waliojiandikisha.

Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni kura halali 15, 193, 862 sawa 97.46% kura zilizokataliwa 402, 248 sawa 2.58% hivyo Magufuli amepata kura ambazo ni 8, 882, 935 sawa na 58.46% ya kura zote halali.

Matokeo ya wagombea wengine akiwemo, Anna Mghwira wa (ACT-Wazalendo) 98,763 sawa 0.65%, Chifu Lutalosa Yemba (ADC), 66, 049 sawa na 0.435 huku Edward Lowassa (Chadema) akimfuatia kwa kura Dk. Magufuli kwa kupata kura 6, 772, 848, sawa 39.97% na Hashim Rungwe wa (CHAUMMA) aliyepata kura 49, 256, sawa na 0.32%.

Wagombea akiwemo Janken Kasambala (NRA) 8, 028 sawa 0.03% na Maximilian Lyimo (TLP) 8, 198 sawa na 0.05% Fahmy Dovutwa (UPDP), 7, 785 sawa 0.05%.""

Ukanda Upi wewe takataka? Ina maana Kanda ya Kaskazini Pekee ina wapiga kura asilimia 42?

Ni wachache wanaothubutu kumpongeza JPM.... nahisi ni kati ya marais watakoukuwa na kazi ngumu sana

Kwanza kwa sababu hajachaguliwa na walio wengi,

Pili anaikuta serikali ikiwa katika hali mbaya kuliko alivyoikuta mkapa,

Tatu itamchukua miaka zaidi ya minne watu kumkubali... maana mpaka sasa hana kibali, watu bado wana rais wao mioyoni!!!!

Nne anaikuta CCM ikiwa vipande kukiwa na wasaliti wengi....

Tano anakutana na watanzania waliokata tamaa na maisha hawana hamu na lifisieM lao...

Ongezea mengine

kama mtu anakataa kupata elimu unategema nini hapo???,

1. Watu hao waliokataa elimu ya bure hawana hata uwezo wa kupata milo 3 kwa siku
2. ....................hawana hata nyumba ya tofali
3. ............................................wanakufa kwa kukosa panadol
4............................................hawana hata viatu vya kutembelea jambo ndala za tsh 1000
5.........................................wanakunywa maji machafu anayokunywa punda (mifugo)
6. ......................................................................................
7. ...................................................................
,...............................................................

Umaskini wa mwili na akili ndio mtaji wa ccm, ccm itatawala milele;

Shule zao zipo maporini wanakakia mawe ndio wanaoongoza kwa kutoa mashamba boy na mabeki tatu!

Upo sahihi kabisa ila hawa Ukiwa wameng'ang'ania 6, 772, 848

Tumieni akili nyie vilaza, hesabu yakura za JPM Ni pamoja na zile zilizokamatwa ndani ya gari zikiwa zishampa ushindi diwani, Mbunge na rais.
Hiyo Ni strategy ya ccm kuendelea kukomba mali zanchi na gesi ndo inawafanya wawekezaji uchwara kudodoka udenda. Na ndani ccm tayari Kuna syndicate ambayo inapora mali za nchi kila kukicha.
 
Hivi Janeth Magufuli ni mzaliwa wa wapi? Nime-Google John Magufuli historia ya mmewe haielezi much (if any) about her or the family in general. Najua ni mwalimu lakini nilitegemea Wikipedia ingekuwa na more information. It's for my own understanding -no shade.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom