Dr. Mwele Malecela aula! Awa Makamu wa Rais IANPHi

Hongera Dr mwele! Le mutuz ana gundu!

Lakini kupigwa gap na sister ni aibu? Ingawa tunasisitiza usawa Le Mutuz naye angejitahidi akawajibu dada zake bwana! Pamoja na uwezesho wote ule yeye akafulia!! AIBUUUUUUUUUUU!!
 
Hongera sana Mwele...wanaundugu nadhani ni Baba mmoja ila Mama mbali mbali. Mama yake Mwele alishafariki miaka mingi ila nilisoma hapa jamvini kwamba Mama yake Le Mutuz bado yu hai.
 
Hongera Dr.wewe ni mashine,sio wale kama wenzetu wanaotegemea kubebwa badala yakuproduce vya kwao
 
Sasa ni wakati muafaka kwa huyu mama kuolewa kwa mara ya kwanza, maana kuendelea kukaa bila mume ni hatari sana kijamii.
 
Wao walipata privilege ya elimu nzuri ndio maana tunapigana kubadili system tuwape pia nafasi watoto wa maskini wa Tanzania

Hata kwetu watu kama ninyi mpo roho hukutoka na kujikunja kwa sababu tu eti kwanini yule,,,,, imekula kwako muulize baba na ndugu zako wengine walikuwa wapi wakati huo na na hata kwa haya mageuzi bado yatakuwa kwa wachache lakini wanofanana ....... pole
 
Kichwa sana huyu tangu akiwa Zanaki. Duh, nimekumbuka ile ajali miaka ilee ambayo waliishia kumpoteza kaka yao mkubwa baada ya kuiba gari na kuwabeba kwenda kwenye party. Huyu aliumia sana kichwani lkn bado zimeendelea kuchemka ! Huyo mwingine analazimisha tu jina....lol

Congrats. Katuwakilishe vema

dr-mwele-ntuli-malecela.jpg


wceo1.jpg
 
Mimi kiukweli nampenda sana mwl.nyerere,ingawa jamaa mmoja aliniambia kuwa mimi ni mtumwa wa legacy ya mwalimu,nakubali sana iwapo utumwa huo utanipa muda zaidi wa kupata interesting stories za Mwl.

Kama mnakumbuka vema,mwaka 1989,mh.Malecela alikuwa balozi nchini uingereza kabla ya kuitwa mwaka 1990 kuja kukamata nafasi ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais Mwinyi.Wakati huo watoto wake wakubwa wa kike,yaani Dr.Mwele, Dr.Seche na Judge Mwendwa walikuwa wanasoma nje ya nchi.Dr mwele akiwa UK,Seche akiwa USA na Mwendwa akiwa chuo cha Birmingham nchini uingereza.

Mzee Malecela alisema kuwa Mwl alifika kwake ubalozini wakati watoto wake wote wakiwa likizo.Wakaitwa mbele za Mwl nakuanza kutambulishwa mmoja baada ya mwingine kwa majina na shughuli au masomo anayofanya.Dakika chache baada ya utambilisho Mwl.alitoa kitambaa na kuanza kufuta machozi kwa muda wa dakika kadhaa.Nikamuuliza mzee Malecela kama mwl. alisema ni nini kilimliza au kama anaweza ku-guess,akasema hajui.Na akakataa kata kata ku-guess.

Jambo hilo lilinishangaza sana,lakini binafsi nilihisi Mwl.alilia kwa sababu ya tofauti alioiona kati ya watoto wake na wa malecela,kielimu na hata kimaisha. Wenzangu mnasemaje?

Hata hivyo nitaendelea kuwaletea yale msiofahamu kuhusu mwl.Nyerere.
hii ni post ya mwanjf mwenzetu
 
Honbgera mama, jishike huko huko usije kwenye siasa, utachafuka mpaka, tumekia nchi kwa nyia hiyoooooooo
 
Back
Top Bottom