Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,002
Dr. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya 5 baada ya kuongoza kwa kupata kura 58.46%.

attachment.php


Lubuva: Kwa kuwa mheshimiwa Dr. Magufuli, John Pombe Joseph wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35(e), 35(f) na 81(b) vya sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343.

Ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi ya urais wa mwaka 2015 kwamba

  1. Mheshimiwa Magufuli John Pombe Joseph amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
  2. Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Asanteni kwa kunisikiliza.



Matokeo ya Urais: DK. Magufuli atangazwa mshindi kwa asilimia 58.46

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2015 kuwa ni Ndugu John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).

Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yametangazwa leo ambapo mwenyekiti huyo amemtangaza Dk. Magufuli kama rais wa Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu, Lubuva alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.

Aidha Lubuva, amesema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basi na mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.

?Kwa kuwa Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2015.

?Mheshimiwa Mheshimiwa John Pombe amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,? alikaririwa na FikraPevu mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 23, 161, 440, waliopiga kura ni 15, 589, 639 sawa na asilimia 67.31 ya wapiga kura wote waliojiandikisha.

Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni kura halali 15, 193, 862 sawa 97.46% kura zilizokataliwa 402, 248 sawa 2.58% hivyo Magufuli amepata kura ambazo ni 8, 882, 935 sawa na 58.46% ya kura zote halali.

Matokeo ya wagombea wengine akiwemo, Anna Mghwira wa (ACT-Wazalendo) 98,763 sawa 0.65%, Chifu Lutalosa Yemba (ADC), 66, 049 sawa na 0.435 huku Edward Lowassa (Chadema) akimfuatia kwa kura Dk. Magufuli kwa kupata kura 6, 772, 848, sawa 39.97% na Hashim Rungwe wa (CHAUMMA) aliyepata kura 49, 256, sawa na 0.32%.

Wagombea akiwemo Janken Kasambala (NRA) 8, 028 sawa 0.03% na Maximilian Lyimo (TLP) 8, 198 sawa na 0.05% Fahmy Dovutwa (UPDP), 7, 785 sawa 0.05%.

Hata hivyo, Vyama 6 vimesaini matokeo ya urais ambapo wagombea wawili wa vyama vya CHADEMA na CHAUMMA, hawajasini karatasi ya matokeo ya nafasi hiyo ya urais.

Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani amesema majimbo 6 hayajafanya uchaguzi na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, wakati majimbo 5 hayajafanya uchaguzi kutokana na mapungufu mbalimbali.
 

Attachments

  • hongera Pombe.jpg
    hongera Pombe.jpg
    27 KB · Views: 13,544
Last edited by a moderator:
Ameshinda kwa asilimia 58.4% the lowest percent in history of Tanzania
 
Where do you see Tanzania five years from today...mungu akulinde, akupe nguvu, akujaze hekima na busara...Goodluck sir.

 
Last edited by a moderator:
Nimemwambia mwenyekiti wangu wa kule kijijini ajipange kupokea mil 50 na pia mwwenyekiti wangu wa mtaa kupokea mil 50. Ni raha tupu
 
Back
Top Bottom