Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Status
Not open for further replies.
Hapa tunaposema 'conflict of interest', yaani 'mgongano wa kimaslahi', tunamaanisha kuwa huwezi kuwa kwenye mchakato wa kuingia dili na Tanesko alafu ukakubali kumchunguza mtu mwingine ambaye naye alikuwa kwenye mchakato wa kuingia dili na Tanesko. Hatusemi shujaa asiwe na kampuni yake japo Ujamaa ulio ndani ya mioyo yetu unatamani kuwe na Mwongozo wa kuzuia kuchanganya Biashara na Siasa. Ila tunasema unapokuwa na kampuni inayoshindana na kampuni nyingine kupata zabuni za Tenesko usifanye mambo Kiwaziri Kijana! Mheshimiwa kashasema sisi sio mabwege tena hivyo tuache ubwege wa kumtetea tu eti kwa sababu ya ushujaa wake dhidi ya Richmond - ushujaa ambao bado hatujaona matunda yake maana hakuna utekelezaji stahiki.

Once a hero not always a hero...

Companero hapo kwenye highlight ndipo bado hatujajua kama that was the case...Na kama ni hivyo usishangazwe wengi wetu tukabadili mawazo....Je Kampuni ya Mwakyembe ilikuwemo kwenye mchakato?
 
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania Toleo No. 4689 la tarehe 15 Machi 2009 chini ya kichwa cha habari "Dk. Mwakyembe Aumbuliwa" imeripotiwa kuwa Dk. Harrison Mwakyembe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kufua umeme na ndio sababu anaipiga vita kampuni ya Dowans ambayo ni mshindani wa kampuni yake.

(Taarifa inaendelea lakini ya muhimu kuhusu Dk. ni hayo)

Kuwa na kampuni si dhambi.
Tusichokitaka ni kampuni kuwa ya kitapeli.
Tatizo liko wapi?
 
Mimi nashangaa sana Shujaa Zitto kachemka watu kibao tumemvalia njuga. Sasa kuna kila dalili kuwa Shujaa Mwakyembe naye kachemka ila watu kibao tunanyanyua bango kumtetea bila hata kuziona taarifa kamili. Nasema hivi: Tuzisome taarifa kamili kutoka Brela n.k. tuone kama ni kampuni ya upepo au la na pia tuone kama alipaswa kulieleza Bunge kuwa kuna mgongano wa kimaslahi au la wakati wanamteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule. Hayo yote yatatusaidia kujua kwa nini Bunge linashindwa kuisimamia Sirikali ili iliue jinamizi la Richmond ikiwa ni mwaka zaidi ya mmoja toka Kamati Teule itoe maazimio/maagizo yake kwa Serikali kuhusu kutatua suala hili tete. Hali kadhalika itatusaidia kuujua ukweli wote kuhusu Richmond na Dowans ambao Kamati Teule iliuficha eti kwa maslahi ya 'umma/taifa'!

Mkuki kwa nguruwe mtamu...

Mkuu Companero

Ninakuunga mkono katika posting yako

Nadhani wana-JF wanakosa standards, badala ya kujadili issue tunaanza kumtetea mtu bila hata ya kuangalia kwa undani kama kunaweza kuwa na utata wowote hasa ukizingatia kuwa Mh. Mwakyembe has a vast knowledge ya migogoro ya wafuaji umeme. In fact alitakiwa aeleze kama na yeye ni mdau katika sekta hiyo ya ufuaji wa umeme. Endapo kama Mh Mwakyembe hakutamka lolote kuhusu uhusika wake katika ufuaji wa umeme basi ana jambo la kutueleza.

Kwa kuanzia, katika ile list ya wabia wenzake, kuna watu ambao Mh Mwakyembe amewataja kama watu ambao aliwahoji wakati wa uchunguzi wake wa kamati ya Richmond na kumpatia taarifa muhimu, je, hawa alieleza kuwa ni washirika wenzie kwenye biashara?

Pili, je hizo hisa zake au umiliki wake ali-declare kwenye ofisi za bunge kama mali anazomiliki?

Nafikiri kwa kuuliza haya na mengineyo ndiyo njia sahihi ya kumtendea haki Mh Mwakyembe, kumtetea bila kuhoji hakusaidii.
 
Nadhani kama kwa mkurugenzi wa maadili ya viongozi ....mwakyembe atakuwa ameweka wazi maslahi yake kwenye hii kampuni,hapo atakuwa amefanya vema kama atakuwa alifanya siri basi anakosa MORAL AUTHORITY ya kulisemea jambp hili kwa sababu itahesabika kuwa ana ajenda ya siri......
 
Companero hapo kwenye highlight ndipo bado hatujajua kama that was the case...Na kama ni hivyo usishangazwe wengi wetu tukabadili mawazo....Je Kampuni ya Mwakyembe ilikuwemo kwenye mchakato?

Kwani Tanesco ina dili moja? Hapa ishu ni entity inayotoa dili. Kama niko kwenye mchakato wa dili fulani na hiyo entity. Na wewe uko kwenye mchakato wa dili fulani na hiyo entity. Basi ni conflict of interest kwangu kukuchunguza wewe bila ku-declare interest. In that case that was the case.
 
Wakuu, ni vema tuangalie conflict of interest in-arise vipi kabla ya ku-conclude.
 
Philemon Mikael said:
wazee nyerere anaingiaje hapa ????,,nyerere alikuwa na mansion ..ipi hiyo...ile nyumba yake ya msasani si alikuwa amekopa THB na akapiga matofali kama watanzania wengine kwa mikono yake...

Philemon Mikael,

..ni kweli Mwalimu alijenga nyumba ya msasani kwa mkopo wa Benki.

..lakini kabla hajamaliza mkopo huo akaiuzia serikali na serikali ikamalizia mkopo.

..alipostaafu serikali ikamzawadia nyumba ile.

..now, you can continue.
 
Kwani Tanesco ina dili moja? Hapa ishu ni entity inayotoa dili. Kama niko kwenye mchakato wa dili fulani na hiyo entity. Na wewe uko kwenye mchakato wa dili fulani na hiyo entity. Basi ni conflict of interest kwangu kukuchunguza wewe bila ku-declare interest. In that case that was the case.

Ndio maana nikauliza kama kampuni ya Mwakyembe ilikuwa included kwenye mchakato ili tuweze ku justify conflict of interest...Huwezi kusema kuwa Mwakyembe alipinga ununuzi wa mitambo michakavu ya kampuni feki ili apewe hiyo contract na wakati kampuni yake haijawania ama haikuwania contract hiyo wakati wa mchakato...Wako waliosema Richmond ni powa wakati wa mchakato na ndio maana ilipewa baraka hizo za kuingiza mitambo chakavu licha ya wao kuwa kampuni feki,sasa je kampuni hiyo ya Mwakyembe nayo ilikuwa inawania? Ama mnakisia tu kwasababu ana share humo?
 
..........Pili, je hizo hisa zake au umiliki wake ali-declare kwenye ofisi za bunge kama mali anazomiliki?

Nafikiri kwa kuuliza haya na mengineyo ndiyo njia sahihi ya kumtendea haki Mh Mwakyembe, kumtetea bila kuhoji hakusaidii.

hapo tuko pamoja mkuu
 
Kuwa na kampuni si dhambi.
Tusichokitaka ni kampuni kuwa ya kitapeli.
Tatizo liko wapi?

Hakuna aliyesema ni dhambi. Hiyo ni mada ya 'Mwongozo' ambayo Mheshimiwa anaufagilia kuhusu kutenganisha Siasa na Biashara. Rudi kwenye hoja ya msingi.

Rejea mada zilizowasilishwa. Dhambi ni kuchunguza kijiti katika jicho langu kabla ya kutoa boriti katika jicho lako. Kesi ya fisi kutaka mfupa atapewaje mbwa mla mifupa?
 
Companero,
Hapa tunaposema 'conflict of interest', yaani 'mgongano wa kimaslahi' tunamaanisha kuwa huwezi kuwa kwenye mchakatao wa kuingia dili na Tanesko alafu ukakubali kumchunguza mtu mwingine ambaye naye alikuwa kwenye mchakato wa kuingia dili na Tanesko
Mkuu, ni mchakato gani ambao shirika la Mwakyembe limeingia dili sawa na hilo analolichunguza! (Richmond/Dowans)..
Sikiliza mkuu wangu...Askari Polisi hawezi kuchunguza au kuwa shahidi ktk kesi ambayo yeye mwenyewe anahusika au ana uhusiano mkubwa na mtuhumiwa..nikiwa na maana kama kweli Mwakyembe pia ali bet katika kufua umeme wa dharura ambao ulihitajio generator za gas au ana uhusiano wa karibu na Tanesco, Richmond/Dowans au mashirika yaliyokosa/kunyimwa tender ile....
lakini huwezi kumzuia Askari Polisi kumchunguza Polisi mwingine kwa sababu yeye ni Polisi, sababu iwe anategemea kupanda cheo (maombi aliyoweka) na kuwa ati kutakuwepo na Conflict of interest..
Mkuu kushindwa kwa Dowans au Richmond kahuwezi kumpa tender hiyo Mwakyembe (mgongano maslahi) na pia Mwakyembe hahusiki na tender au madudu yote yaliyotokea ndani ya mkataba wa dharura kiasi kwamba ukasema kuna mgongano wa kimaslahi iwe kiuchumi au kinadharia..Umeme wa Upepo vs Umeme wa generator kwa dharura ni two cases tofauti kabisa..
Chungwa na Embe, yote matunda lakini tofauti kabisa - yanayostawi sehemu tofauti na nyakati tofauti na mkuliwa wake ana kazi tofauti..Kisha walaji wanaweza kula matunda yote biola ulazima wa kuchagua..

Shirika la Mwakyembe limeingiza maombi yake ya kufua umeme kama mashirika yote yanayohusiana na kufua Umeme na Tanesco ndio wenye maamuzi na nguvu yote inayoweza kuzaa Mgongano wa Kimaslahi..

Ni utaratibu unaotakiwa kisheria laa sivyo huwezi kusambaza umeme nchini..Sasa mlitaka akaombe wapi kama sio Tanesco...
 
mimi nafikiri ni bora kuangalia ubora wa huu mradi wa umeme upepo...tukianza kuupiga vita kama kumkomoa mwakyembe tutakuwa tunajimaliza kimaendelea......hata mradi wa umeme wa dowans ..tuukatae kwa vigezo lakini tusitumie siasa..na tumeukataa...

mwelekeo wa nchi leo hii ni siasa na kukomoana ...na hii tabia ya visasi itatudumaza maendeleo..kwani tumeshakosa mradi wa kiwira kwa sababu za kisiasa kwani inajulikana wazi kuwa wawekezaji wenye mtaji kwenye mradi huu walikuwa wachina ..hawa anaben...ni local partner tu hawana mtaji wala technology......wawekezaji baada ya kuona vita vya maneno wamekimbia....

tutofautishe biashara ...kazi na siasa kwa mbali,siasa zetu mbaya...nashangaa kwakuwa wenzetu wakenya hawaingilii uwekezaji kwa sababu za kisiasa....mwanasiasa kuwa na hisa kwenye kampuni isiwe sababu ya kuihukumu kampuni..
 
Hivi mkikuta kampuni yenyewe hata ku-operate haija-operate na kwamba labda iko tu kwenye makabrasha ya BRELA.

Haya endeleeni na mjadala wenu mwaya.
 
Kasheshe,
Sio wakikuta.. Ukweli ni kwamba kampuni hiyo ipo ktk makabrasha na sasa hivi wameanza kuwachimba wote wale wanaopingana na Rostam/Lowassa..Nia yao ni kuwamaliza Kisiasa na kiuchumi lakini this time wamegota!
Wanahaha wanatapatapa utafikiri wafa maji........Na bado!
 
Lets be fair and objective here, maana naona zile za hatuamini na Utomaso zinaweza kutupofusha kabisa na kuanza kuwa washabiki kama wa Simba ambao hata kama Yanaga wakicheza vizuri, wao kwao Yanga ni bomu.

Swali la kujiuliza, je Kampuni ya Mwakyembe ilianzishwa lini na Mwakyembe ameshatoa taarifa Bungeni na Serikalini katika ile tume ya maadili kuwa ana hisa kwenye kampuni ya kufua umeme?

Sasa tukishatoka hapo, ndipo tuje kwenye nafasi ya Mwakyembe kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge kuhusiana na suala la Richmond. Kama wakati wa sakata la Richmond, MWakyembe tayari alishakuwa mmiliki wa hii kampuni ya umeme wa upepo, basi hakustahili kuwa Mwenyekiti wa Kamati hii na alipaswa kumfuata Spika na kujitoa ili kulinda integrity ya kamati na credibility yake. Hasara ya yeye kushindwa kujitoa kwenye hili la Riuchmond ndilo linaloleta ile picha ya Conflict if Interest!

Naona tuliliona sana suala la Conflict if Unterest wakati wa Mkapa mna Yona na Kiwira yao, lakini hapa tunataka lifumbia macho na kutoa visababu tuu kadhaa maana Mwakyembe kafanya kile tulichofurahia nacho ni kumvunja nguvu mtu ambaye tulikuwa hatumpendi (lowassa na wenzake).

Kama kweli Mwakyembe alikuwa mmiliki na mwenye hisa katika kampuni hii wakati wa uchunguzi wa Richmond, hadhi na heshima ya Mwakeyembe kama mtu muadilifu, mfuata kanuni na sheria na mwenye kuwa mkweli inashuka na kuwa na madoa kwa kuwa kila alichokisema tangu wakati ule na mpaka sasa kitaonekana kuwa ni cha upendeleo kumchafulia jina mshindani mwenzake wa kibiashara (richmond) hata ka ni kweli kuwa Richmond na Dowans walikiuka mengi na walihusika na Rushwa.

Nitamtetea mwakyembe ikiwa itabainika kuwa yeye kawa mmiliki na mwenye hiswa wa hii kampuni mpya ya umeme tangu jana au leo hii. Sababu ya kusema hivyo ni kutokana na kauli zake za hivi karibuni kuhusu na Dowans ambazo ni wajibu wake kuzisema kama mlinzi na mteteaji wa maslahi ya Taifa.

Lakini kama nilivyoisema awali, kitendo cha yeye Mwakyembe kutokutoa taarifa mapema kwetu wananchi au kabla ya kuanza kuzungumzia suala la Richmond/Dowans kuwa naye ana kampuni ya uzalishaji umeme, kinaonyesha kuwa Mwakyembe anatumia vibaya nafasi yake ili kuhakikisha kuwa kampuni yake inakuwa na ushindani dhaifu au mdogo kwa kukata mapanga washindani wengine!
 
Mkandara 'usinilishe' maneno. Nasema hivi: Kama kampuni A ilikuwa katika mchakato wa kutafuta Dili A kwa Tanesko. Na Kampuni B ilikuwa katika mchakato wa Kutafuta Dili B kwa Tanesko. Je, ni halali kwa mtu mwenye hisa kwenye Kampuni A kuichunguza Kampuni B kuhusiana na Dili B? Na, je, uchunguzi wake ukionesha kuwa Kampuni B ni ya ufisadi huoni atakuwa amempunguza mshindani mmojawapo katika soko la umeme. Pia atakuwa amejitengenezea fursa ya kutafuta Dili B pale 'wananchi watakapoamua baada ya kuwa na giza nchini, mahospitali kushindwa kutoa huduma, viwanda kushindwa kuzalisha na wanafunzi kushindwa kusoma kutokana na kukosekana na kwa umeme kwa kuwa hatukuchukua hatua'?

Kasheshe suala sio ku-operate. Kwani Richmond ili-operate? Suala ni, je, kampuni yake ilisajiliwa Brela na, je, ilianza mchakato wa kupata Dili fulani za Tanesko kabla ya 2008?

JMushi acha kujifanya u mgumu kuelewa- kuna aina tofauti za 'conflicts of interest'. Hapa tunazungumzia ile ya kumchunguza mtu ambaye ana interests kama zako bila kusema wazi kabisa kuwa na wewe una interests za aina hiyo. Au alisema wazi bungeni kwa mujibu wa kanuni za Bunge?
 
tafadhali dont judge the book by its cover...habari hii kama imetoka mtanzania ambalo rostam ana interest haifanyi habari hii kulaumiwa tu kwa sababu ya mchapishaji nani...hata ingeandikwa na mzalendo au nipashe ....muhimu kuangalia kama ni ya kweli au la......

nadhani kama ni kweli ...na mwakyembe kama mwanasheria atakuwa hakumueleza spika interest yake kwenye kampuni ya nishati wakati anachaguliwa kuwa kwenye kamati ...na hasa kama kwa idara ya maadili hakutaja kwenye fomu ya ku declare mali zake ....basi that will be a mistake..

but as i said ....tuache siasa kwenye biashara....
 
Mkandara 'usinilishe' maneno. Nasema hivi: Kama kampuni A ilikuwa katika mchakato wa kutafuta Dili A kwa Tanesko. Na Kampuni B ilikuwa katika mchakato wa Kutafuta Dili B kwa Tanesko. Je, ni halali kwa mtu mwenye hisa kwenye Kampuni A kuichunguza Kampuni B kuhusiana na Dili B? Na, je, uchunguzi wake ukionesha kuwa Kampuni B ni ya ufisadi huoni atakuwa amempunguza mshindani mmojawapo katika soko la umeme. Pia atakuwa amejitengenezea fursa ya kutafuta Dili B pale 'wananchi watakapoamua baada ya kuwa na giza nchini, mahospitali kushindwa kutoa huduma, viwanda kushindwa kuzalisha na wanafunzi kushindwa kusoma kutokana na kukosekana na kwa umeme kwa kuwa hatukuchukua hatua'?

Kasheshe suala sio ku-operate. Kwani Richmond ili-operate? Suala ni, je, kampuni yake ilisajiliwa Brela na, je, ilianza mchakato wa kupata Dili fulani za Tanesko kabla ya 2008?

JMushi acha kujifanya u mgumu kuelewa- kuna aina tofauti za 'conflicts of interest'. Hapa tunazungumzia ile ya kumchunguza mtu ambaye ana interests kama zako bila kusema wazi kabisa kuwa na wewe una interests za aina hiyo. Au alisema wazi bungeni kwa mujibu wa kanuni za Bunge?

Mkuu Companero nilichokuwa nikihitaji kujuwa ni kama kampuni hiyo ya Mwakyembe ilikuwa kwenye ushindani na Dowans wakati wa kuwania ununuzi wa mitambo hiyo. Na pia,Je alipoteuliwa kwenye kamati hiyo ya uchunguzi alikuwa tayari ana own kampuni hiyo ya kufua umeme? Mbona ni swali simple tu mkuu? Maana unavyozungumza ni kama ume confirm kuwa that is the case.
 
Thread ipo speed mpaka nashindwa ku-catch up na speed yake. Nasubiri ipoe nisome tangia mwanzo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom