Dr. Namala Mkopi (kiongozi wa MAT) afikishwa mahakama ya Kisutu

Electron

Member
Jul 3, 2012
92
49
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.


N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.


Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....




Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne
 
Nendeni mkamuwekee dhamana maana hana cha kujibu hapo, mahakama imeishaigiliwa na mhimili mwingine wa DOLA katika maamuzi.
Mahakama ikitaka kutenda haki itoe tamko juu ya DOLA kuingilia mhimili wake, inaonekana mahakimu wetu wanasukumwa na DOLA katika kutekeleza majukumu yao? Jaji mkuu alishasema kuwa serikali inaingilia mahakama.
Mwisho kinachotakiwa ni vitendea kazi mahospitalini siyo kuandama mtu mmoja mmoja kisa Daktari.
 
Kwanini wamlazimishe kutoa tangazo la kusitisha mgomo wakati sio yeye aliyetangaza mgomo, naona serikali inachezea kodi zetu kwa kesi amabazo huna hata hja ya kuweka wakili kushinda.
 
Dr Namala Mkopi go... Tuko nyuma yako kabisa.. Wachache hawajui kazi yetu ni ya kuendana na kiapo na kwa namna tunavyodai haya madai ya kuboreshwa huduma mbalimbali katika sekta ya afya,baadhi wanaidiverge hoja kwenda kwenye dai la 7 au la 8 huko kati ya madai yote...

Lakini hawajui yote ni kwamba tunataka kiapo chetu tukitekeleze barabara... Tukilazimika kufanya kazi kwa mtindo huu,nina imani kubwa kwamba baadhi yetu,si wote,ila baadhi yetu,tutakuwa na ganzi katika kukikukumbuka na kukiheshimu kiapo chetu...
 
Madaktari wote waliokwenye mgomo na kuacha ndugu zetu wakifa hovyo nawaona kama mazuzu tu

Hapa si kwamba tunaunga mkono Mgomo, maana sisi ndiyo tunaumia zaidi kuliko hao Mafahari wawili. Ila tunatia shaka jinsi Serikali inavyolishughulikia tangu mgomo wa kwanza haujaanza.

Wamefanikiwa kupiga Propaganda na Kuipandisha daraja Hospitali ya Lugalo kuwa ya Rufaa kama ndiyo suluhu ya harakaharaka. Hapa wanataka wananchi tujue Serikali inalihangaikia hili Tatizo, wakati wanafanya kiini macho cha kumpeleka Mahakamani mtu asiyehusika.

Mbaya tunaendelea kutesena na kufa kwa kukosa huduma.

Pia nakushauri kwa huo mchango wako hapa, ungeanzisha thread yako.
 
Inakuwaje Mwenyekiti wa MAT kushtakiwa kwa kosa la Mwenyekiti wa Jumuiaya ya Maktari. Ina maana Polisi hawaoni kuwa anaweza kuwashinda na kama sheria ingekuwa inaruhusu angewadai fidia. Lakini sheria hairuhusu Mtuhumiwa kudai fidia ndio maana wamemfikisha mahakamani.
 
inachofanya serikali ni kuwatisha tu...haa ukizingatia kuwa dr mkopi ameandika barua Umojawa mataifa.....kinachofanyika ni kutaka kumnyamazisha tu
 
duuh!hiii kali yani mwenye kuitisha mgomo mwingine aliyekamatwa na kushitakiwa mwingine hakika hii haiitaji kuwa profesa kugunduwa kuwa kuna ushawishi wa kisiasa katika hili haya ngoja tuone mwisho wa picha hili itakuwaje
 
Chama cha Kigaidi chenye selikali inayo uwa watu na kuwatesa. Hivi Mwalimu,Kolimba,Kombe nawengine wengi waliuwawa na nani?
 
Madaktari wote waliokwenye mgomo na kuacha ndugu zetu wakifa hovyo nawaona kama mazuzu tu
JF si mahali pa watu wa aina yako,wasiojua nini kinaongelewa na kujibu tofauti na hoja iliyopo mezani
katafute mitandao ya watu wanaoweka akili zao likizo kama wewe.
kuhusu Dr.Mkopi don't worry Mungu siku zote anasimama upande wa haki" ni suala la muda tu.
 
Heri vita inayodai haki na utu kuliko amani inayopumbaza nakumbuka maneno haya hasa jinsi mambo yanavyoendeshwa ndivyo sivyo kwa kisingizio cha aman
 
someone said yaweza pia kuwa ni mbinu chafu ya kuwachanganya madaktari na vibweka vingi wasiweze kujipanga vizuri dhidi ya serikali...
 
Back
Top Bottom