Dr Mwigulu: Ni dhambi kubwa kuwarithisha madeni watoto wetu, Watatuuliza kama hatukuwa na hela tulijenga Bwawa na SGR za nini?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Waziri wa fedha mh Mwigulu Nchemba alisema Bungeni kwamba bado miradi mikubwa ya Bwawa la umeme na SGR inahitaji fedha hivyo siyo vema kuchukua mikopo kwa sasa.

Dkt. Mwigullu amesema ni dhambi kubwa kuwarithisha madeni watoto wetu kwani watahoji kama tulikuwa hatuna hela kwanini tumejenga bwawa na SGR?

Dkt. Mwigullu Nchemba alilisihi bunge kwamba miradi ya sasa igharamiwe na kizazi hiki hiki ili tuwape furaha watoto wetu baadae na ndio maana ikaanzishwa kodi ya kizalendo kwenye miamala ya simu na laini zake.

Chanzo: Kutoka Bungeni
 
Hilo Bwawa na Hizo SGR, Hazima Umuhimu wowote kama Ni Kutunyonya Kwa Niamba ya wajukuu zetu. Kwenye Vipao Mbele Ni vema Viangaliwe Upya.

Hatuko Tayari Kukamliwa kwa Miradi ambayo Hatukuhusishwa. Waziri wa fedha wa Ajabu sana Kupata Kutokea, Maana yeye anachofikiria ni Kumaliza tu Miradi bila kuangalia Welfare ya watu wake.
 
Waziri wa fedha mh Mwigullu Nchemba alisema bungeni kwamba bado miradi mikubwa ya Bwawa la umeme na SGR inahitaji fedha hivyo siyo vema kuchukua mikopo kwa sasa...
Magufuli alisema wazi kuwa hela za kujenga hilo bwawa na sgr ipo. Inakuwaje ghafla leo hawa waliokuwa wasaidizi wake watake kutukamua ili kulipia tena miradi ile ile iliyokuwa na hela? Kuna harufu za EPA hapa.

Mwigulu must go!
 
Maendeleo makubwa si kazi rahisi kuyafikia.

Bahati mbaya baadhi yetu Watanzania tunapenda "SHORTCUTS".....hatutaki/hatupendi kujiumiza hata kidogo kwa ajili ya KIZAZI.....

But all and all WANANCHI NDIO WENYE NCHI YAO.

#KaziIendelee
 
You mean Madeni ambayo wahitimu wakimaliza wadaiwa wala bila guarantee ya kipato cha kuweza kujikimu let alone kulipa hayo madeni ?

Hao watoto hawawezi kusema lolote ukizingatia wazazi wao wameshakopa mpaka kuuza asset zao ili tu wapate cheti ambacho hakina msaada kwa watoto wala wazazi wao
 
Waziri wa fedha mh Mwigullu Nchemba alisema bungeni kwamba bado miradi mikubwa ya Bwawa la umeme na SGR inahitaji fedha hivyo siyo vema kuchukua mikopo kwa sasa...
Huyu Waziri awahishwe hospitali.Inawezekana kuna tatizo kubwa somewhere,kodi zingine tunazolipa kumbe siyo za kizalendo?Hizo tozo zinaweza kufanya miradi ya matamanio ya watawala na kulipa deni la Taifa lote?

Mwigulu anataka tuamini kuwa hivyo miradi ni bora kulikoni ustawi wa Watanzania?Tunalazimishwa na nani kuwa na SGR,JNHEP,Busisi-Kigongo Bridge, Tanzanite Bridge,Flyovers nk.kwa wakati moja?

Kama hatuna resources sasa tugange njaa hadi wakati muafaka au twende kwa awamu.Busara ya kawaida tu ingetosha kuepusha vurumai na vichoko choko vinavyoepukika.
 
Tulikopa kwa exim ya china kwa ajili ya tpdc, je huo mkopo umesaidia nini watanzania? Bomba linatumika 6% tu huku watanzania tukilipa zaidi ya trilioni 5.

Hii nchi haitaweza kuendelea kama ccm wataendelea kutawala.
Fedha zilizotupwa Stiegler's ingekamilisha Kinyerezi hata 20 leo tungekuwa tunauza umeme Afrika nzima.Kuongozwa na Lunatics ni hatari.

Badala ya kujenga SGR along TRC central line ni uzembe mwingine,ingejengwa Mtwara-Mbamba Bay ingefungua Southern corridor na SGR ya TAZARA iwe ya umeme huku tukikarabati TRC line zote.Akili za CCM wanaziweza wao pekee.

Badala ya madege John ya hapa kazi tu tungekamilisha miradi ya afya na elimu nchi nzima nk.

CCM must go!

Tunataka Katiba ya Wananchi
 
Mathalani ujenzi wa BWAWA LA KUFUA UMEME LA MWALIMU NYERERE utakamilika MWAKANI 2022.......
Kama ni hivyo it's fine make hata current generation kodi zetu zitakuwa zimetufuta jasho. But nakukumbusha jiwe alituhakikishia by Nov 2019 dar to Moro tutakuwa tunatambaa na treni la umeme lkn mpaka Leo ziiiii
 
Back
Top Bottom