Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Nilisema Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kumbe wapiga kura wengi walikuwa na fikra na mtazamo kama wangu.

Hizi hoja za kusema idadi ya kura imekosewa au kura zimeibiwa ni hoja za kufurahisha kijiwe cha Jamiiforums.

Watu wenye fikra na mitazamo pevu wameishakubali kama Magufuli ni Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano pamoja na kwamba fikra na mitazamo yao ilikuwa tofauti kabla ya kupiga kura.

Get used to a new reality, Dude!
 
Kuna ndugu yetu ambaye hana kazi na kila siku anahamahama mara leo kwangu, kesho kwa kaka yangu. Lakini ukiangalia matatizo yake yanayotatuliwa na sisi ghafla akawa mshabiki mkubwa wa CCM kwenye kampeni. Kuchunguza tukagundua kuwa amepewa kofia, fulana na CCM.

Pia kuna mwingine yeye ni mwalimu kila akipata tatizo la kukopa anakuja kwangu. Nikazoea kwamba kila ikifika Novemba lazima anikope kwa sababu ya kulipia watoto wake shule January. Ghafla na yeye wakati wa kampeni hadi tukakorofishana kwa sababu ya mimi kushabikia hoja za UKAWA na yeye za CCM. NIkagundua kwamba kumbe amepata khanga, na kofia na ghafla wakati wa kampeni amekuwa na hela. Hanikopi tena na hata simu hanipigii wakati Novemba imekaribia tena kama alivyozoea.

Mtaani kwetu kuna majirani ambao ni mama lishe na sisi ndiyo wanunuzi wao. Pamoja na umama lishe wao bado wakipata shida wanakuja ama kukopa kwangu au kwa yeyote. Sasa nimetembelea vituo vyote vya jirani nikaona CHADEMA ndiyo iliongoza kwa asilimia kubwa. Maana yake wateja wa hawa mama lishe na sisi ni wapenzi wa hoja za UKAWA. Lakini kwenye kampeni nikaona ameweka bango kuba la Magufuli na amekuwa na majibu yasiyo ya kawaida. Sasa leo Magufuli katangazwa ananipigia simu kuwa tujenge Tanzania moja kwa mimi kuendelea kununua chakula kwake! Hapo bao hela aliyopewa kwenye kampeni haijaisha. Inawezekana saasa amepata akili kwamba bado ataendelea kuishi na sisi wana-CHADEMA wakati waliompa hela wako Ikulu au kwenye Wizara.

Kuna muuza mgahawa linikataza kabisa nisikanyage cafe yake kwa sababu ninaleta mambo ya UKAWA kwa sababu cafe yake pale Mbezi Mwisho iko karibu na ofisi ya CCM.

Kuna jamaa mmoja naye alinipiga marufuku nisikanyage baa yake kwa sababu ninaleta mambo ya UKAWA. Na mimi sikuona taabu na tangu siku hiyo ninaenda Supermrket ya NAKUMATT nanunua beer na wine caton nzima nakunywa kwa wiki na nimeshaachana naye.

Ninachotaka kusema ni kwamba, uchaguzi huu umeleta makovu ya namna hii. Mtu ananikataza nisiingize hela kwenye biashara yake kwa sababu kanisikia nikiisifia UKAWA lakini aliwaruhusu kusifia CCM.

Sasa uchaguzi umekwisha. naamimi hali hii imetokea kwingi. Kuipenda UKAWA ilikuwa ni mapenzi yangu kwa sababu sikuona CCM inachoweza kunisaidia. Sasa, kama ulikataa huduma au hela yangu wakati wa kampeni sitarajii uje na visingizo kwamba uitake hela yangu wakati huu.

Yule ndugu yetu anayehamahama leo kwangu kesho kwa kaka, ndiyo ameshatumika kama toilet paper. Waliomtumia labda wamkumbuke Septemba 2020. Sasa anabaki na sisi. Na mimi msimamo wangu ni kwamba alipata ndugu wapya wakati wa kampeni tuone sasa wanavyokidhi haja zake ambazo sisi tumezijua miaka nenda rudi.

YUle mwingine wa kukopa hatanikopa Novemba hii, ana hela alizopewa wakati wa kampeni. Sijui utanieleza vipi kuanza tena kusikiliza hoja zako. Yule mwenye baa aliyenifukuza, jioni nimeona anatoa smiling face kana kwamba si aliyenifukuza majuzi. Yule mama lishe kanipigia mwenye simu, kaishaondoa mabango ya Magufuli na sasa anataka kurudi tena kwa sisi wateja wake na si wateja wateja wale aliowapata zilipoanza kampeni.

Tusipotoa fundisho kwa watu kama hawa nchi haitabadilika. Mimi msimamo wangu ni kwamba unaponikana bila sababu za msingi, halafu kesho waliokurubini wakiondoka unanirudia basi ni bora uangamia ii kutoa fundisho kwa wengine.


Kuipenda CCM ni haki yako. lakini kutuzuia tusinunue bidhaa yako kwa sababu unaogopa wana_CCM wenzako, basi ni bora uendelee kuwaogopa milele na wabadilike wawe wateja wako au wawe ndugu zako.

Bahati nzuri kampeni imetufunulia jambo moja. Maduka yaliyokuwa na bendera za CCM au CHADEMA yanajulikana. Hivyo, sasa hivi si kama zamani ukikosa duka au huduma inaoyeodeshwa na mpinzani basi huna la kufanya.

Nilichogundua baa, maduka, biashara, bodaboda, daladala vinavyendeshwa na wapinzani ni vingi kuliko maelezo. Kama mtu alitangaza vita ya kutokubali wateja kwa mujibu wa upenzi wa chama chake, basi tuendelee na vita ya namna hiyo tuone ni nani atashindwa.

Maana huko hakuna uchakachuaji. Kama itafikia hali kwamba biashara za CHADEMA na CCM ziwekwe mbalimbali na bora iwe iwe hivyo maana sasa hivi tuko sawa kwa sawa. Ni wazi baadhi ya mduka yatafungwa.

Mtaani kwetu mama mmoja wa CCM namhurumia. Kafungua duka na ndipo kuna ofisi za CCM. lakini ninauona uhasama wa namna hiyo waziwazi mtu anaenda kununua kwa duka la UKAWA wanamuacha na ndani ya miezi miwili naamini atafunga biashara.

Haya ndiyo matokeo tuyatarajie, ni matokeo ambayo huwezi kuyadhibiti kwa kuitisha defender ya polisi au gari ya washawasha.

Mimi naona ni bor aiwe hivyo na iwe fundisho huko mbeleni tuwe wastaarabu. kwa sababu chama kinakufuata wakati wa kampeni tu. Kampeni zikiisha sisi ndiyo tunabak ndugu zako, sisi ndiyo tunabaki wanywa beer zako na wine zako, sisi ndiyo tunabaki wateja wako.
 
Nilisema Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kumbe wapiga kura wengi walikuwa na fikra na mtazamo kama wangu.

Hizi hoja za kusema idadi ya kura imekosewa au kura zimeibiwa ni hoja za kufurahisha kijiwe cha Jamiiforums.

Watu wenye fikra na mitazamo pevu wameishakubali kama Magufuli ni Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano pamoja na kwamba fikra na mitazamo yao ilikuwa tofauti kabla ya kupiga kura.

Get used to a new reality, Dude!

Na hiyo pia huioni mkuu duh
 
Nilisema Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kumbe wapiga kura wengi walikuwa na fikra na mtazamo kama wangu.

Hizi hoja za kusema idadi ya kura imekosewa au kura zimeibiwa ni hoja za kufurahisha kijiwe cha Jamiiforums.

Watu wenye fikra na mitazamo pevu wameishakubali kama Magufuli ni Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano pamoja na kwamba fikra na mitazamo yao ilikuwa tofauti kabla ya kupiga kura.

Get used to a new reality, Dude!

Na hiyo pia huioni mkuu duh hapa ni elimu elimu elimu basi.
 
Nilisema Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kumbe wapiga kura wengi walikuwa na fikra na mtazamo kama wangu.

Hizi hoja za kusema idadi ya kura imekosewa au kura zimeibiwa ni hoja za kufurahisha kijiwe cha Jamiiforums.

Watu wenye fikra na mitazamo pevu wameishakubali kama Magufuli ni Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano pamoja na kwamba fikra na mitazamo yao ilikuwa tofauti kabla ya kupiga kura.

Get used to a new reality, Dude!
Mbona sijaona mstari uliojibu hoja?
 
hiyo ndio imefanya kisiwa cha Pemba hakuna kiti cha CCM hata kimoja . UKIJIONA WEWE NI SEHEMU YA WATAWALA WAKATI LOFA ukimaliza uchaguzi UNAKABILIANA na WATAWALIWA.
 
Amani ya Mungu iwe nawe raisi wangu mteule mpendwa,

Kwanza napenda kukupongeza kwa moyo wangu mmoja kwa sababu wewe ndo naamini ni mtu unayeifaa Tanzania. Niliwai kuandika humu kwenye thread zilizotangulia kuwa Tanzania inayosumbuliwa na kiwango kikubwa cha wananchi wasiopenda kufanya kazi, wapenda dili na wizi, wapenda maneno matupu na wasiopenda kufanya kazi kwa ufasaha inaitaji mtu mkali ambaye niliwai kusema dikteta mzalendo. Tangu uchukuaji wa fomu CCM ulipoanza mie niliwaunga mkono wewe na Prof Muhongo kwa sababu niliamini nyie ndo watu mnaokidhi hiki kigezo cha dikteta mzalendo ambaye atakuwa mkali na kuwageuza wananchi kuwa wafanya kazi na sio wapenda vya bure, ambae atasababisha utumishi wa umma kuwa utumishi kweli na si vinginevyo.

Kwa wewe kuchaguliwa na watanzania kusema kweli Nimemshukuru Mungu na nasema jina la bwana lihimidiwe.
Nikiwa nakufananisha sana na watu kama Paol Kagame, Meles Zenawi(marehemu waziri mkuu wa ethiopia ambaye hadi duia imemuheshimu kwa jinsi alivyoitransform Ethiopia kiuchumi) naamini kwa moyo mmoja kuwa sasa Tanzania ipo kwenye mikono salama na stahiki.

Raisi wangu mteule umeona mwenyewe mgsawanyiko wa kura ulizopata ulivo, umeona maeneo yaliyokupigia kura kwa wingi na kuna watu wamekuwa wanakebehi eti umepigiwa kura na masikini na watu wasio na maendeleo ivyo basi nakuomba kwa uongozi wako ufanye yafuatayo.

1. Kwanza ufanye reshuffle kubwa sana serikalini hasa kwa wale watu ambao obvious una uhakika watakuangusha. Najua washauri wako watakuelezea vizuri katika hili. Hii ni kwa sababu kuna watu waliside kabisa na upande mwingine na hawakutaka wewqe uingie sasa kwa usalama wa serikali yako naomba uanze na hii reshuffle ya hawa watu.

2. Pamoja na jitihada zako za kubana matumizi ya serikali naomba kweli uyabane muheshimiwa na uwe na target kabisa ya kusave kiasi fulani cha fedha ambacho utakielekeza sehemu fulani.

3. Kwenye kuboresha mishahara ya wafanyakazio naomba uanze na waalimu na madaktari kwa sababu haya ndo makundi yanayokutana na watu wa hali ya chini karibu siku zote za maisha ya wananchi wa nchi yako, waalimu wakiwa na maslahi mazuri obvious hawatawalisha sumu na matango wanafunzi kuichukia serikali, pia watafundisha kwa morali hadi wazazi wao watafurahi na kuipenda serikali yako. Pia madaktari nao watafanyas kazi kwa hali na watatoa huduma nzuri na wananchi watafurahia na kuisupport serikali yako.

3. Naomba uwekeze zaidi kwenye miradi ya maji na umeme kwa sababu hivi ni vilio vikubwa sana vinavochangia watu kuichukia serikali. wekeza kwenye mega projects za maji na umeme ambazo zitaelekezwa kwenye maeneo yenye watu wengi. Hili litakubeba sana.

4. Naomba kwenye ahadi zako priority hasa kwenye hospitali,madawa na mikopo uanze kwa maeneo ambayo yanasemwa kuwa watapata shida pamoja na kukupigia kura nyingi. Nasisitiza kwenye hili kwa sababu asikwambie mtu raisi wangu hawa watu walikuchagua kwa sababu waliamini katika wewe na ili wasiwe na moyo uliosinyaa naomba kwenye miradi yako utekelezaji wake uanzie kwenye mikoa hii ili wakisemwa vibaya waseme tulimchagua na hatujajuta kumchagua. Then ukitoka huko ndo uende na kwingine kule ambapo walikupa kura chache na hawakuiamini CCM.

5. Naomba uboreshe na urekebishe utendaji serikalini hasa masikini na mtu wa kawaida aone kuwa kweli utendaji,uwajibikaji na huduma za serikali zimebadirika. Usilee wazembe,walarushwa na waonevu bali wape nafasi wachapa kazi.

6. Tilia maanani sana mfumo wa ukasanyaji kodi na uhakikishe mamlaka ya kodi inakuwa na watumishi wenye weredi na maadili na ambao hawaendekezi rushwa. Hapa kuwa mkali sana ikiwezekana kuunda mfumo wa kufuatilia mali na fedha za wafanyakazi wa mamlaka ya kodi kwa sababu kusema kweli hili ni sehemu mabayo imekuwa ikiirudisha sana nchi yetu.

Raisi wangu mteule haya ni mambo 6 niliyokuandikia na naomba uyatilie maanani sana na nakuamini kwa uwezo wako huwezi kushindwa.

MUNGU AKUBARIKI RAISI WANGU NA AKUPE UJASIRI, NGUVU, HEKIMA NA UTHUBUTU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Niungane na wewe kumpongeza Dr Magufuli kwa Watanzania kumuamini kuongoza usukani kuliongeza Taifa letu. Nimekua nikimkubali Dr Magufuli sana, ila niseme waz nmekua sikubaliani na mienendo ya chama CCM.

Nikichangia ushauri uliompa,nitajikita kwenye item ya kwanza, nayo ni Reshuffle Serikalini na Overhaul, Reshuffle ndani ya CCM. Lakini kwa kuwa reshuffle ndani ya CCM haina umuhimu sana kwa Watanzania wote(maana wengi hawana vyama), basi tumsihi afanye mabadiliko makubwa katika taasis zote za serikali, na ateu watu kwa fani husika,tena aanze upya kabisa. Viongozi wote waandamizi wapaswa kubadilishwa au kuhamishwa ili kuondoa kufanyakaz kwa mazoea! Viongozi wakubwa wa Mashirika ya Umma,Wakala za Serikali,Wizara, Wakuu wa Idara,Mifuko ya Jamii,Makatibu lazima aangalie upya, ili kuongeza tija na uwajibikaji.

Kuna tatizo kubwa sana la uendeshaji katika Halmashauri zetu. Miradi mingi inafanyika ndivyo sivyo, siasa ni nyingi kuliko kuheshimu taaluma. Chukulia mfano barabara zinazosimamiwa na Halmashauri zimeonyesha kuwa chini ya kiwango kwanza ni kutokana na bajeti ndogo, uadilifu, uhaba wa wataalam, muingiliano wa wanasiasa(madiwani nk).

Lakini kitu kingine ni kupunguza Wizara.Ukubwa wa Baraza la Mawaziri na Wizara kwa ujumla ni jambo muhimu sana kwa sasa.Kuna Wizara zingine zilizopo sasa zingefaa kuwa ni Idara tu. Nitatoa mifano:Wizara ya Afrika Mashariki inastahili kuwa ni Idara tu ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje.
Wizara ya Elimu inaweza kuchukua Michezo na Utamaduni huku vijana wakienda Ajira na Kazi na Utumishi hapo Wizara ya Michezo na habari inajifuta. Wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu inarudi kama enzi za Mkapa. Wizara ya Ujenzi inakua kubwa ikiwa na Uchukuz huku Idara zikiboreshwa au kuwe na Wakala ya Uchukuz ndani ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi!
 
hizi ndo tunaita AKILI PUMBAVU una pika matokeo na kuyaleta kwa ufahamu au kwa kutokufahamu na bado unapata wafuasi wenye akili PUMBAVU kama zako

kasome upya kura za eddo

ndo maana mnaitwa nyumbu ni kutokana na kuwa na AKILI PUMBAVU badae ufatilie unalopoka
 
Hii hesabu nadhani alipiga polepole make hata hizo kura halisi na zilizokataliwa ukijumlisha haileti hesabu iliyotajwa.
 
Utata kuhusu!!
1.Tume kabla ya uchaguzi idadi rasmi ya wapiga kura 22.7M

2. Jk pale dodoma 28M

3. Leo wakati wa kutangaza matokeo 23.1M
 
Kwanza nachukua fursa hii kukupongeza kwa ushindi ulioupta maana umepita katika chujio kali na mapito magumu ila sala na maombi yamekuongoza maana Allah katuamrisha tumwombe msaada wake pale ambapo tunaona tuko katika kipindi kigumu na hata cha hatari pia ili atupe ushindi au atunusuru na mabalaa ya wanadamu na mashetani (majini). Ni imani yangu nawe ulifanya maombi na Allah amekulinda kisha kukupa ushindi dhidi ya washidani wako.
Ushauri wangu kwako
1) Dumu katika kumwomba allah/mungu ili akuongoze na pia azidi kukulinda dhidi ya maadui maana nasi tutazidi kukuombea ili Allah akuongoze kutenda haki na kukulinda kwa ajili ya kulinda amani, mshikamano wetu na upendo!
2) Chama kinaonekana kuwa kimeanza kumomonyoka kimaadili, umoja na mshikamano ni vyema kukisuka upya ili kuondoa mgawanyiko ulivyoonekana katika kumtafuta mgombea ili kuwa kitu kimoja maana wananchi bado wana imani na chama kilichokusimamisha kugombea ni bora kukijenga upya mara utakapokabidhiwa jukumu la kukiongoza.
3) Kwa upande wa watumishi umma/serikalini nako bado kuna mgawanyiko kutokana na wanasiasa kujali maslahi yao (Mfano Profesa na Dr. wanaacha kufundisha vyuoni kutokana na maslahi/pensheni ndogo na kazi ngumu) zaidi huku wakisahau watumishi wa umma/serikali. Hivyo kuna watumishi wa umma/serikali wanaolalamika kusahaulika ama haki zao (Mishahara midogo na pia mafao madogo) kupuuzwa na mfumo uliopo na pia kuna wengine wanaonufaika zaidi na mfumo uliopo kuliko wengine hali wote ni watumishi wa umma!! Mfano ni utofauti uliopo katika mishahara kati ya mashirika umma na serikali kuu au serikali za mitaa. Ni bora pakaangaliwa upya ili kupunguza utofauti huo ili kuondoa malalamiko yaliyopo na kuwapa morari waliokata tamaa au kuona kuwa wao daima hawana pa kusemea!!
4) Ni vyema ukapanga ratiba binafsi za kushtukiza katika tasisi za umma/serikali ili kujionea utendaji wa watumishi wa umma uliopo ili kujua mizizi na matatizo katika mashirika ya umma/serikali ili kuondoa kero zilizowakabili wananchi muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na hivyo wewe kuwa ni mwenye kujionea jinsi wananchi wako wanavyopata huduma nzuri/mbovu kutoka katika tasisi za umma ili kurudisha matumaini ya wananchi katika chama chako na serikali kwa ujumla na aliyefanya vyema apongezwe na aliyetenda kinyume hatua stahiki zichukuliwe ili kuleta nidhamu ya utumishi wa umma na kuondoa dhana ya kulindana!
5) Taaluma mbalimbali zimeanza kuaangamia maana wanasiasa sasa wanafanya kazi za kitalaamu ama kulazimisha vitu vya kitalaamu kufanywa kisiasa ili tu kuridhisha wapiga kura na hivyo kusababisha migogoro kati ya wanasiasa na watalaamu bora taaluma zikapewa haki yake na hivyo kuleta tija na kutoka hapa tulipo!!
Yangu ni hayo tu nikuombee Allah akulinde, akuongoze na akujalie kila la kheri katika kazi yako mpya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom