DR. Namala Mkopi amepandishwa mahakama ya Kisutu kinyume cha Sheria

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
374
509
Wakuu nimeweka hapa kwa wajuvi wa Sheria ili tuweze kuangalia jambo hili, kwani MJL ameeleza kuwa Kupandishwa kwa Dr. Mkopi katika mahakama ya Kisutu ni makosa, soma maelezo hapo chini tujadiliane;
Baada ya serikali kuitumia mahakama ya Kazi kujaribu kuwadhibiti madaktari, sasa imekimbilia mahakama ya Kisutu, ambako kuna vijana wanaoutaka Ujaji-wakiambiwa, wanafanya!

Ndugu zangu, kwa mujibu wa sheria, Penal Code, Sura ya 16, kifungu cha 114, kosa analotuhumiwa nalo Dr. Mpoki ni kudharau mahakama. Period!.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, anayedharau amri ya mahakama huwa anapelekwa mbele ya Jaji au Hakimu aliyetoa AMRI iliyokaidiwa. Kwa msingi huu, nathubutu kusema, na niko tayari kutetea kauli hii, kwamba kesi iliyo mahakama ya Kisutu, haiko sawa kisheria.

Hivi, wahusika wote katika system ya administration of justice, hawajui jambo hili ambalo "anybody with a browing acquaintance with law" analijua?.

Kwa lugha nyingine, inawezekana kwamba hawajui kuwa kwa hakika wao ndion wanafanya kosa la CONTEMPT OF COURT, kwa kuonyesha, kwa kujua ama kutokujua(which is never a defence), kwamba Mh. Jaji Sekela Moshi aliyetoa amri ile HANA UWEZO WA KUISIMAMIA AMRI YAKE?

Je Hakimu hajui kuwa anafanya kosa lile lile kwa kupokea kesi ambayo iko kwa mkubwa wake kikazi? Kosa linalodaiwa limefanywa "in limine litis" yaani katikati ya shauri linaloendelea Mahakama Kuu.

Mahakama inao uwezo wa kutokukubali mashauri yanayopelekwa kwake kinyume cha sheria. Ni vema mahakimu wetu wakaelewa mamlaka waliyonayo katika kupokea na kusikiliza mashauri.

Hivyo ndivyo sheria ilivyo,

Source:
Mutabaazi Lugaziya wa Mabadiliko Forums
 
Back
Top Bottom