Wachunguzi wa mambo wanaamini kuwa ushujaa wa Dk. Mwakyembe kuishambulia kampuni ya Richmond, na baadaye Dowans, unatokana na mgongano wa kimaslahi.
Kwa maneno mepesi, wanasema Dk. Mwakyembe na wenzake wanapinga Dowans kununuliwa ili wapate mwanya wa kuuza umeme utakaozalishwa na kampuni yao ya Power Pool East Africa Limited, ingawa nao kwa vyovyote vile utakuwa haujatosheleza mahitaji ya umeme nchini.
Dk. Mwakyembe na wenzake walianzisha kampuni yao kabla ya ujio wa kampuni iliyozua utata mkubwa wa Richmond. Matarajio yao yalikuwa kwamba wazalishe umeme na kisha waiuzie Tanesco, lakini ujio wa Richmond ulionekana kutaka kuwakwaza. Richmond ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ajiuzulu Februari mwaka jana.
Akiwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, hakuwahi kutangaza hata mara moja mgongano wa kimaslahi aliokuwa nao kwenye suala hilo.
Pamoja na Dk. Mwakyembe anayemiliki hisa 1,485 katika kampuni hiyo, wengine wenye hisa katika kampuni hiyo ni Emmanuel Kasyanju (99), Victor Mwambalaswa (99), Mwacha Kagoswe (4,455), Josephine Pina (99), Athumani Ngwilizi (99), Prosper Tesha (99), TBC (199 Limited inayomilikwa na Isaac Mwamango (297) na MECCO Limited, inayomilikwa na Maungo Kwabibi hisa moja.
Wakuu nadhani sote sisi ni Wabongo na wepesi sana wa kussoma alama inapofikia hali kama hii...
Ukisoma kwa makini maelezo ya gazeti hili utaelewa kabisa kwamba hii ni njama nzito sana yenye malengo mabaya kwa Mwakyembe na sio shirika husika..
Kwanza, Hilo shirika la Mwakyembe hata kama lipo linafua Umeme kwa njia ya Upepe jambo ambao halikuwepo ktk mpango wa dharura..
Pili maeneo yanayozungumziwa hayahusiani kabisa na sehemu ambazo Richmond au Doiwans walitakiwa kuwekeshaji..
Tatu, shirika hili halipo ktk list za mashirika yaliyoomba tender ya ushindani ktk mchakato wowote ule unaowashirikisha Richmond na Dowans..
Kwa hiyo ukisoma habari hii utagundua kwamba imepambwa sana kuonyesha ubaya wa Mtu badala ya mapungufu ya shirika husika ktk ufuaji umeme..Labda kwa taarifa yao hawa vibaraza wanatakiwa kufahamu kwamba wananchi wanagomba na Richmond/Dowans kama mashirika yenye mpango wa ufisadi sio swala la Ushindani.. Issue kwetu sisi wananchi ni UFISADI sio swala la Uwekezaji ktk nguvu za umeme na nani mmiliki wa shirika fulani..Kila kiongozi nchini ana shirika au amenunua hisa ktk mashirika ya uzalishaji iweje issue hii igeuzwe toka UFISADI hadi kuwa nani kawekeza sehemu fulani..
Na kibaya zaidi ktk Unafiki wa watu hawa, gazeti hili limeweza kutaja kwa asilimia hisa zote za wamiliki wa shirika hili lakini wameshindwa kutupa mhisa hata mmoja (Mtanzania) ktk wamiliki wa Richmond au Dowans zaidi ya kutufunga kamba..
Mohammed Gire alikuwa CEO wa Richmond kulingana na taratibu za uongozi, CEO ni mwajiriwa sio lazima awe mmiliki wa hata asilimia moja..tunafahamu jinsi walivyomtumia Gire kama kawaida yao wanapowatumia watu kama Manji na wahindi wengine wezi kama wao...
Sasa nachotaka gazeti hili wafanye ni watupe wamiliki wa Dowans kwa utaratibu uliotumika kumuumbua Mwakeyembe kama wanavyodai..
Kutokana na kifo cha azimio la Arusha, miiko ya viongozi yote imeondolewa na Mwakyembe hana tofauti kabisa na viongozi wengine ktk uwekezaji na hakika binafsi napongeza sana kiongozi kama Mwakyembe ambaye kawekesha ktk muundombinu muhimu sana kwa Taifa letu from scratch..
Dr. Mwakyembe, kwa habari kama hizi mkuu tunakupongeza sana na hakika Tanzania inataka viongozi kama huyu ambaye binafsi amejikita ktk mradi mkubwa kama huu kisheria pamoja na kwamba hana uwezo mkubwa kam hao majambazi kina Rostam/Lowassa....