Dr. Pallangyo, Mbunge mpya Arumeru ashindwa kuuliza swali la nyongeza Bungeni

Huyo mbunge anaangukia kwenye lile kundi la wabunge walioteuliwa na Mkurugenzi. Very hopeless.
 
Mkuu huyo ni jiran kabisa nlkuwa nikipita pemben ya fence yake nikienda shule o level, unayoyasema ni ya kweli kabisa, pamoja na fedha zote hzo hawez kukumbukwa kwa msaada wowote,
Huyu jamaa nimefuatilia taarifa zake wanadai ana fedha na ana vitalu vya uwindaji, kuwa na fedha kumembeba kufika hapa alipo.

Wanaomfahamu wanadai kati ya 2010 kwenda 2015 aligawa sana fedha za Rushwa kuupata ubunge , aliwanunulia vijana magari ya kushawishi watu wamchague. Ni rafiki yake nyarandu na walicheza Sana na fursa nyarandu akiwa maliasili.

Pamoja na kuwa fedha nyingi wapiga kura wake wanadai hana alichowahi kufanya tofauti na kujenga kituo kimoja Cha polisi. Sasa ni wakati wa yeye kutoa pesa kwenye miradi ya wananchi la sivyo akienda kwenye sanduku la kura ataanguka maana hadi anapata ubunge hakupigiwa kura
 
Nasikia huko jimboni kwake ni yeye tu alikuwa na Sifa kati ya wagombea wenzake 10. Balaa lingine la kina Waitara walikataa kufika chai ila sasa hivi wako kwenye kichaka cha kusifia
 
Ni tatizo la watu kupewa madaraka au nafasi kwa kuzingatia umri au kiasi chake Cha fedha. Msomi wa PHD kushindwa kutofautisha kutoa hotuba na kuuliza swali ni jambo la kushangaza. Nimesikiliza clip, inaonekana hata issue ya kutumza muda,kutumia mic hajui. Lakini mwishoni anasikika akimtaka waziri/Naibu waziri waongozane kwenda jimboni mwake

Kauli ya tuongozane ni ya kukariri, Ni kauli pendwa ya wabunge wengi lakini mnaongozana kufanya nini wakati hata swali tu umeshindwa kumuuliza Waziri?

CCM washinikizeni wabunge wenu kusoma na kujielimisha, wamerelax Sana kwa sababu angekuwa mpinzani lazima angekesha kusoma kanuni na taratibu zote bila kujali ngazi ya elimu yake

Huyu DR. Hawezi kusoma files yawezekana amezoea kuelekeza watu wafanye kama anataasisi anayoingoza au alikuwa mtumishi wa umma
Tuna Kundi kubwa la Wasomi wa Nadharia na sio wa Vitendo Mkuu.
 
Mimi nadhani mnamuonea huyo mbunge, wakati alichokifanya ndio uwezo wake! Ebu wote tujiulize mbunge hakupiga kampeni na kukutana na wapiga kura na kujua kero zao, mlitaka aulize swali gani? achilia mbali kuzijua kanuni siyo issue sana ila angeuliza maswali gani wakati katokea nyumbani kwake moja kwa moja kwenda bungeni? Inawezekanaje mbunge kabisa yupo ndani ya ukumbi wa bunge na anamuona spika mbele yake anamuita mh rais? soo sad.
Mh rais ? Hahahahahaha
 
Back
Top Bottom