Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5


M

mang ii

Senior Member
Joined
Oct 16, 2015
Messages
112
Points
0
M

mang ii

Senior Member
Joined Oct 16, 2015
112 0
Utata kuhusu!!
1.Tume kabla ya uchaguzi idadi rasmi ya wapiga kura 22.7M

2. Jk pale dodoma 28M

3. Leo wakati wa kutangaza matokeo 23.1M
 
H

haki na usawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
476
Points
195
H

haki na usawa

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
476 195
Kwanza nachukua fursa hii kukupongeza kwa ushindi ulioupta maana umepita katika chujio kali na mapito magumu ila sala na maombi yamekuongoza maana Allah katuamrisha tumwombe msaada wake pale ambapo tunaona tuko katika kipindi kigumu na hata cha hatari pia ili atupe ushindi au atunusuru na mabalaa ya wanadamu na mashetani (majini). Ni imani yangu nawe ulifanya maombi na Allah amekulinda kisha kukupa ushindi dhidi ya washidani wako.
Ushauri wangu kwako
1) Dumu katika kumwomba allah/mungu ili akuongoze na pia azidi kukulinda dhidi ya maadui maana nasi tutazidi kukuombea ili Allah akuongoze kutenda haki na kukulinda kwa ajili ya kulinda amani, mshikamano wetu na upendo!
2) Chama kinaonekana kuwa kimeanza kumomonyoka kimaadili, umoja na mshikamano ni vyema kukisuka upya ili kuondoa mgawanyiko ulivyoonekana katika kumtafuta mgombea ili kuwa kitu kimoja maana wananchi bado wana imani na chama kilichokusimamisha kugombea ni bora kukijenga upya mara utakapokabidhiwa jukumu la kukiongoza.
3) Kwa upande wa watumishi umma/serikalini nako bado kuna mgawanyiko kutokana na wanasiasa kujali maslahi yao (Mfano Profesa na Dr. wanaacha kufundisha vyuoni kutokana na maslahi/pensheni ndogo na kazi ngumu) zaidi huku wakisahau watumishi wa umma/serikali. Hivyo kuna watumishi wa umma/serikali wanaolalamika kusahaulika ama haki zao (Mishahara midogo na pia mafao madogo) kupuuzwa na mfumo uliopo na pia kuna wengine wanaonufaika zaidi na mfumo uliopo kuliko wengine hali wote ni watumishi wa umma!! Mfano ni utofauti uliopo katika mishahara kati ya mashirika umma na serikali kuu au serikali za mitaa. Ni bora pakaangaliwa upya ili kupunguza utofauti huo ili kuondoa malalamiko yaliyopo na kuwapa morari waliokata tamaa au kuona kuwa wao daima hawana pa kusemea!!
4) Ni vyema ukapanga ratiba binafsi za kushtukiza katika tasisi za umma/serikali ili kujionea utendaji wa watumishi wa umma uliopo ili kujua mizizi na matatizo katika mashirika ya umma/serikali ili kuondoa kero zilizowakabili wananchi muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na hivyo wewe kuwa ni mwenye kujionea jinsi wananchi wako wanavyopata huduma nzuri/mbovu kutoka katika tasisi za umma ili kurudisha matumaini ya wananchi katika chama chako na serikali kwa ujumla na aliyefanya vyema apongezwe na aliyetenda kinyume hatua stahiki zichukuliwe ili kuleta nidhamu ya utumishi wa umma na kuondoa dhana ya kulindana!
5) Taaluma mbalimbali zimeanza kuaangamia maana wanasiasa sasa wanafanya kazi za kitalaamu ama kulazimisha vitu vya kitalaamu kufanywa kisiasa ili tu kuridhisha wapiga kura na hivyo kusababisha migogoro kati ya wanasiasa na watalaamu bora taaluma zikapewa haki yake na hivyo kuleta tija na kutoka hapa tulipo!!
Yangu ni hayo tu nikuombee Allah akulinde, akuongoze na akujalie kila la kheri katika kazi yako mpya.
 
Z

Zungu Pule

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2008
Messages
2,218
Points
2,000
Z

Zungu Pule

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2008
2,218 2,000
Sasa Kazi Tu!
Hongera Rais mteule John Pombe Magufuli, pamoja na wengine wote walioshinda katika uchaguzi huu.
Hapa kazi tu! > Sasa kazi tu! > [Business as usual?]
 
PRINCE CROWN

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
4,652
Points
2,000
Age
43
PRINCE CROWN

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
4,652 2,000
hizi ndo tunaita AKILI PUMBAVU una pika matokeo na kuyaleta kwa ufahamu au kwa kutokufahamu na bado unapata wafuasi wenye akili PUMBAVU kama zako

kasome upya kura za eddo

ndo maana mnaitwa nyumbu ni kutokana na kuwa na AKILI PUMBAVU badae ufatilie unalopoka
Mkuu Kwani Uwezi Kubishana Kwa HOJA Mpaka Uporomoshe MITUSI? Au Matusi Kwa Sasa Ndiyo Sera Ya Chama?
 
I

iArmaniAdamson

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Messages
947
Points
225
I

iArmaniAdamson

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2015
947 225
~*~*~

Nitumie nafasi hii kumpongeza Daktari John Joseph Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Heko kwako Raisi Mteule na Heko kwa Wananchi wote wa Bara na Visiwani.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika

~*~*~*~

Sir. Armani Adamson
 
titimunda

titimunda

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2014
Messages
7,598
Points
2,000
titimunda

titimunda

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2014
7,598 2,000
Wamekubali elfu hamsini kila kijiji, flyover, laptop kwa kila mwalimu, viwanda vikuu kuu, mahakama ya mafisadi, madaraja, yaan hata kwa uchawi mahakama ya mafisadi haiwezekani, na mengne mengi tu, naomba miaka hii mitano niwe hai
Ngoja na mimi niombe uhai nije niyashudie hayo maajabu ya magufuli maana utekelezaji wake unahitaji miujiza
 
Chitolaki Napwachi

Chitolaki Napwachi

Member
Joined
Mar 31, 2015
Messages
84
Points
125
Chitolaki Napwachi

Chitolaki Napwachi

Member
Joined Mar 31, 2015
84 125
Wakuu,
Kwanza natoa pongezi zangu za dhati kwa watanzania kwa kushiriki kwa wingi katika mchakato mzima wa uchaguzi mpaka kufikia hatua ya leo ambapo tume imemtangaza mshindi.
Pamoja na mengi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu kumekuwa na wimbi mkubwa la watabiri na 'watumishi wa mungu' ambao wamedai kutumwa na Mungu kuleta 'Unabii' kwa watanzania juu ya 'chaguo la Mungu' katika kuiongoza nchi hii.
Wapo waliothubutu hata kuagiza kwamba wapo tayari kuuwawa endapo unabii wao hautakuwa kweli.
Je,muda umefika sasa kwa watanzania kuanza kuwatembelea watabiri na manabii hawa mmoja baada ya mwingine tukiwa na ujira mkononi ili kumlipa kila mmoja sawasawa na matendo yake?
Je utabiri/unabii usipotimia una tofauti gani na ramli chonganishi?
Je hawa manabii/watabiri wanastahili kupewa nafasi gani katika jamii yetu?
Jongeeni hapa wakuu tukumbushane kuhusu tabiri na nabii hizo na mchango wake katika kushawishi kura za watanzania.
 
moshi vijijini

moshi vijijini

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2015
Messages
3,348
Points
2,000
Age
24
moshi vijijini

moshi vijijini

JF-Expert Member
Joined May 14, 2015
3,348 2,000
Kwa hali ilivyo ndani ya taifa ili sio shwari kabisa na ukitizima mitizamo ya wana ukawa imekwama na ni ule mpango wa kupiga dili zao kwa kumtumia lowasa kushindwa pia nikumbushe ccm mtandao wao ni mkubwa kama mtawala pia tuliambiwa lowasa alihaidi swala la kulinda kura apewe yeye na cha kushangaza vijana wa IT wa ukawa walikuwa wanatumia mfumo wa mbovu kufanya tally pia niseme ni muda wa ccm kuleta mabadiliko naamin jp magufuli anatosha

Mungu ibariki tz mungu mbariki rais wetu
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,378
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,378 2,000
Umejifunzia hesabu wapi?
58% ya wapiga kura halali sio 58% ya watanzania wote.
6000000/53000000*100
Rekebisha kichwa cha habari
 
M

malifedha75

Member
Joined
Oct 27, 2015
Messages
13
Points
0
M

malifedha75

Member
Joined Oct 27, 2015
13 0
Maneno ya mfa maji mtakaaa mkisubiri Nchi imshinde na dua zenu mbaya, MUNGU HANAWAPENDA SANA WATANZANIA NDIO MAANA KATUPA RAIS BORA NA C BORA RAIS, TANZANIA KWANZAA MAJUNGU HAYANA NAFASI (HAPA KAZI TU)
 
T

TRUVADA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2014
Messages
4,527
Points
2,000
T

TRUVADA

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2014
4,527 2,000
Nadhani Lowasa kachanganyikiwa-kwani nimesikia anasema eti tume imtangaze yy kwani matokeo yake yanaonyesha kuwa kashinda kwa 62% huyu jamaa ni mbabe kiasi cha kuamuru tume imtangaze kwa data zake za nyumbani kwake.
usiumize kichwa mkuu ona aina ya watu wanaomzunguka .. kama SUMAYE MNGEJA KINGUNGE NA MREMA NDIO CAMPENI MENAJA WAO UNATEGEMEA NINI , Wao wanamdanganya et yeye kashinda mara mara kura zinachakachuliwa . wakiambiwa. waongeshe ushahidi hawataki , wao kulalamika tuuu
 
Wambandwa

Wambandwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
2,255
Points
1,500
Wambandwa

Wambandwa

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2006
2,255 1,500
Ngoja tuone, chizi kapewa pangs sokoni na akiamua kufyeka chochote mbele yake hakuna WA kumzuia.
Jk upo? Malipo hapa hapa...
 
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
13,363
Points
2,000
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
13,363 2,000
Ameshinda kwa asilimia 58.4% the lowest percent in history of Tanzania
Ndugu unaamini kuwa ameshinda?
Tume inatangaza, Mgombea ametangazwa kuwa ameshinda....hilo la kuchaguliwa na wengi mimi sina uhakika.
Tusubiri Chadema/UKAWA kama watatoa vielelezo vinavyothibitisha malalamiko yao kuwa wameibiwa ushindi.

Lakini nina wasiwasi kuwa wadanganyika wanaweza kumpigia "kula" mtu mwenye jina linaloambatana na mambo ya kilevi, hiyo itafanyika tu kama watu hao hawajielewi pia kama ni wapumbavu na malofa.

Unafikiri ni kwa bahati mbaya kuwa matokeo ya Uraisi hayawezi kuhojiwa mahakamani?
Huwezi kupinga matokeo ya Urais Mahakamani kwa hivyo goli la mkono liko hapo na litaendela kuwa hapo mpaka pale huu upuuzi utakapobadilishwa.
 
J

JBITUNGO

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Messages
1,223
Points
1,250
J

JBITUNGO

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2012
1,223 1,250
Sasa ni mwisho wa siasa za uchaguzi mkuu, hongera sana Dr. JPM. Huyu ni raisi wetu wote, tumpe ushirikiano, tujenge nchi yetu.
 

Forum statistics

Threads 1,284,202
Members 493,978
Posts 30,817,083
Top