Dr. Mwakyembe tumekusikia, Sasa tuambie ukweli kuhusu ile siri mliyoificha kuhusu Richmond

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,304
12,965
Mh. Dr. Mwakyembe amekanusha kuhusika kumchafua Lowassa katika mbio za kugombea urais. Katika maelezo yake amesema kazi ya kuchunguza kashfa ya Richmond walitenda haki na kwa uadilifu mkubwa.

Lakini wakati alipowasilisha ripoti bungeni na wakati mjadala umepamba moto wakidaiwa kutokutenda haki katika kazi yao ya kuchunguza, alisimama akasema kama watu hawaridhiki waombe kanuni zitenguliwe ili awasilishe upya ripoti yao ili aseme na siri waliyoificha ili kuiokoa serikali isiporomoke yote.

Sasa wakati akisisitiza kuwa walitenda haki wakati alisema kuwa kuna siri waliificha inakuwa vigumu kumuelewa huo uadilifu anaousema. Mimi namshauri Dr. Mwakyembe sasa aitoe hadharani ile siri waliyoificha kuepusha serikali kuporomoka yote na hivyo kupelekea serikali kuporomoka nusu kwa kujiuzulu kwa Mh. Lowassa.

Kwa sasa hakuna cha kupoteza Dr. kwasababu serikali iliyopo inaenda kuporomoka yenyewe kwa mujibu wa katiba hapo ifikapo mwezi Octoba. Hivyo wewe huna cha kupoteza na wala serikali iliyopo itakuwa haina cha kupoteza kwasababu uhai wake unaishia ukingoni. Bila kuisema hiyo siri uliyosema mliificha, suala la Richmond litabaki kuwa tata hadi ukamilifu wa dahari.

Tuliwagharimia kwa mamilioni mzunguke duniani kwenda kuutafuata ukweli. Nanyi mkafanya kazi yenu vizuri na kuupata ukweli wote. Mliporudi badala ya kutupa ukweli tuliowatuma, mkatupa ukweli nusu. Ukweli usiposemwa wote huo huwa hauwi ukweli kamili, na kwakuwa unakuwa haujasemwa wote, ndani ya huo ukweli nusu unaosemwa huwa kunakuwa kumechanganyika na uongo na uongo ukichukua nafasi kubwa maana nzima ya ukweli hupotea.

Hivyo ndivyo mlivyoipoteza maana nzima ya ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya Richmond kwani ukweli mkuu haukusemwa. Hiyo ilikuwa ni sawa na kumpa mgonjwa nusu dozi matokeo yake maradhi huwa sugu. Maradhi sugu tuliyoyapata ni kuzaliwa kwa ESCROW ambayo nayo haina tofauti sana na EPA na RADA. Ukiangalia maradhi yote hayo ni kutokana na kutotoa ukweli kamili.

Hivyo kama nawe ni mmoja wa watangaza nia, msalaba wako mkubwa itakuwa ni kuusema ukweli kwani ukweli humuweka mtu huru naye huwa huru kweli kweli. kwakuwa mpaka sasa unajaribu kujitetea bila kusema ukweli, itakuwa vigumu kwa watu wenye akili timamu kukuamini kwa lolote sana sana utaonekana ni mtu uliyetayari kuificha kweli kwa tamaa ya vyeo vipitavyo.

Ni dhahiri katika kuuficha huo UKWELI mtakuwa mliwaumiza watu wengine ambao hawakupaswa kuumia na kudharilika. Mlichokifanya kilikuwa sawa na kukivunja kichwa kwa kosa lililofanywa na ulimi - Ulimi uliponza kichwa, kichwa kikavunjwa bila sababu "NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO!"
 
Umeongea jambo la msingi sana.

Ni kweli wakati anawasilisha ripoti ya Richmond, akiwa Mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyochunguza ksshfa hiyo, alinukuliwa akihitimisha ripoti hiyo akisema kuwa kama kamati yake ingeamua kuanika hadharani kila lilichokiona wakati wa uchunguzi wake basi serikali iliyoko madarakani ingeweza kuanguka.

Sasa hapo ndipo linapojitokeza swali la msingi, ni kipi hasa kilichofichwa na kamati ya Mwakyembe, ambacho kilikuwa na lengo la kuiokoa serikali ya Sisiem isianguke?!
 
mwakyembe mnafiki mkubwa alificha ile siri kwa manufaa ya nani yeye ni mwanasheria tena mwalimu wa sheria lakini ameidhalilisha taaluma ya sheria kwani aliingiza siasa kwenye sheria ndio amempa kichwa mamvi kujitangaza kuwa hakuhusika alitakiwa amwambie ukweli sio kumwambia ajipime
 
Dhambi hiyo itamtafuna siku zote za maisha yake. Tiba yake itakubalika tu kama atasema ukweli alioficha kwa lengo la kuumiza wengine huku akidanganya ni kuilinda serikali. Sijui ni Mungu yupi anadai alimtanguliza. Watu wanamchezea Mungu sana.
 
Wewe jiulize kwa nini mamvi anapigwa vita hadi kuna watu wanakesha kumuombea dua afe? Mamvi akichukua nch piga ua zaragaza zika fukua baada ya miez miwili atamuachia Babu Seya na papii huru kama kisasi cha kwanza cha faster.
 
Hapo atamkomesha JK
 
Mh. Dr. Mwakyembe amekanusha kuhusika kumchafua Lowassa katika mbio za kugombea urais. Katika maelezo yake amesema kazi ya kuchunguza kashfa ya Richmond walitenda haki na kwa uadilifu mkubwa.

Lakini wakati alipowasilisha ripoti bungeni na wakati mjadala umepamba moto wakidaiwa kutokutenda haki katika kazi yao ya kuchunguza, alisimama akasema kama watu hawaridhiki waombe kanuni zitenguliwe ili awasilishe upya ripoti yao ili aseme na siri waliyoificha ili kuiokoa serikali isiporomoke yote.

Sasa wakati akisisitiza kuwa walitenda haki wakati alisema kuwa kuna siri waliificha inakuwa vigumu kumuelewa huo uadilifu anaousema. Mimi namshauri Dr. Mwakyembe sasa aitoe hadharani ile siri waliyoificha kuepusha serikali kuporomoka yote na hivyo kupelekea serikali kuporomoka nusu kwa kujiuzulu kwa Mh. Lowassa.

Kwa sasa hakuna cha kupoteza Dr. kwasababu serikali iliyopo inaenda kuporomoka yenyewe kwa mujibu wa katiba hapo ifikapo mwezi Octoba. Hivyo wewe huna cha kupoteza na wala serikali iliyopo itakuwa haina cha kupoteza kwasababu uhai wake unaishia ukingoni. Bila kuisema hiyo siri uliyosema mliificha, suala la Richmond litabaki kuwa tata hadi ukamilifu wa dahari.

Tuliwagharimia kwa mamilioni mzunguke duniani kwenda kuutafuata ukweli. Nanyi mkafanya kazi yenu vizuri na kuupata ukweli wote. Mliporudi badala ya kutupa ukweli tuliowatuma, mkatupa ukweli nusu. Ukweli usiposemwa wote huo huwa hauwi ukweli kamili, na kwakuwa unakuwa haujasemwa wote, ndani ya huo ukweli nusu unaosemwa huwa kunakuwa kumechanganyika na uongo na uongo ukichukua nafasi kubwa maana nzima ya ukweli hupotea.

Hivyo ndivyo mlivyoipoteza maana nzima ya ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya Richmond kwani ukweli mkuu haukusemwa. Hiyo ilikuwa ni sawa na kumpa mgonjwa nusu dozi matokeo yake maradhi huwa sugu. Maradhi sugu tuliyoyapata ni kuzaliwa kwa ESCROW ambayo nayo haina tofauti sana na EPA na RADA. Ukiangalia maradhi yote hayo ni kutokana na kutotoa ukweli kamili.

Hivyo kama nawe ni mmoja wa watangaza nia, msalaba wako mkubwa itakuwa ni kuusema ukweli kwani ukweli humuweka mtu huru naye huwa huru kweli kweli. kwakuwa mpaka sasa unajaribu kujitetea bila kusema ukweli, itakuwa vigumu kwa watu wenye akili timamu kukuamini kwa lolote sana sana utaonekana ni mtu uliyetayari kuificha kweli kwa tamaa ya vyeo vipitavyo.

Ni dhahiri katika kuuficha huo UKWELI mtakuwa mliwaumiza watu wengine ambao hawakupaswa kuumia na kudharilika. Mlichokifanya kilikuwa sawa na kukivunja kichwa kwa kosa lililofanywa na ulimi - Ulimi uliponza kichwa, kichwa kikavunjwa bila sababu "NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO!"

Hao hao kina zi.ttto.!

Anasema nusu wananchi wanamuona shujaa ., anaficha nusu mafisadi wanamuona ni nyota ya jaha.!
 
na tafute jimbo lingine hata chalinze huku Kyela hatumtaki hata kumsikia!
 
Umeongea jambo la msingi sana.

Ni kweli wakati anawasilisha ripoti ya Richmond, akiwa Mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyochunguza ksshfa hiyo, alinukuliwa akihitimisha ripoti hiyo akisema kuwa kama kamati yake ingeamua kuanika hadharani kila lilichokiona wakati wa uchunguzi wake basi serikali iliyoko madarakani ingeweza kuanguka.

Sasa hapo ndipo linapojitokeza swali la msingi, ni kipi hasa kilichofichwa na kamati ya Mwakyembe, ambacho kilikuwa na lengo la kuiokoa serikali ya Sisiem isianguke?!

Hata mimi nilimsikia wakati akisema kwenye bunge lile la viwango na kasi ila kweli aisee inawezekana edo kuna kamchezo alichezewa ila kama anaujua ukweli wenzie walimwaga ugali na yeye si amwage mboga? Kisa cha kufa na kihoro nini.
 
Huu Uzi dr atajidai hajauona ila ile mingine inayomuelezea fitina zake kwa EL ndo anasomaga na kujidai kushitaki watu, sasa natoa tamko kabla hujashitaki watu jibu hoja hii nini ambacho unaficha kwenye sakata la Richmond
 
nilimtegemea sana mwakyembe ktk uraisi nimpe kura. ila umenikumbusha alivyowai. niuzi kwa jambo ilo. sasa sioni mwingine tena! daa! ok. nimekata shauli lasmi natangaza kwanzia sasa najiunga ukawa kwa kupitia chadema. peeeeeple's. kesho nachukua kadi.nipokeeni kwa mikono miwili.
 
Huyu Dr. Mwakyembe nae ni mchumia tumbo tu hana jipya, wakati yuko nje ya cabinet alikua mpiga kelele mzuri na watu wakaona kweli ni jembe, lakini baada ya kupewa cheo tu kimya.. Huu ni unafiki!! Kama kweli report ilikua ya kuiteteresha serikali basi serikali hii inaondoka aongee ule ukweli wa hio report.. Na Edo nae atakuja na upande wake ili wananchi wachuje chuya na mchele mchele au sio. Nilikua nataka CCM iendelee but kwa sasa NO nimebadili mwelekeo CCM wote wezi+mafisadi+ wanafiki... Tanzania inahitaji mabadiliko now!! UKAWA inatakiwa ichukue nchi kwa sasa, watu wamechoka kuona mafisadi wanabadilishana vijiti na kuvaa ngozi ya kondoo kumbe ni simba au chui.Wabongo wajifunze from Nigerians and Kenyans.
KAULi MBIU: wakati wa mabadiliko ni sasa chagua UKAWA!! CCM tupa kule!!
 
Na muda ukifika Edo atamwaga hiyo mboga na ameanza kwa kusema hausiki na richmond, na utakuta ni kweli anapakwa matope na ambao wanajua huyu jamaa akichukua nchi hata ukatibu tarafa hawataupata, mwakyembe umetumika kumchafua Lowassa wewe na kamati yako:what:
 
Baada ya leo mh.Lowassa kufunguki japo kwa ufupi kuhusu Richmond,naweza sema tu Mwakyembe ni wa kuogopa kama ukoma linapokuja swala la kutumika.
 
Kutumika vip?au unamaanisha kueleza ukweli aliousema Waziri Msabaha nje ya kiapo kuwa "richmond ni kampuni ya Waziri Mkuu na mshirika wake wa biashara yaan Rostam Aziz", Mwakyembe alisema abishe ili atoe data vizuri.
 
Back
Top Bottom