Dr. Mwigulu Nchemba: Mikataba ya Wazabuni wote wa Jeshi la Polisi kupitiwa upya

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,904
141,853
Waziri wa mambi ya ndani Dr Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la polisi kuipitia upya mikataba yote ya wazabuni ili kubaini uhalali wake.

Kamishna wa fedha wa jeshi hilo ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa wakati na kulitolea ripoti.

Source: Eatv habari!
 
Hivi uhakiki utafanywa kwa muda gani, mara ngapi na vyombo/taasisi ngapi? Inaelekea serikali hsiamini vyombo vyake au ni mwendelezo wa dhuluma kwa wananchi?
 
mwigulu ameona amekaa mda mrefu bila tamko kitu ambacho ni kinyume na serikali ya awamu ya tano, kutotoa tamko lolote ktk hii serikali ni uzembe pia kutoendana na kasi ya JIWE. asante bwana [HASHTAG]#mwigulu[/HASHTAG]
 
Waziri wa mambi ya ndani Dr Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la polisi kuipitia upya mikataba yote ya wazabuni ili kubaini uhalali wake.

Kamishna wa fedha wa jeshi hilo ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa wakati na kulitolea ripoti.

Source: Eatv habari!
Ule wa Lugumi umefikia wapi ?
 
Yaani hao hao waliingia mikataba halafu hao wenyewe waipitie then waje na majibu kuwa ni batiri? hivi ule wa lugumi imeishia wapi kwanza.
 
Yaan Mtuhumiwa kapewa kazi ya kuchunguza Na kutolea ufafanuzi ukweli Au uongo wa tuhuma zinazomkabili!

Wahusika waliotoa zabuni ndio wameambiwa wachunguze uhalali wa Zabuni hizo!

Kila la Kheir kwenye uchunguzi huo
 
Waziri wa mambi ya ndani Dr Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la polisi kuipitia upya mikataba yote ya wazabuni ili kubaini uhalali wake.

Kamishna wa fedha wa jeshi hilo ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa wakati na kulitolea ripoti.

Source: Eatv habari!
Wizara inaongozwa na yule aliepeleka magari kilimanjaro kutengenezea
 
Jambo jema sana kwa mustakabali wa Jeshi letu na Nchi yetu kwa ujumla. Pia angazia msambazaji wa vile vifimbo vya ngozi vya maaskari vimepinda pinda tofaut na zaman, pia sare zinawahi kuchuja hizi baba zimetengenezwa kimaslahi zaidi.
 
Back
Top Bottom