Dr Mwele Malecela kuchukua nafasi ya Blandina Nyoni?

Mteule wenu Waganga anafaa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali (CMO) na sio Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
 
Blanduma hana kosa ndivyo alishauriwa na Daktari kilaza CMO Mtasiwa.
Kuwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Daktari ni mwiko kwani Wizara ya Afya haina kada moja tu ya udaktari au kama vipi madaktari mpatiwe wizara ya Madaktari ambapo mtajiongoza wenyewe. Ipo siku kwa ufinyu wenu wa kufikiri mtasema hata wahasibu, wachumi, maafisa Utawala na Utumishi katika wizara ya Afya wawe Madaktari;

Mkuu sijakuelewa!!unapata wapi ujasiri wa kusema kuwa katibu wa wizara ya afya ni mwiko kuwa daktari!!?kama umesema idara ya afya ina kada zingine blandina alikuwa wa kada gani upande wa afya?kwangu mimi ni vizuri waziri na makatibu wao kuwa na fani husika,mfano waziri wa fedha awe amesomea masuala ya fedha/uhasibu,si vizuri mtu amesomea kilimo sua anakuja kuwa waziri wa fedha,vice verse is true!
 
Tatiana_Elephantiasis[5].jpg

Katibu Mkuu (in waiting) Dada Mwele Malecela​

Huyu hana tofauti na Blandina Nyoni. Nae anatabia ya kukiuka taratibu za manunuzi katika manunuzi ya Maua na vifaa kwa ajili ya sherehe ya Nane Nane ya mwaka 2011 ambapo alicomand direct procurement kutoka Mariedo bila kuwa na mkataba na wala bila kushindanisha na wauzaji wengine. Kwa kifupi nae ni Mateka wa Mariedo!
 
Sina hakika na ubashiri wa Mwele lakini chochote chaweza kutokea hapo wizarani. Rais atajitokeza na kujitakasa na kumaliza huu mgogoro. Atajitakasaje sasa? Nadhani watu lazima wawajibike ama kuwajibishwa.
 
kwa baadhi yetu tunaomfahamu vizuri mama nyoni muda mrefu, anavyosemwa katika jf si sahihi ni kupakwa matope na wasiomtakia mema. Huyu mama ni kiongozi mzuri, anayejua analolifanya na kupenda wafanyakazi waliochini yake. Ana msimamo thabiti kwa jambo analoamini yuko sahihi na huwa na vielelezo kwa kila jambo analofanya. Kwa mtu yeyote ambaye anajua menejimenti, a professional manager anaweza kuongoza sehemu yoyote ya kazi si lazima awe na taaluma husika. Wale wanaofikiri madaktari ndio wanaweza tu kuwa viongozi wa wizara ya afya ni wazi hawajui menejimenti ni nini. Mama nyoni ni meneja, ndio maana kama makatibu wakuu wengine na hata mawaziri si lazima awe wa taaluma husika ya wizara. Ni vyema kumhukumu mtu kwa matendo yake na haki yake apewe.
wewebchamu huna lolote umejiunga jamii forum ili kumtetea blandina?ukweli aachie ngazi kazidi kuonea madaktari.ananunua ving'amuzi vya magari wakati madaktari hawalipi hela zao?
 
Kwa baadhi yetu tunaomfahamu vizuri mama Nyoni muda mrefu, anavyosemwa katika jf si sahihi ni kupakwa matope na wasiomtakia mema. Huyu mama ni kiongozi mzuri, anayejua analolifanya na kupenda wafanyakazi waliochini yake. Ana msimamo thabiti kwa jambo analoamini yuko sahihi na huwa na vielelezo kwa kila jambo analofanya. Kwa mtu yeyote ambaye anajua Menejimenti, a professional manager anaweza kuongoza sehemu yoyote ya kazi si lazima awe na taaluma husika. Wale wanaofikiri madaktari ndio wanaweza tu kuwa viongozi wa wizara ya afya ni wazi hawajui menejimenti ni nini. Mama Nyoni ni meneja, ndio maana kama Makatibu wakuu wengine na hata mawaziri si lazima awe wa taaluma husika ya wizara. Ni vyema kumhukumu mtu kwa matendo yake na haki yake apewe.

Rafiki unasema Blandina Nyoni ni kiongozi mzuri anaejua analolifanya? Well hatuwezi kukupinga maana Mwizi anapoiba anajua kuwa anaiba. Kuhusu kwamba anapenda wafanyakazi walio chini yake hakika unadanganya. Kamuulize mfanyakazi yeyote ambae yupo Wizara ya Maliali na Afya watakwambia jinsi gani huyu Mama asivyowajali watumishi wake. Kuhusu kwamba ana msimamo thabiti kwa jambo analoliamini kwamba yuko sahihi offcoz siwezi kukupinga maana ameonyesha ni jinsi gani ni muhimu kuwafukuza Intern Doctor na kuwapeleka Mikoani only katika cases za Migomo tu. Pia unasema kwamba wale wanaofikiri madaktari ndio wanaweza tu kuwa viongozi wa wizara ya afya ni wazi hawajui menejimenti ni nini offcoz tunaweza kukubalina na wewe kama hii Menejementi ya Blandina Nyoni unaiona ni Bora kuliko hata ya kina Wilson Mukama, Hilda Ngowi, Mwafisi, et al.
 
Mkuu sijakuelewa!!unapata wapi ujasiri wa kusema kuwa katibu wa wizara ya afya ni mwiko kuwa daktari!!?kama umesema idara ya afya ina kada zingine blandina alikuwa wa kada gani upande wa afya?kwangu mimi ni vizuri waziri na makatibu wao kuwa na fani husika,mfano waziri wa fedha awe amesomea masuala ya fedha/uhasibu,si vizuri mtu amesomea kilimo sua anakuja kuwa waziri wa fedha,vice verse is true!
Nimekusoma lakini sio lazima sana awe Daktari anaweza kuwa Afisa Muuguzi, Afisa Afya, Afisa Ustawi wa Jamii, Pharmacist, Katibu wa Afya, Afisa Mtekinolojia Maabara NK katika sekta ya afya
 
Anafaa kuwa Katibu Mkuu wa Madaktari na sio Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
 
Nakubaliana kabisa hapa. Dr. Mwele ana uwezo mkubwa sana na ana sifa nzuri; watu kama hawa haitakiwi kuwaingiza kwenye mazingira ya siasa kwa sababu mwisho wake wanakuwa victims wa ujinga uliojaa serikalini. Itakuwa vyema kama akiachwa palepale NIMR kuliko kumuingiza kwenye mfumo mbovu usiojua kutenganisha siasa na utaalam.

Mimi nauliza kitu kimoja tu. Hivi huyu Mwele Malecela aliipataje hiyo post ya Ukurugenzi wa NIMR. Je aliomba kazi? Alifanyiwe Interview? Je alishindanishwa na Watanzania wengine? Au ni mwendelezo wa nasaba za Watawala?
 
Nini kilichomshinda mpaka mgomo wa madaktari ukatokea.

Mkuu,
Hili ni swali zito sana kwa Watetezi wa Blandina Nyoni. Watakwambia tu Oooh ni kiongozi mzuri, Oooh anaziba mianya ya wizi, Oooh ana CV ndefu!
 
Haijatulia kabisa ikiwa Wazira wa Afya ni Daktari, Naibu waziri ni Daktari, Mganga Mkuu wa Serikali ni Daktari, Wakurugenzi wote wa Wizara pamoja na Idara za Utawala na Mipango, Madaktari, Manaibu Wakurugenzi wote wa Wizara Madaktari, Wakuu wa miradi yote ya Wizara (Program) Madaktari, Mhasibu Mkuu wa Wizara Daktari, Afisa Manunuzi wa Wizara Daktari, Viongozo wa Idara ya Afya katika Mikoa na Halmashauri ni Madaktari wakurugenzi wote Hospitali Madaktari. Kwa ulafi huu wa Madaraka na ubaguzi wa kada nyingine za Afya nashauri kuanzishwe Wizara ya Madaktari tu.
 
Back
Top Bottom