Dr. Mwigulu Nchemba shughulikia kero hii

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,109
7,685
Kwanza nachhukua nafasi kumpa Hongera Dr. Mwigulu Nchemba kwa kubaki katika Baraza la Mawaziri na safari hii katika Wizara injini ya Taifa; Wizara ya Fedha, Hakika Mhe. Rais amekuamoni sana na anamatarajio makubwa sana lkn sisi wananchi pia tunamatarajio makubwa sana kwani hatuna shaka na utendaji wako mahiri na ulio tukuka.

Tafadhali baada ya kula kiapo hiyo kesho shughulikia kero ya madai ya Malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma ambayo imekaliwa kwa muda mrefu, hicho ni kilio cha muda mrefu, wapeni haki yao nao wapate furaha na matumaini mapya. Hakika Mungu atabariki kazi yako kwa kuhakikisha haki zao zinapatikana.
Mungu huwabariki zaidi viongozi ambao wanajali haki za watu na kuzitatua.

Hongera sana na Mungu akubariki.
 
Mhe. Waziri mteule akitaaka kuanza na baraka ahakikishe anasimamia uharaka wa ulipwaji wa WASTAAFU hapa nchini hakika hili ni janga SASA IVIIII
 
Mhe.Waziri mteule akitaaka kuanza na baraka ahakikishe anasimamia uharaka wa ulipwaji wa WASTAAFU hapa nchini hakika hili ni janga SASA IVIIII
Wengne wanalia na madaraja🙉🙉hakika waziri ana Mambo mengi ya kushughulikia
 
Mwagilu is a man of action, am sure 100% ata chukua hatua haraka kushughulikia kero zilizo kaliwa hazina.
nadhani pia hazina yetu bado inachembe chembe za urasimu.
 
leo trh 1/3/202, tunawatakia mawaziri wote watakao kula kiapo leo Mbele ya Mhe. Rais tunawatakia kila la heri.

Katika awamu hii ya 6 tunawataka wafanye kazi kwa bidii na maarifa zaidi maaana awamu hii imejipambanua wazi kuwa kamwe haitomlea wala kuvumilia uozo wowote ule.
Kazi Kazi.

KAZI.......KAZI, MAJUNGU FITINA havina nafasi.
 
Back
Top Bottom