Dr Norbert Kayombo afariki dunia.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,720
Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa, Dr Norbert Kayombo amefariki dunia hapo jana jioni jijini Dar.

Taarifa zinasema mazishi yake yatafanyika kesho 02/12/2010 jijini Dar.

Dr.Kayombo alikuwa mweledi wa Sayansi za majini(Marine Science), na kwa siku za mwishoni alikuwa mmojawapo kwenye jopo la watu waliopewa jukumu la kuandaa mpango-mkakati wa kurejesha Tanzania mifupa(skeleton) ya mnyama wa kale (dinasours) iliyoko kwenye jumba la makumbusho huko Berlin-Ujerumani.

Mungu ailaze pema roho ya Marehemu.
 
Kama namuona vile na shati lake ya kitenge na suruali ya kitambaa, alikuwa mtu wa kawaida sana, mnyenyekevu,mpole na msikivu sana Dr. Kayombo.
Amefariki hata bila la kuona ufunguzi wa Makumbusho mpya ya Taifa.
R.I.P Dr.Kayombo
 
R.IP Dr wa Ukweli. Utakumbukwa kwa upole wako na umahiri kwenye tasnia ya Utamaduni na Makumbusho.
 
r.i.p kayombo
kuna bwana kayombo mmoja mtu wa kilaji na vimwana balaa ni ndugu yake huyu?
 
Kweli ni huzuni kubwa, alikuwa mtu mcheshi, mwenye hekima, busara na msaada mkubwa. Nakumbuka nilikutana naye ofisini kwake tarehe 27/10/2010. Tuliongea kwa muda wa kama dk 20. Ninapoumia zaidi ni pale ninapokumbuka yale tuliyozungumza na kupanga kuanza kuyafanyia kazi katikati ya mwezi wa 12. Kumbe hatukujua kuwa hatutakutana tena.

Ina Lilahi Waina Ilayhi Raj'un.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom