Inashangaza jinsi watu wanavyoweza kudanganywa na kudanganyika kirahisi namna hii. Au ndio matunda ya shule za yeboyebo? Huyo anayejiita Dr Ndodi ni muongo na tapeli mkubwa, hana hata chembe ya elimu ya tiba. Kinachomwezesha kuwafikishieni uongo wake ni uwezo wake wa kulipia vipindi vya TV ambao anaupata kutoka kwa wadanganyika. Biashara huria. Na wataalamu tuliowasomesha kwa kodi zetu wapo, wanakaa kimya huku tukiangamizwa na matangazo ya tiba feki. Nguvu ya pesa. Ni uleule ufisadi unaendelea kutuguguna. Wizi mtupu.